Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Maelfu ya wapalestina washikiliwa na mamlaka za Israeli bila kujulikana waliko
    Hii leo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imechapisha ripoti kuhusu mamlaka za Israeli kukamata wapalestina kiholela na kwa muda mrefu tangu mwezi Oktoba mwaka jana akiwemo mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 80 mwenye ugonjwa wa kusahau. Assumpta Massoi amepitia ripoti hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo. (Taarifa ya Assumpta Massoi)Ripoti ni ya kurasa 23 ikiweka bayana machungu wanayopitia wale wanaoshikiliwa na Israeli,  halikadhalika ikinyooshea mkono vikundi vilivyojihami vya kipalestina, ikiwemo Hamas ambao wanashikilia mateka wa Israeli tangu vita ianze Oktoba 7 mwaka jana.Wapalestina walikamatwa wakati wamesaka hifadhi kwenye shule, hospitail, nyumbani au kwenye vituo vya ukaguzi wakati idadi kubwa ya wapalestina walikuwa wanahama kutoka kaskazini mwa Gaza kuelekea kusini.Miongoni mwao ni mwanamke huyo wa umri wa zaidi ya miaka 80 pamoja na wasichana, wavulana, na wanaume wasiohusiana na vikundi vilivyojihami.Jeremy Laurence, Msemaji wa Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu anasema, ripoti inajumuisha madai ya kuteswa na kutendewa vibaya na aina nyingine za ukatili. Mahabusu wanashikiliwa kwenye maeneo kama vizimba, wanavuliwa nguo zote na kuachwa na nguo ya ndani pekee kwa muda mrefu, mbwa wakiachiliwa wawang’ate, wananing’inizwa kwenye dari na pia kuna ripoti za ukatili wa kijinsia na kingono wanapokuwa wanashikiliwa.”Mamlaka za Palestina kwa upande wake zimeripotiwa kukamata kiholela watu huko Ukingo wa Magharibi ili kuzuia kukosolewa na upinzani wa kisiasa.Bwana Laurence anasema sheria ya kimataifa inataka wale wanaoshikiliwa  watendewe kiutu na kibinadamu na inakataza mateso au aina nyingine ya ukatili.Hivyo anasema, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu. Volker Türk, anasisitiza wito wake wa kuachiliwa mara moja kwa mateka wote wanaoshikiliwa Gaza. Wapalestina wote wanaoshikiliwa kiholela na Israeli lazima waachiliwe huru.Kamishna Mkuu Türk  ametaka pia uchunguzi wa haraka, huru na wa kina wa matukio yote yaliyosababisha ukiukwaji wa sheria ya kimataifa, na kuhakikisha wahusika wanawajibishwa na kwamba manusura na familia zao wapatiwe haki yao ya fidia. TAGS: Haki za binadamuAdditional: Amani na UsalamaNews: Gaza, Palestina, IsraeliRegion: Mashariki ya KatiUN/Partner: OHCHR
    2 min
  • 31 Julai 2024
    Hii leo katika jarida la Umoja wa Mataifa Leah Mushi anakuletea taarifa mbalimbali ikiwemo ripoti kuhusu mamlaka za Israeli kukamata wapalestina kiholela na kwa muda mrefu tangu mwezi Oktoba mwaka jana, juhudi za UNAIDS kuelimisha vijana nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR jinsi ya kujikinga na UKIMWI. Makala utasikia kuhusu ufugaji nzi weusi kwa ajili ya chakula cha mifugo na mashinani utasikia jinsi UNICEF inavyosaidia jamii huku Timbuktu nchini Mali kupambana na utapiamlo hususan kwa watoto. 
    10 min
  • 30 JULAI 2024
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Fora Nducha anakuletea-Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA linasema watoto wengi  wako hatarini kuambukizwa ugonjwa wa homa ya ini aina ya A -Venezuela ambako kulifanyika uchaguzi wa Rais Jumapili,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza azma ya wananchi kwa kuelezea utashi wao kwa amani kupitia sanduku la kupigia kura-Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO inasema msichana barubaru 1 kati ya 6 waliokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi mwaka jana, alikumbwa na ukatili wa kimwili au kingono kutoka kwa mpenzi wake-Katika mada kwa kina tuko Jamhuriya Kidemkrasia ya Congo DRC ambako shirikala mpango wa chakula duniani WFP laleta nuru kwa wakimbizi  wa ndani Magina-Na mashinani katika kuadhimisha siku ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu duniani utapata ujumbe kutoka kwa IOM Khazakstan kuhusu  jinsi ya kuzuia usafirishaji haramu wa watoto kupitia mtandao
    10 min
  • Mkimbizi Sudan Kusini atumia stadi za ujasiriamali kuhudumia familia yake
    Zaidi ya watu 1,000 wanaokimbia vita nchini Sudan wanavuka mpaka na kuingia nchini Sudan Kusini kila siku, na hivyo kuvipatia shinikizo vituo vya mpito vilivyoko mji wa mpakani wa Renk nchini Sudan Kusini. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema idadi kubwa ni wakimbizi wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani ambao wamekuwa wakiishi Sudan tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao Sudan Kusini. Miongoni mwao ni Juma Peter Gai ambaye yeye na familia yake sasa wameamua kusalia Renk. Mapito na changamoto zao ndio msingi wa makala hii inayowasilishwa kwako na Assumpta Massoi.
    4 min
  • WFP yasaidia wakulima nchini Kenya kuchangamkia kilimo biashara
    Jitihada za kujikomboa na janga la njaa bado zinaendela nchini Kenya, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kupitia kituo cha huduma kwa wakulima likiwapa wakulima elimu ya namna sahihi ya kuongeza uzalishaji licha ya changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo na hasa kwa kukumbatia kilimo biashara.(Taarifa ya Bosco Cosmas)Kilimo ni uti wa mgongo kwa jamii nyingi sana za Afrika, ndivyo ilivyo katika nchi ya Kenya ambapo wakulima wamekuwa wakipitia changamoto kubwa ya uzalishaji kutokana na majanga ya asili yanayoendelea nchini humo ikiwemo mafuriko.Shirika la WFP kupitia mpango wake wa huduma kwa wakulima, limeweza kumsaidia mkulima Farah ambaye hapo awali alikumbana na uzalishaji hafifu kwaajili ya matumizi ya chakula na sasa amehimizwa kwenda mbali zaidi ya mlo wa kila siku kwa kuingia katika kilimo biashara.Uelewa wa kilimo biashara si mkubwa lakini Farah, anasimama kidete huku akionesha nita yake ya kuondoa njaa.(CUT, FARAH )“Lengo langu ni kuboresha uhakika wa chakula katika nyumba yangu, cha pili ni kuingia kwenye biashara, cha tatu kuondoa njaa nchini Kenya.”WFP kupitia mradi wake, imeweza kubadili fikra za Farah kuhusu kilimo(CUT, FARAH )“Tangu nilipozaliwa, nilikuta baba yangu akifanya shughuli za kilimo lakini sio cha kisasa, lakini mwaka jana baada ya WFP kutambulisha mpango mpya wa huduma kwa wakulima imesaidia kutuinua. Tulikuwa hatufanyi kilimo kama biashara kwa sababu tulikuta baba zetu wanafanya hivyo.”Katika mradi huo WFP inafanya kazi kwa kushirikiana na wadau wa kilimo ili kuimarisha uhakika na uzalishaji wa mazao kwa ajili ya lishe bora na kusaidia wakulima sio tu kuweka mlo mezani bali kilimo pia kuwaingizia fedha kwa kukigeuza kuwa kuwa biashara.
    3 min
  • Watu 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa katika mashambulizi Al- Fasher Sudan, UN yalaani vikali
    Takriban raia 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kwenye mashambulizi katika hospitali, maeneo ya makazi na soko la mifugo kwenye Jiji la Al Fasher katika Jimbo la Darfur Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami. Flora Nducha na taarifa zaidi(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Asante Leah katika taarifa hiyo aliyoitoa mjini Port Sudan Nkweta- Salami amelaani vikali muaji hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki . Amesema "Nimehuzunishwa sana na mashambulizi haya ya kutisha dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia kama vile hospitali, nyumba na masoko. Miundombinu ya kiraia haipaswi kamwe kulengwa na inalindwa chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu. Umoja wa Mataifa nchini Sudan unalaani vikali mashambulizi haya ya kiholela na tunatuma rambirambi zetu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.”Ameongeza kuwa mashambulizi hayo ya Al Fasher yamewashtukiza watu kwani mji ulikuwa umetulia kwa karibu wimbi mbili hali iliyoruhusu masoko kufunguliwa na familia nyingi kuendelea na maisha.Kurejea kwa hali ya kuweza kutafuta riziki kwa watu na shughuli nyingine za kiuchumi, ufikishaji wa msaada wa kibinadamu usiozuiliwa na ongezeko la ufadhili wa kibinadamu ni muhimu kwa Sudan ili kuepusha tishio linalokuja la njaa. Amesema Nkweta- Salami.Ameendelea kusema kuwa nchi hiyo inakabiliwa na viwango vibaya zaidi vya uhaba wa chakula katika historia yake, huku zaidi ya nusu ya wakazi wake sawa na watu milioni 25.6 wakiwa na njaa kali, wengine milioni 8.5 wanakabiliwa na viwango vya dharura vya njaa na wakati zaidi ya watu 755,000 wako katika hali ya janga katika majimbo  ya Darfur, Kordofan Kusini na Kaskazini, Blue Nile, Al Jazirah, na Khartoum.Tangu kuzuka kwa mzozo mpya Aprili mwaka jana zaidi ya watu 18,800 wameuawa, zaidi ya 33,000 kujeruhiwa na watu zaidi ya milioni 10 wamezikimbia nyumba zao na miongini mwao zaidi milioni 5 wakivuka mpka na Kwenda kusaka usalama nchi  za jirani.Nkweta-Salami ametoa wito kwa pande zote katika mzozo huo kukomesha mapigano mara moja na kuwalinda raia kwa gharama yoyote.
    2 min
  • 29 JULAI 2024
    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akiangazia shambulio huko Sudan, kilimo biashara nchini Kenya. Makala inakupeleka Sudan Kusini harakati za mkimbizi aliyefurushwa mara mbili na sasa amerejea nyumbani na mashinani ni huko Paris Ufaransa kunakofanyika michezo ya olimpiki ya majira ya joto.Takriban raia 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kwenye mashambulizi katika hospitali, maeneo ya makazi na soko la mifugo kwenye Jiji la Al Fasher katika Jimbo la Darfur Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami. Flora Nducha na taarifa zaidiJitihada za kujikomboa na janga la njaa bado zinaendela nchini Kenya, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kupitia kituo cha huduma kwa wakulima likiwapa wakulima elimu ya namna sahihi ya kuongeza uzalishaji licha ya changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo na hasa kwa kukumbatia kilimo biashara.Makala: Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR anakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia mkimbizi aliyelazimika kurejea nyumbani baada ya vita kuzuka nchini Sudan mwezi Aprili mwaka jana wa 2023.Mashinani: Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake (UN Women) Sima Bahous, akitoa kauli yake kuhusu kuwatambua na kuwapa fursa sawa wanariadha wa kike. Karibu!
    10 min
  • Perina Nakang alenga kushinda Olimpiki kuinua timu na familia yake
    Perina Nakang, ni mmoja wa wanariadha 37 wanaounda timu thabiti ya wakimbizi kwenye michezo ya Olimpiki iliyoanza leo Julai 26 huko Paris, Ufaransa. Familia yake ilikimbia Sudan Kusini kwa sababu ya vita yeye akiwa na umri wa miaka 7 na kufika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Sasa ana umri wa miaka 21, akikimbia mbio za mita 800 ambapo katika mazoezi alimaliza kwa muda wa dakika 2 na sekunde 12 na lengo lake ni kufikia muda wa dakika 2 na sekunde 10. Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na UNHCR anamulika safari yake ya mazoezi na ndoto yake Perina.
    4 min
  • Guterres: Pongezi IOC kwa kuendelea kujumuisha wanariadha wakimbizi kwenye Olimpiki
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Paris Ufaransa kuhudhuria ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 amezungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach na kuipongeza kamati hiyo kwa kuendelea kuwajumuisha wakimbizi wanamichezo. Flora Nducha amefuatilia hotuba hiyo na kuandaa ripoti ifuatayo.Hakika Leah! Hotuba ya Katibu Mkuu imeoanisha michezo ya Olimpiki na amani na jinsi ilivyoweza kuwapatia fursa wanamichezo waliofurushwa makwao kutokana na vita kuweza kuonesha vipaji vyao kwenye michezo hiyo.Guterres amesema napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kile ambacho Kamati hii ya Olimpiki imefanya kwa kuruhusu timu ya wakimbizi kushindana kwa mara nyingine tena kwenye michezo ya Olimpiki.Amesema yeye alikuwa Kamishna Mkuu wa wakimbizi kwa miaka 10 na ni muhimu sana kutomwacha mtu yeyote nyuma, na zaidi kutowaacha nyuma wale waliolazimika kukimbia, kuacha nchi zao na wana haki sawa ya kushiriki michezo kama raia wengine wa dunia.Amezungumzia pia umuhimu wa nchi zilizo kwenye mizozo kuzingatia sitisho la kwanza kabisa la mapigano wakati wa michezo ya Olimpiki karne ya 8 huko Ugiriki ili kuepusha mashambulizi wakati wa michezo.Guterres amesema tunaishi katika dunia iliyogawanyika, ambako mizozo inaendelea kwa kiasi kikubwa kuanzia Ukraine hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Hivyo amesema katika zama kama hizo, ni muhimu kusema kuzingatia sitisho hilo la mapigano la kwanza duniani.Amesisitiza kuwa michezo ya Olimpiki inapoanza ni wakati wa kukumbusha dunia kuzingatia sitisho hilo la mapgano ili kuifanya dunia itambua umuhimu wa kunyamazisha silaha.Katibu Mkuu ametaka nchi zote duniani zishikamane pamoja kama ilivyo kwa wanamichezo wa Olimpiki ambao wanacheza  bila kujali tofauti zao.Michezo ya olimpiki ya majira ya joto inaanza Julai 26 hadi tarehe 11 Agosti, ikifuatiwa na ile ya watu wenye ulemavu itakayoanza tarehe 28 Agosti hadi tarehe 8 Septemba nchini Ufaransa
    2 min
  • 26 Julai 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ufunguzi wa michezo ya Olimpiki na Jitihada za pamoja za kukabiliana na changamoto za afya ya umma barani Afrika. Makala tutasalia nchini Paris katika michezo ya Olimpiki na mashinani tunasikia mafunzo kushusu ulemavu wa kutosikia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Paris Ufaransa kuhudhuria ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 amezungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach na kuipongeza kamati hiyo kwa kuendelea kuwajumuisha wakimbizi wanamichezo.Jitihada za pamoja za kukabiliana na changamoto za afya ya umma zinazidi kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma za afya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika kwa kushirikiana na nchi wanachama na washirika wake linaendelea kutimiza ajenda yake ya mabadiliko ili kuimarisha mifumo ya afya na kuongeza misaada kwa nchi katika ukanda wa Afrika.Makala inamulika mmoja wa wanariadha wanaowakilisha timu ya wakimbizi kwenye michezo ya olimpiki iliyoanza leo Paris, Ufaransa. Safari yake na matumaini yake akilenga kukimbia mbio za mita 800 kwa dakika 2 na sekunde 10 badala ya dakika 2 na sekunde 12.Na mashinani Dkt. Kaitesi Batamuliza Mukara, Mshauri wa masuala ya masikio, kusikia na uangalizi wa macho kutoka Ofisi ya kikanda barani Afrika ya Shirika la Afya Duniani, WHO akieleza juhudi za shirika hilo za kusaidia watu wenye changamoto ya kusikia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners