Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 22 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya juhudi za kutokomeza ukimwi, na miradi ya WFP kwa wakimbizi nchini Uganda. Makala tunamulika faida ngamia kkwa wafugaji nchini Kenya, na mashinani tunaangazia ziara za Fillipo Grandi nchini Ukraine.Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na muungano  wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi unaojumuisha mashirika mbalimbali, inaonyesha kwamba dunia iko katika wakati muhimu wa kubaini endapo viongozi wa dunia watatimiza  ahadi zao  za      kumaliza janga la ukimwi kama tishio la afya ya umma  ifikapo mwaka 2030.Je wafahamu kuwa Uganda ndio nchi inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika? Na sera rafiki za maendeleo za nchi hiyo zinawapa wakimbizi fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe. Mmoja wa wanaofaidi sera hizo ni Jeniffer mkimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambaye anaeleza ni muhimu kwa wakimbizi kuzalisha chakula chao wenyewe.Makala tunakwenda kauti ya Samburu Kaskazini mwa Kenya ambayo ni miongoni mwa maeneo mengi yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ya Wasamburu kwa kawaida ni wafugaji, baada ya ukame kukatili maisha ya mifugo yao haswa ng’ombe na mbuzi wakazi wengi walipoteza matumaini hadi pale FAO ilipowaletea mradi wa ufugaji wa ngamia kama mbadala wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.Na mashinani tunamsikia Fillipo Grandi, Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambaye amehitimisha ziara yake mwishoni mwa wiki nchini Ukraine kushuhudia matokeo ya mlipuko wa hivi karibuni wa hospital ya Okhmatdyt.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • Tanzania, Kenya na Uganda zasonga mbele kuzuia maambukizi ya UKIMWI kwa watoto- UNAIDS
    Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na muungano  wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi unaojumuisha mashirika mbalimbali, inaonyesha kwamba dunia iko katika wakati muhimu wa kubaini endapo viongozi wa dunia watatimiza  ahadi zao  za  kumaliza janga la ukimwi kama tishio la afya ya umma  ifikapo mwaka 2030. Ripoti hiyo, iliyotolewa mjini Geneva na Munich inasisitiza uharaka wa kuchukua hatua kwani ukimwi uko  njiapanda na inatanabaiisha, takwimu mpya na tafiti zinazoonyesha kwamba maamuzi na uchaguzi wa sera vinahitajika sasa.Inasema utoaji wa haraka wa huduma za VVU pekee ndio utakaotimiza ahadi ya kukomesha UKIMWI kwa watoto ifikapo 2030.Ripoti hiyo”Kubadili maono kuwa hali halisi” inaonyesha kwamba janga la Ukimwi linaweza kumalizika ifikapo 2030, endapo viongozi wa dunia wataongeza rasilimali na kulinda haki za binadamu hivi sasa.Kwani inaonyesha kuwa programu maalum zinazolenga maambukizi ya VVU zimesaidia kuepusha maambukizi milioni 4 miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 0-14 tangu mwaka 2000.Ulimwenguni kote, maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 0-14 yamepungua kwa asilimia 38 tangu mwaka 2015 na vifo vimepungua kwa asilimia 43.Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima amesema"Ninapongeza maendeleo ambayo mataifa mengi yanapata katika kusambaza huduma za VVU ili kuwapa afya bora  wanawake vijana na kuwalinda watoto wachanga na watoto wengine dhidi ya VVU. Kwa dawa na sayansi zilizopo leo, tunaweza kuhakikisha kuwa watoto wote wanazaliwa na kuishi bila VVU, na kwamba watoto wote wanaoishi na VVU wanapata huduma na kusalia kwenye matibabu. Huduma za matibabu na kinga lazima ziongezeke mara moja ili kuhakikisha kuwa zinawafikia watoto wote kila mahali. “Ameongeza kuwa  Hatuwezi kupumzika kwani kifo cha mtoto yeyote kutokana na sababu zinazohusiana na UKIMWI sio tu janga, lakini pia hasira. Ninakotoka, watoto wote ni watoto wetu. Ulimwengu unaweza na lazima utimize ahadi yake ya kukomesha UKIMWI kwa watoto ifikapo 2030.”Miongoni mwa nchi 12 za muungano wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi, kadhaa zimefanikisha upatikanaji wa matibabu ya kudumu ya dawa za kuongeza mud awa kuishi miongoni mwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wanaoishi na VVU, huku Uganda ikikaribia asilimia 100, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 98, na Afrika Kusini kwa asilimia 97, Msumbiji imefikia asilimia 90, Zambia asilimia 90, Angola na Kenya kwa asilimia 89, Zimbabwe kwa asilimia 88, na Cote d'Ivoire kwa asilimia 84.
    2 min
  • WHO: Polio mwiba mpya kwa watu wa Gaza, wahudumu wa kibinadamu wanaonya
    Wananchi wa Gaza wakikabiliwa na machungu ya kila namna, kugunduliwa kwa tishio la ugonjwa wa polio unaoambukiza sana unaohusishwa na hali mbaya ya usafi iliyosababishwa na mzozo unaoendelea kumekuwa kama chumvi kwenye kidonda.Katika taarifa aliyoitoa Christian Lindmeier, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi leo amesema virusi vya polio (VDPV2) vimepatikana katika maeneo sita katika sampuli za maji taka zilizokusanywa tarehe 23 mwezi Juni kutoka katika maeneo ya Khan Younis na Deir al Balah huko Ukanda wa Gaza."Ni muhimu kutambua virusi vimetengwa kutoka kwenye mazingira kwa wakati huu tu; hakuna tukio lolote lililogunduliwa la kupooza linalohusiana na haya," amewaambia waandishi wa habari.Kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na hali hiyo, WHO katika eneo linalokaliwa la Palestina tayari inafanya kazi na mamlaka ya afya ya eneo hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) na washirika wanatathimini ni kwa ukubwa kiasi gani virusi hivyo vya polio vimeenea.“Kazi hii itaamua hatua zinazohitajika kukomesha kuenea zaidi, "ikiwa ni pamoja na kampeni za chanjo za haraka", msemaji wa WHO ameeleza.Virusi vya polio mwitu vilitokomezwa zaidi ya miaka 25 iliyopita katika Gaza kutokana na kampeni ya kina ya chanjo. WHO inasema chanjo kabla ya vita ilikuwa asilimia 95 mwaka 2022.Lakini zaidi ya miezi tisa ya vita, kuhama mara kwa mara kwa watu wengi na "kuharibika kwa mfumo wa afya, ukosefu wa usalama, viuzuizi, uhamisho wa mara kwa mara wa watu, uhaba wa vifaa vya matibabu, uduni wa ubora wa maji na vyoo dhaifu" vimeunda "mazingira bora” kwa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kuenea na polio ni moja kati ya hayo amebainisha Christian Lindmeier wa WHO.Leo huko Gaza, ni hospitali 16 tu kati ya 36 ambazo zinafanya kazi kwa kiasi, na 45 kati ya vituo 105 vya huduma ya afya ya msingi ndivyo vinafanya kazi, kulingana na afisa huyo wa WHO, ambaye amesisitiza kuwa ni usitishaji wa mapigano tu ndio utakaoruhusu kuongezeka kwa kasi kwa shughuli za chanjo "kushughulikia mapungufu yaliyotokana na vita vinavyoendelea".
    2 min
  • Monicah Malith: Hizi ndizo sababu zimenifanya kusomea sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi
    Katika makala hii Anold Kayanda Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Monicah Malith mmoja wa vijana waliofika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria Jukwaa la Kisiasa la Ngazi za Juu la Umoja wa Mataifa (HLPF) mwaka 2024. Monicah Malith aliikimbia  nchi yake Sudan Kusini na kuingia Kenya.  Kupitia makala hii anaeleza kwa nini aliamua kuisoma kozi anayoisoma sasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwani ana matumaini kozi hiyo itasaidia kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.
    3 min
  • 19 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia tishio la polio Gaza, na kauli za chuki zinazoweza kusababisha mauaji ya kimbari na ukosefu wa amani. Makala tunaangazia vijana kutoka Uganda katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu, na mashinani tunakupeleka nchini Somalia, kulikoni?Wananchi wa Gaza wakikabiliwa na machungu ya kila namna, kugunduliwa kwa tishio la ugonjwa wa polio unaoambukiza sana unaohusishwa na hali mbaya ya usafi iliyosababishwa na mzozo unaoendelea kumekuwa kama kuongeza chumvi kwenye kidonda.Alice Wairimu Nderitu mashauri maalum wa Umoja wa Mataifa  katika kuzuia auaji ya kimbari akizungumza na UN New Kiswahili hivi karibuni na huku akitoa raia kuhusu mauaji hayo na kutaka kila mtu kumakinika na kuchukua hatua.Katika makala Anold Kayanda anazungumza na Monicah Malith mmoja wa vijana waliofika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria Jukwaa la Kisiasa la Ngazi za Juu la Umoja wa Mataifa (HLPF) mwaka 2024. Monicah Malith aliikimbia  nchi yake Sudan Kusini na kuingia Kenya.  Kupitia makala hii anaeleza kwa nini aliamua kuisoma kozi anayoisoma sasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwani ana matumaini kozi hiyo itasaidia kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.Na mashinani Fosiya Ibarahim Botan mkulima katika kijiji cha Erigavo nchini Somalia akitueleza jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, linasaidia wakulima kujikimu kimaisha kupitia msaada wa fedha taslimu, elimu na uundaji wa vyama vya mikopo vya akiba vya vijiji.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Alice Nderitu: Kauli za chuki na mauaji ya kimbari ni lila na fila havitengamani
    Alice Wairimu Nderitu mashauri maalum wa Umoja wa Mataifa  katika kuzuia auaji ya kimbari akizungumza na UN New Kiswahili hivi karibuni na huku akitoa raia kuhusu mauaji hayo na kutaka kila mtu kumakinika na kuchukua hatua.“Ningependa watu wajue kwamba mauaji ya kimbari huwa hayafanyiki bila mpango. Na wenye kupanga huwa wanajua wale watu  wanaopanga kuwaangamiza ni lazima kwanza wawatoe utu , wawaonyeshe kwamba wao sio binadamu. Na ndio maana huwa wanaitwa mende kama walivyokuwa wakiwaita Watutsi, au chawa kama walivyowaita watu wa Rohingya au watu wachafu kama walivyokuwa wanawaita watu wa Yazid huko Iraq. Na kila mtu akisikia watu wanaitwa haya majina ya wanyaka inafaa wajue mpango unaweza kuwepo, na huo mpango unaweza kuwa ni wa mauaji ya kimbari.”Akaenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa,“Kwa hivyo kila mtu achukulie kauli za chuki kwa uzito mkubwa. Kama tungependa kuishi kama watu walio na utu na tungependa kurejesha utu duniani , tuendelee kuwasaka walio na utu ndio tuweze kuwachukulia hatua wale wanaotoa kauli za chuki, kuzungumza nao na kuwafunza watoto na kufunza watu wengi kwenye hii dunia maana ya kauli za chuki sababu nisingependa watu wasahau ya kwamba hakuna mauaji ya kimbari  yalishafanyika bila kauli za chuki. Hatungependa yale yaliyofanyika Rwanda yatokee tena. Hivyo kama hatutaki yafanyike tena tukumbuke kwamba kauali za chuki zinatuelekeza sote kwenye mauaji ya kimbari.
    2 min
  • 18 JULAI 2024
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -WFP limeonya kwamba amri ya hivi karibuni kabisa ya Jeshi la Israel ya watu kuondoka Gaza imesababisha idadi kubwa zaidi ya watu kutawanywa tangu mwezi Oktoba mwaka jana.-Leo ni siku ya kimtaifa ya Nelson Mandel mwaka huu ikibeba maudhui “Bado ni jukumu letu kutokomeza njaa na pengo la usawa” -Hatua za haraka zinahitajika  kuhakikisha  haki za binadamu katika vituo vya rumande nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR,  kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA. -Mada yetu kwa kina leo inaangazia siku ya Mandela na jinsi  watu wanavyomfahamu na kuenzi mchango  wake-Na matika jifunze Kiswahili tunakupeleka  Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA nchini Tanzania kupata ufafanuzi waneno HAZAMA
    10 min
  • Edem Wosornu: Watu wa Haiti wanaomba mambo matatu
    Wakati wa ziara ya siku nne nchini Haiti hivi karibuni, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utetezi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Dharura (OCHA), Edem Wosornu ametembelea maeneo kadhaa ya miradi ya misaada ya kibinadamu na kukutana na jamii zilizoathirika, mamlaka za Haiti, pamoja na washirika wa kitaifa, kimataifa na wa ndani, kujadili janga la kibinadamu nchini humo pamoja na mikakati zaidi ya misaada ya dharura.Akieleza hali aliyoikuta Bi Wosornu anasema, “Watu wa Haiti wanaomba mambo matatu. Wanaomba amani, wanaomba ghasia za magenge zikome, wanaomba kurejeshewa nchi yao.”Ziara hiyo inakuja wakati ambapo Haiti inakabiliwa na mgogoro ambao umezidi kuwa mbaya zaidi tangu Machi mwaka huu kukiwa na vurugu mpya katika mji mkuu, Port-au-Prince. Kwa mujibu wa OCHA, zaidi ya watu 578,000 kwa sasa wamekimbia makazi yao nchini Haiti, na zaidi ya shule 900 zimefungwa tangu Januari mwaka huu yaani zaidi ya nusu mwaka.Anaeleza alichozungumza na watoto akisema,"Watoto nilioshirikiana nao huko Gonaives, huko Les Cayes lakini pia huko Port-au-Prince, wanaomba kuweza kurejea shuleni. Watoto niliokutana nao wanataka kuwa madaktari, wanataka kuwa wanasheria, wanataka kuwa walimu, wanataka kuwa wauguzi. Watu wa Haiti wamechoshwa na ghasia. Watu wa Haiti wanataka kurejea katika maisha yao.”Emile Macier, mkuu wa shule ya Joseph Bernard des Frères ya mjini Port-au-Prince kwa masikitiko anaeleza,“Maelfu ya wanafunzi wananyimwa masomo. Nani anajua, labda magenge yamewachukua. Nia yangu kubwa ni kwamba tutafute sehemu nyingine ya kuwahifadhi waliofurushwa ili shule ifanye kazi. Hatuwezi kufunga shule. Je, itakuwaje kwa watoto? Huwezi kujua magenge yamewawajiri wangapi? Huweze kujua wasichana wangapi walibakwa na kupata mimba. Hatujui.”Kwa upande wa afya nako hali ni tete kama alivyojionea Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utetezi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Dharura (OCHA), Edem Wosornu,“Tunatakiwa kuhakikisha kuwa vituo vya afya vya nchi hii vina uwezo wa kuwasaidia wananchi. Tunahitaji kuhakikisha kuwa miundombinu ya elimu ina uwezo wa kusaidia watu. Suluhu za muda mrefu zinahitajika za haraka na za muda mfupi.Bi Wosornu anaeleza kwamba, Bi Wosornu anaeleza kwamba, "Watu milioni 1.6 kati ya watu milioni 5 ambao wana uhaba wa chakula katika nchi hii wanahitaji sana usaidizi. Nchi inayozalisha maembe na ndizi na viazi vikuu na ndizi na nchi ambayo ina udongo halisi, wenye rutuba na wenye rutuba haipaswi kuwa na uhaba wa chakula. Vurugu lazima zikome ili kuruhusu watu kurudi kwenye mashamba yao, ili waweze kuishi maisha yao.Ni nini kifanyike? Wosornu anaeleza,"Wadau wa misaada ya kibinadamu ni sehemu ya suluhisho, lakini pia tunahitaji washirika wa maendeleo kwa mbinu za muda mrefu. Tunahitaji suluhu za pamoja, sio tu kutoka kwa sehemu moja ya mwavuli wa usaidizi, lakini kutoka kwa nyanja zote tofauti za mambo.”
    4 min
  • UN: Hali inaendelea kuwa kizungumkuti Gaza mashambulizi yakishika kasi
    Hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya Gaza huku leo mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa  Mataifa yakiripoti kuendelea kwa mashambulizi yanayokatili maisha ya watu na kuathiri miundombinu ya raia kuanzia kwenye shule hadi vituo vya afya huku maelfu ya watu wakiendelea kukabiliwa na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo afya, makazi, maji  na  chakula kadri vita vinavyoendelea. Asante Leah nikianza na shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO ambalo leo limeendelea kusihi pande zinazozozana kwenye Ukanda wa Gaza kuheshimu sheria za kimataifa na kulinda vituo vya afya na wahudumu wa afya linasema tangu Oktoba 7 mwaka jana mzozo huu mpya ulipozuka limeorodhesha mashambulizi zaidi ya 1000 kwenye vituo vya afya katika eneo hilo linalokaliwa la Palestina.Hivyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X limesema “Tunatoa ombi la ulinzi  wa wahudumu wa afya na vituo vya afya kwa ajili ya fursa za kuweza kutoa msaada wa kibinadamu na mapigano lazima yakome mara moja.”Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa  Kipalestina UNRWA likiunga mkono usitishwaji wa  mapigano mara moja kwa minajili ya kibinadamu limesema Watoto wa Ukanda wa Gaza wameporwa utoto wao na mustakbali wao, elimu imegeuka ndoto na madhila ya kiafya  ni tishio lingine.Philippe Lazzarini Kamishina Mkuu wa UNRWA ameandika kwenye ukurasa wake wa X kwamba “Karibu kila siku kuna mashambulizi dhidi ya vituo vya elimu. Takribani shule 8 zimeshambuliwa katika  siku 10 zilizopita zikiwemo shule 6 za UNRWA. Vita vimewapora wasichana na wavulana wa Gaza utoto wao na elimu yao.”Ameongeza kuwa changamoto za afya ni mtihani mwingine unaotishia mustakbali wa watoto wa Gaza akimtolea mfano mvulana wa umri wa miaka minne akisema “ Mvulana huyu anaugua magonjwa ya ngozi kutokana na hali mbaya ya familia yake, wakilala katika mahema yaliyoezekwa kwa karatasi za plastiki bila kupata vifaa vya usafi au maji safi ya kutosha hii ni hatari kubwa. Timu zetu za UNRWA zinatoa dawa, lakini bila ya hali kuboreka, maambukizi ya magonjwa yanarudi tena”.Amesisitiza kwamba ili madhila yote haya yaishe ni lazima vita vikome mara moja.
    2 min
  • 17 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na huduma za afya kwa watoto na wanawake nchini Afghanistan. Makala inatupeleka nchini Haiti na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya Gaza huku leo mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa  Mataifa yakiripoti kuendelea kwa mashambulizi yanayokatili maisha ya watu na kuathiri miundombinu ya raia kuanzia kwenye shule hadi vituo vya afya huku maelfu ya watu wakiendelea kukabiliwa na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo afya, makazi, maji  na      chakula kadri vita vinavyoendelea.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF nchini Afghanistan limeweka programu maalum ya mama na watoto inayotolewa na waajiriwa wanawake ambao huwafanyia uchunguzi na kuwatibu watoto wenye utapiamlo na pia kuwafundisha wakina mama namna ya kuandaa chakula chenye lishe bora kwa watoto waoMakala inaangazia ziara ya siku nne nchini Haiti aliyoifanya hivi karibuni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utetezi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Dharura (OCHA), Edem Wosornu.Mashinani Inatupeleka katika kaunri ya Marsabit nchini Kenya kusikia ujumbe wa Amina Godana ambaye ni Msaidizi wa chifu, na Halima Somo, Mwanachama wa kikundi cha raia wanaohakikisha uwepo wa amani na utangamano wakieleza ni kwa jinsi gani Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limeziwezesha jamii za kijiji chao kuondokana na usafirishaji haramu wa binadamu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners