Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Madaraja yaliyojengwa na UNMISS yaondolea adha wananchi nchini Sudan Kusini
    Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefadhili ujenzi wa madaraja matatu huko Yubu, Turbiwa na Bundri kwenye kaunti  ya Tambura jimboni Equitoria Magharibi. Lengo la ujenzi huo kupitia miradi ya matokeo ya haraka au QIPs, ni kurahisisha kurudi nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi waliofurushwa makwao.Madaraja hayo matatu yanalenga kuwaunganisha watu, kuimarisha mshikamano wa kijamii, na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, shule, na masoko halikadhalika utekelezaji wa jukumu la ulinzi wa raia.Benina Mbiko, mama wa watoto watano, anaamini kwamba daraja hilo litaongeza biashara na hivyo kuinua uchumi na zaidi ya yote..."Kwetu sisi tulio kijijini, huwa ni vigumu kuja mjini wakati wa msimu wa mvua kwa sababu maji yanapokuwa mengi, hatuwezi kuvuka mto. Daraja hili ni zuri sana, asante kwa wale waliojitokeza kutujengea."  Kwa wengi, miundombinu mipya inayonufaisha jamii nzima ni ishara ya maendeleo yanayokuwa kama anavyoeleza Chifu Mkuu wa Kijiji cha Tambura, Mboribamo Renzi.Anasema daraja hili litasaidia jamii kwa jumla katika nyanja za kilimo, kusafirisha bidhaa zao hadi sokoni, kurahisisha usafiri wa wagonjwa kutoka vijijini hadi mjini, kuimarisha usalama;  na haya yote ni sehemu ya maendeleo.”Kwa upande wake, Mwakilishi wa UNMISS, Anthony Moudie, alisisitiza athari chanya za mradi kama huu akisema..‘‘Daraja hili litasaidia au kurahisisha ulinzi wa raia wa pande zote mbili. Litasaidia serikali kupeleka vyombo vya usalama kuhakikisha kuwa raia wanakuwa salama. Pia, daraja hili litafanikisha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa pande zote mbili.’’UNMISS imesema itaendelea kufadhili baadhi ya  miradi midogo inayodhaniwa kuwa na uwezo wa kuboresha kwa kiasi kikubwa maisha ya jamii za maeneo ambako miradi hiyo inatekelezwa.
    3 min
  • 24 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti mpya ya Hali ya Uhakika wa Chakula na Lishe Duniani SOFI, na miundombinu yanayofadhiliwa na UNMISS nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Chad, kulikoni?Takriban watu milioni 733 walikabiliwa na njaa mwaka 2023, hii ikiwa ni sawa na mtu 1 kati ya 11 duniani na mtu mmoja kati ya watano barani Afrika, kulingana na ripoti mpya ya Hali ya Uhakika wa Chakula na Lishe Duniani SOFI, iliyochapishwa leo na mashirika matano ya Umoja wa Mataifa.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefadhili ujenzi wa madaraja matatu huko Yubu, Turbiwa na Bundri kwenye kaunti  ya Tambura jimboni Equitoria Magharibi. Lengo la ujenzi huo kupitia miradi ya matokeo ya haraka au QIPs, ni kurahisisha kurudi nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi waliofurushwa makwao.Makala inatupeleka mkoa wa Singida ulioko katikati mwa Tanzania kumsikia mnufaika wa mafunzo kilimo cha viazi lishe yaliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini humo. Mnufaika huyo ambaye atajitaja jina lake, anazungumza akiwa katikati ya shamba lake la matuta ya viazi lishe.Na katika mashinani ikiwa tangu mwezi Aprili mwaka jana wa 2023, zaidi ya watu takribani laki 5 wakiwemo watoto zaidi ya laki 3 wamekimbia Sudan na kuvuka mpaka na kuingia Chad, mmoja wao ni Roumaiza, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 ambaye anaeleza matumaini anayoyapata sasa katika kambi ya wakimbizi nchini Chad ambayo inahudumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na wadau wengine.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • UN Ripoti SOFI: Watu takriban milioni 733 walikabiliwa na njaa 2023
    Takriban watu milioni 733 walikabiliwa na njaa mwaka 2023, hii ikiwa ni sawa na mtu 1 kati ya 11 duniani na mtu mmoja kati ya watano barani Afrika, kulingana na ripoti mpya ya Hali ya Uhakika wa Chakula na Lishe Duniani SOFI, iliyochapishwa leo na mashirika matano ya Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo ya kila mwaka iliyozinduliwa nchini Brazili katika mkutano wa mawaziri wa nchi 20 zenye kipato cha juu duniani  au G-20 imeonya kwamba  dunia iko mbali sana kufikia lengo la 2 la Maendeleo Endelevu, la kutokomeza njaa, ifikapo mwaka 2030.Pia inafichua kwamba dunia imerudi nyuma miaka 15, huku viwango vya utapiamlo vikilinganishwa na vile vya mwaka  2008-2009.Ripoti inasema licha ya maendeleo kiasi yaliyopigwa katika maeneo maalum kama vile kudumaa na kunyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee, viwango vya njaa duniani vimedorora kwa miaka mitatu mfululizo, na mwaka 2023, kulikuwa na watu milioni 152 zaidi wenye utapiamlo kuliko mwaka 2019.Kwa mmujibu wa mashirika matano ya Umoja wa Mataifa yaliyoandaa ripoti hiyo lile la chakula na kilimo FAO, la mpangowa chakula duniani WFP, la ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD, la kuhudumia  watoto UNICEF na la afya duniani WHObara linaloongoza kwa ongezeko la watu wenye njaa ni Afrika kwa asilimia  20.4, Asia  asilimia 8.1 na Amerika ya Kusini asilimia 6.2.Ripoti hiyo imegawanyika katika  sehemu tatu: Mosi viasharia vya njaa ambapo inasema upatikanaji wa chakula unaendelea kuwa mtihani kwa mamilioni ya watu, ukosefu wa fursa za kiuchumi za kupata mlo kamili ni changmoto kubwa ,watoto kuzaliwa na uzito mdogo na kudumaa ni matatizo sugu na katika muongo uliopita kumekuwa na ongezeko kubwa  la utipwatipwa.Pili  imetaja sababu za ongezeko la njaa kuwa ni  mfumuko wa bei, vita na mabadiliko ya tabianchi.Na tatu nini kifanyike: Ripoti inapendekeza uwekezaji ili kufadhili kukomesha njaa, uhaba wa chakula na aina zote za utapiamlo.Na imeonya kwamba ikiwa hali ya sasa itaendelea, takriban watu milioni 582 watakuwa na utapiamlo sugu ifikapo 2030, nusu yao wakiwa barani Afrika.
    2 min
  • 23 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika maoni ya vijana kuhusu SDGs, mmoja wao ni Monicah Malith Mkimbizi nchini Kenya kutoka Sudan Kusini akieleza alichotoka nacho kwenye mkutano wa HLPF. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imelaani ukimbizi wa mara kwa mara utokanao na amri za kuhama zinazotolewa na jeshi la Israeli dhidi ya raia huko kaskazini mwa Khan Younis, Ukanda wa Gaza.Barani Afrika, mashambulizi mapya yanayofanywa na vikundi vilivyojihami dhidi ya raia huko mashariki mwa Burkina Faso yamelazimu maelfu ya watu hao kukimbilia nchi jirani ya Niger ili kusaka usalama, wakati huu ambapo hali ya dharura inazidi kushamiri kwenye taifa hilo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.Na hatimaye michezo ya olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 inaanza Ijumaa hii huko Paris, UFaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe wake.Mashinani ikiwa jana Julai 22 Ripoti mpya kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi ilitolewa, hivyonampa fursa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS Winnie Byanyima akitahadhrisha kuhusu kuongeza kasi ya vita dhidi ya ukimwi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Wafugaji Samburu: Ngamia sio tu wamenusuru familia zetu, pia wametufungulia ukurasa mpya
    Kauti ya Samburu Kaskazini mwa Keny ni miongoni mwa maeneo mengi yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ya Wasamburu kwa kawaida ni wafugaji, baada ya ukame kukatili maisha ya mifugo yao haswa ng’ombe na mbuzi wakazi wengi walipoteza matumaini hadi pale FAO ilipowaletea mradi wa ufugaji wa ngamia kama mbadala wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Nankaya Lepitiling, mwanachama wa kikundi cha wanawake cha Salato Samburu ambaye ameona faida ya ufugaji wa ngamia kupitia mradi wa FAO, anasema “Tumewaonna ngamia kwa mda mrefu kwenye kikundi chetu, na mimi niimeshakuwa kiongozi wa kikundi cha Salato, tulipewa ngamia wa mradi, wanafika karibu  ngamia 30 hivi”Ntomuan Selaina naye ni mnufaifa wa mradi huo..“Wametusaidia  sana kwa chakula cha  watoto, hakuna shida hata kidogo, hata chai wengine wanakunywa ya siturungi nami nakunywa ya maziwa , nawapatia pia watu wengine na sasa kuna huyu mtoto  amekuja hapa kwa sababu mama yake hana maziwa tunampatia ya ngamia wngu.”Kwamujibu wa FAO ukame ulichochea ongezeko la utapiamlo na magonjwa mengine ya ukosefu wa lishe bora hususan miongoni mwa  watoto ndio FAO ikachukua hatua kwa kuanza kugawa ngamia kupitia mradi wa ubunifu wa PEAR ambao pia unawapa wafugaji mafunzo . Timothy Lesingran ni mtaalam wa wanyama katika mradi huo wa PEAR“Tunatoa mafunzo kwa wanawake na tumewafunza wanawake wengi tuu katika ngazi mbalimbali na wengi wamefurahia sana kufanyakazi nasi.”Pia mradi huu umewapa wanawake hawa wafugaji fursa nyingine kama wanavyosema Ntomuan na Nangaya,“Hata vikapu tunavyotumia kukamua maziwa tunavishona wenyewe na tunaviuza pesa tunayopata tunanunua chakula cha kutulisha sisi na watoto wetu. Na tangu tulipopata ngamia tena tukenda kujenga mahali pengine duka la maziwa sasa tunakamua maziwa , tunayaweka kwenye mashine, tunachuja mafuta , tunauza maziwa freshi na mazia lala, na tunatengeneza peremende ya jibini ya maziwa ya ngamia”Mradi huu wa FAO umewalenga zaidi wanawake na familia zinazogawiwa ngamia zimewajibika kutia saini mkabata unaosema ngamia waliyepokea ni wa mama wa familia hiyo, lakini faida kubwa imekuwa kwa familia  nzima na hasa watoto kama Juma Lesaina mtoto wa Ntomuan, anasema mama (PARAPHRASE)“Alininunulia sare za shule kutokna na maziwa aliyopata ya ngamia na  ndipo nilipoweza kujiunga na shule kwa msaada wa ngamia, na nimesomea uhandisi wa masualaya umeme , hivyo nimefika hapa nimatokeo ya ngamia na watu waliona ngamia maisha yao yamebadilika.”FAO sasa imepanua wigo wa mradi huo katika kaunti zingine za jirani ikiwemo Isiolo na lengo ni kuzifikia kaunti nyingi zaidi za wafugaji.
    4 min
  • WFP: Sera rafiki zinawainua kiuchumi wakimbizi nchini Uganda
    Je wafahamu kuwa Uganda ndio nchi inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika? Na sera rafiki za maendeleo za nchi hiyo zinawapa wakimbizi fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe.Mmoja wa wanaofaidi sera hizo ni Jeniffer mkimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambaye anaeleza ni muhimu kwa wakimbizi kuzalisha chakula chao wenyewe.“Niliondoka DR Congo sababu ya vita. Ninapokea Msaada wa chakula kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP lakini ukweli ni kuwa chakula hicho hakitoshi ndio maana nikahamia kwenye kilimo.”Wakimbizi milioni 1.6 wanapatiwa hifadhi nchini Uganda, idadi hii ni mara nne zaidi ya idadi ilivyokuwa muongo mmoja uliopita. Wakimbizi wanapatiwa fursa ya kumiliki ardhi na kuyafikia masoko na hii inawapa fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe“Nilikuwa mkulima nilipokuwa nchini kwangu na hapa niliungana na wananchi wa hapa pamoja na wakimbiziwengine na tukaanza kilimo cha mbogamboga. Tunashirikiana na wazawa na sote tunafundishana, tunalima nyanya, kabichi, maharage na matikiti maji. Mwezi uliopita niluza mazao yang una kupata dola 140, nilitumia fedha hizo kununua chakula na kukodisha ardhi zaidi ya kilimo.”WFP inafanya kazi na wakimbizi na jamii zinazowakaribisha kujenga jamii zenye ustahimilivu.
    2 min
  • 22 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya juhudi za kutokomeza ukimwi, na miradi ya WFP kwa wakimbizi nchini Uganda. Makala tunamulika faida ngamia kkwa wafugaji nchini Kenya, na mashinani tunaangazia ziara za Fillipo Grandi nchini Ukraine.Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na muungano  wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi unaojumuisha mashirika mbalimbali, inaonyesha kwamba dunia iko katika wakati muhimu wa kubaini endapo viongozi wa dunia watatimiza  ahadi zao  za      kumaliza janga la ukimwi kama tishio la afya ya umma  ifikapo mwaka 2030.Je wafahamu kuwa Uganda ndio nchi inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika? Na sera rafiki za maendeleo za nchi hiyo zinawapa wakimbizi fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe. Mmoja wa wanaofaidi sera hizo ni Jeniffer mkimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambaye anaeleza ni muhimu kwa wakimbizi kuzalisha chakula chao wenyewe.Makala tunakwenda kauti ya Samburu Kaskazini mwa Kenya ambayo ni miongoni mwa maeneo mengi yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ya Wasamburu kwa kawaida ni wafugaji, baada ya ukame kukatili maisha ya mifugo yao haswa ng’ombe na mbuzi wakazi wengi walipoteza matumaini hadi pale FAO ilipowaletea mradi wa ufugaji wa ngamia kama mbadala wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.Na mashinani tunamsikia Fillipo Grandi, Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambaye amehitimisha ziara yake mwishoni mwa wiki nchini Ukraine kushuhudia matokeo ya mlipuko wa hivi karibuni wa hospital ya Okhmatdyt.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • Tanzania, Kenya na Uganda zasonga mbele kuzuia maambukizi ya UKIMWI kwa watoto- UNAIDS
    Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na muungano  wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi unaojumuisha mashirika mbalimbali, inaonyesha kwamba dunia iko katika wakati muhimu wa kubaini endapo viongozi wa dunia watatimiza  ahadi zao  za  kumaliza janga la ukimwi kama tishio la afya ya umma  ifikapo mwaka 2030. Ripoti hiyo, iliyotolewa mjini Geneva na Munich inasisitiza uharaka wa kuchukua hatua kwani ukimwi uko  njiapanda na inatanabaiisha, takwimu mpya na tafiti zinazoonyesha kwamba maamuzi na uchaguzi wa sera vinahitajika sasa.Inasema utoaji wa haraka wa huduma za VVU pekee ndio utakaotimiza ahadi ya kukomesha UKIMWI kwa watoto ifikapo 2030.Ripoti hiyo”Kubadili maono kuwa hali halisi” inaonyesha kwamba janga la Ukimwi linaweza kumalizika ifikapo 2030, endapo viongozi wa dunia wataongeza rasilimali na kulinda haki za binadamu hivi sasa.Kwani inaonyesha kuwa programu maalum zinazolenga maambukizi ya VVU zimesaidia kuepusha maambukizi milioni 4 miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 0-14 tangu mwaka 2000.Ulimwenguni kote, maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 0-14 yamepungua kwa asilimia 38 tangu mwaka 2015 na vifo vimepungua kwa asilimia 43.Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima amesema"Ninapongeza maendeleo ambayo mataifa mengi yanapata katika kusambaza huduma za VVU ili kuwapa afya bora  wanawake vijana na kuwalinda watoto wachanga na watoto wengine dhidi ya VVU. Kwa dawa na sayansi zilizopo leo, tunaweza kuhakikisha kuwa watoto wote wanazaliwa na kuishi bila VVU, na kwamba watoto wote wanaoishi na VVU wanapata huduma na kusalia kwenye matibabu. Huduma za matibabu na kinga lazima ziongezeke mara moja ili kuhakikisha kuwa zinawafikia watoto wote kila mahali. “Ameongeza kuwa  Hatuwezi kupumzika kwani kifo cha mtoto yeyote kutokana na sababu zinazohusiana na UKIMWI sio tu janga, lakini pia hasira. Ninakotoka, watoto wote ni watoto wetu. Ulimwengu unaweza na lazima utimize ahadi yake ya kukomesha UKIMWI kwa watoto ifikapo 2030.”Miongoni mwa nchi 12 za muungano wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi, kadhaa zimefanikisha upatikanaji wa matibabu ya kudumu ya dawa za kuongeza mud awa kuishi miongoni mwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wanaoishi na VVU, huku Uganda ikikaribia asilimia 100, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 98, na Afrika Kusini kwa asilimia 97, Msumbiji imefikia asilimia 90, Zambia asilimia 90, Angola na Kenya kwa asilimia 89, Zimbabwe kwa asilimia 88, na Cote d'Ivoire kwa asilimia 84.
    2 min
  • WHO: Polio mwiba mpya kwa watu wa Gaza, wahudumu wa kibinadamu wanaonya
    Wananchi wa Gaza wakikabiliwa na machungu ya kila namna, kugunduliwa kwa tishio la ugonjwa wa polio unaoambukiza sana unaohusishwa na hali mbaya ya usafi iliyosababishwa na mzozo unaoendelea kumekuwa kama chumvi kwenye kidonda.Katika taarifa aliyoitoa Christian Lindmeier, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi leo amesema virusi vya polio (VDPV2) vimepatikana katika maeneo sita katika sampuli za maji taka zilizokusanywa tarehe 23 mwezi Juni kutoka katika maeneo ya Khan Younis na Deir al Balah huko Ukanda wa Gaza."Ni muhimu kutambua virusi vimetengwa kutoka kwenye mazingira kwa wakati huu tu; hakuna tukio lolote lililogunduliwa la kupooza linalohusiana na haya," amewaambia waandishi wa habari.Kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na hali hiyo, WHO katika eneo linalokaliwa la Palestina tayari inafanya kazi na mamlaka ya afya ya eneo hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) na washirika wanatathimini ni kwa ukubwa kiasi gani virusi hivyo vya polio vimeenea.“Kazi hii itaamua hatua zinazohitajika kukomesha kuenea zaidi, "ikiwa ni pamoja na kampeni za chanjo za haraka", msemaji wa WHO ameeleza.Virusi vya polio mwitu vilitokomezwa zaidi ya miaka 25 iliyopita katika Gaza kutokana na kampeni ya kina ya chanjo. WHO inasema chanjo kabla ya vita ilikuwa asilimia 95 mwaka 2022.Lakini zaidi ya miezi tisa ya vita, kuhama mara kwa mara kwa watu wengi na "kuharibika kwa mfumo wa afya, ukosefu wa usalama, viuzuizi, uhamisho wa mara kwa mara wa watu, uhaba wa vifaa vya matibabu, uduni wa ubora wa maji na vyoo dhaifu" vimeunda "mazingira bora” kwa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kuenea na polio ni moja kati ya hayo amebainisha Christian Lindmeier wa WHO.Leo huko Gaza, ni hospitali 16 tu kati ya 36 ambazo zinafanya kazi kwa kiasi, na 45 kati ya vituo 105 vya huduma ya afya ya msingi ndivyo vinafanya kazi, kulingana na afisa huyo wa WHO, ambaye amesisitiza kuwa ni usitishaji wa mapigano tu ndio utakaoruhusu kuongezeka kwa kasi kwa shughuli za chanjo "kushughulikia mapungufu yaliyotokana na vita vinavyoendelea".
    2 min
  • Monicah Malith: Hizi ndizo sababu zimenifanya kusomea sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi
    Katika makala hii Anold Kayanda Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Monicah Malith mmoja wa vijana waliofika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria Jukwaa la Kisiasa la Ngazi za Juu la Umoja wa Mataifa (HLPF) mwaka 2024. Monicah Malith aliikimbia  nchi yake Sudan Kusini na kuingia Kenya.  Kupitia makala hii anaeleza kwa nini aliamua kuisoma kozi anayoisoma sasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwani ana matumaini kozi hiyo itasaidia kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners