Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNICEF nchini Afghanistan inatoa huduma za lishe bora kwa wanawake na watoto
    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF nchini Afghanistan limeweka programu maalum ya mama na watoto inayotolewa na waajiriwa wanawake ambao huwafanyia uchunguzi na kuwatibu watoto wenye utapiamlo na pia kuwafundisha wakina mama namna ya kuandaa chakula chenye lishe bora kwa watoto wao.Video ya UNICEF inaanza kwa kuwaonesha wanawake watatu kila mmoja akiwa amembeba mtoto wakielekea katika kituo cha afya kinachotoa virutubisho vya lishe kila siku. Mmoja wa wanawake hao ni Khatira Salemii. Anasema, “katika kituo hichi, wamempa mwanangu chakula cha lishe, baada ya kuhuduhuria kwa takriban mara tano au sita walimpima uzito na urefu wake na nilishukuru waliponiambia ni sasa mtoto wangu mwenye afya tena”.Mjini Kabul, vituo vya afya mara nyingi huwa na msongamano mkubwa wa watu au wafanyakazi wachache hivyo UNICEF hili kushughulikia tatizo hilo ilianzisha vituo 50 vinavyotoa lishe katika vitongoji vyenye watu wengi.Wote wanaotoa huduma vituoni hapo ni wanawake na mmoja wao ni Sodaba Osman.“Tunatoa chakula cha matibabu kilicho tayari kutumika kwa watoto wenye utapiamlo, inafurahisha sana kwamba ninafanya kazi ya kuponya watoto, pia tunawashauri wajawazito na wakina mama wanaonyonyesha. Nawafundisha kuwa wakiwa nyumbani wanapaswa kula vyakula vyenye afya, mboga mboga na vyakula vingine ambavyo ni vyema kwao na vinajumuisha vitamini nyingi, hilo linanifurahisha sana”Kwa mwaka huu UNICEF inalenga kuwafanyia uchunguzi watoto milioni 1.2 wenye utapiamlo, kutibu watoto 90,000 wenye utapiamlo mkali na kufikia akina mama 347,000 wanaonyonyesha nakuhakikisha wanapata lishe bora.
    2 min
  • Mataifa yanapaswa kushikamana kusongesha agenda 2030 ya SDGs: Mweli
    Jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF, kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs linaelekea ukingoni hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa  likitarajiwa kukunja jamvi hapo kesho Julai 17. Wawakilishi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamekuwa hapa kwa takriban wiki mbili kujadili jinsi ya kusongesha malengo hayo endelevu. Miongoni mwao ni Gerald Geofrey Mweli, Katibu Mkuu kutoka wizara ya kilimo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amemweleza Flora Nducha wa idhaa hii kuhusu ushiriki wake katika jukwaa hili.
    9 min
  • 16 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Gerald Geofrey Mweli, Katibu Mkuu kutoka wizara ya kilimo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuotoa mkutano wa HLPF amezungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Muda unazidi kuyoyoma kwa raia wanaokabiliwa na njaa nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wameonya leo wakati mazungumzo yanayohusisha pande zinazozozana nchini humo yakiendelea mjini Geneva wiki hii.Dharura ya kibinadamu nchini Haiti inahitaji uangalizi wa haraka, Wawakilishi kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na Idara ya Ulinzi wa Raia na Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Ulaya (ECHO) wamesema walipokamilisha ziara ya siku nne nchini humo.Na Cote d'Ivoire ikiwa inakabiliwa na kuongezeka kwa matatizo ya maji na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye rasilimali za maji inazopakana na majirani zake, nchi hiyo sasa imejiunga na Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa wa kuboresha usimamizi wa pamoja wa maji katika mipaka.Mashinani ikiwa hivi karibuni dunia imetoka kuadhimisha siku ya idadi ya watu duniani shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi UNFPA likisihi mataifa yote duniani kuelimisha uma kuhusu mchango wa sensa katika malengo ya maendeleo endelevu, nampisha kijana kutoka Mwanza, nchini Tanzania akieleza umuhimu wa sensa katika utendaji wa serikali.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • FAO: Mradi wa maendeleo ya mifumo ya chakula kutekelezwa Zanzibar
    Uwepo wa athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli kibinadamu umeendelea kupata ufumbuzi ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), nchini Tanzania limeratibu kikao kazi cha maandalizi ya kutengeneza Mradi wa maendeleo ya mifumo ya chakula katika nyanda za juu kusini maeneo ya Bonde la Usangu pamoja na visiwani Zanzibar, Mradi ambao tayari umetengewa Dola za kimarekani Milioni 8.4 kwa ufadhili wa Mfuko wa mazingira wa Dunia (GEF – 8). Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time kutoka Mkoa wa Morogoro amefuatilia Kikao kazi hicho na kuandaa makala hii.
    5 min
  • UNMISS wapatia mafunzo ya ulinzi wa amani polisi wa Sudan Kusini
    Maafisa wa polisi wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wametoa mafunzo kwa askari polisi wa nchi hiyo ili waweze kuimarisha ulinzi na usalama wakati huo huo wakiheshimu haki za binadamu. TNchi ya Sudan Kusini inakabiliwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei huku ajira nazo zikiwa ngumu kupatikana hali hizi mbaya zimechocheea uhalifu. Jeshi la polisi limejikuta kwenye shinikizo kubwa la kushughulikia changamoto hizo wakati wakiwa na rasilimali chache wakati huo huo wakienda miezi kadhaa bila ya kulipwa mishahara.Pamoja na changamoto hizo bado wanawajibu wa kulinda raia na mali zao ndio maana polisi wa UNMISS wakaandaaa mafunzo ya vitendo katika makao makuu ya nchi hiyo jijini Juba yakihusu matumizi sahihi ya nguvu wanapokamata wahalifu, namna ya kuwasaka watuhumiwa kwa usalama, ulinzi usio na silaha, huduma ya kwanza, ulinzi wa viongozi na watu mashuhuri, usalama wa misafara ya magari, doria ndani ya jamii na kufanya uchunguzi.Sophia Ennim ni Afisa Polisi wa Umoja wa Mataifa chini ya UNMISS na anasema mafunzo hayo yatasaidia sio tu kupambana na wahalifu bali pia wakati wa uchaguzi wa kwanza ya nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu“Tunataka kubadilishana nao uzoefu na tena, tunajua wanajitayarisha kuelekea uchaguzi na tunafikiri wakati huu ndio bora kwao kujikumbusha upya mbinu zao za kipolisi.”Samuel Nai, ni mmoja wa maafisa wa Polisi wa Sudan Kusini aliyehitimu mafunzo hayo.“Kazi hii ya upolisi inachosha sana, inachangamoto sana, lakini uzoefu tulioupata hapa utatusaidia kufanya vyema zaidi katika siku zijazo. Haya ndiyo mabadiliko tunayotaka kutoka kwa polisi.”Mbali na kushukuru kwa mafunzo hayo Afisa wa polisi wa Suda Kusini Lilian Poni ambaye anatumikia polisi kwa miaka 19 ametoa wito kwa wanawake zaidi kupata fursa sawa ili kukuza zaidi taaluma zao.“Nikiwa nimekaa hapa, naona wanaume ni wengi wanawake ni wachache. Kwa hivyo angalau wanapaswa kuweka usawa wa kijinsia, ikiwa wanaume ni 10, wanawake wanapaswa kuwa 10 pia.”Mafunzo haya kwa jeshi la polisi yanafuatia kikao cha usimamizi wa utulivu wa umma ambacho kiliomba askari wapatiwe mafunzo ili kusaidia kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unafanyika kwa njia huru, ya haki, ya kuaminika na ya amani.UNMISS wameeleza kuwa pamoja na changamoto za ulinzi na usalama na taifa hilo kujiandaaa na uchaguzi lakini mafunzo yanayoendeshwa nao yana lengo kuu la kujenga uwezo wa maafisa wa polisi wa Sudan Kusini kukidhi mahitaji ya jamii zao.
    2 min
  • 15 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya harakati za chanjo kwa watoto na ulinzi wa amani na usalama inaozingatia haki za binadamu nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Rwanda, kulikoni?Viwango vya chanjo za utotoni ulimwenguni kote vilikwama mwaka 2023 na kuacha watoto milioni 2.7 bila chanjo au kupata kiwango kisichotosheleza cha chanjo ikilinganishwa na viwango vya kabla ya janga la COVID-19 mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu za ripoti mpya zilizochapishwa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  duniani UNICEFMaafisa wa polisi wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wametoa mafunzo kwa askari polisi wa nchi hiyo ili waweze kuimarisha ulinzi na usalama wakati huo huo wakiheshimu haki za binadamu.Katika makala Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Tanzania limefanya kikao kazi cha maandalizi ya kutengeneza Mradi wa maendeleo ya mifumo ya chakula katika nyanda za juu kusini maeneo ya Bonde la Usangu pamoja na visiwani Zanzibar.Na mashinani Prince ISHIMWE mwanafunzi wa Shule ya ufundi ya Forever TSS nchini Rwanda anatueleza jinsi uunganishwaji wa intaneti shuleni unamsaidia kuwasiliana na  kushirikiana  na wanafunzi wenzake katika  kujifunza na kuafanya utafiti mtandaoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    13 min
  • WHO/UNICEF: Watoto 3 kati ya 4 wanaishi katika nchi ambako upatikanaji wa chanjo ni mdogo na kusababisha milipuko ya magonjwa
    Viwango vya chanjo za utotoni ulimwenguni kote vilikwama mwaka  2023 na kuacha watoto milioni 2.7 bila chanjo au kupata kiwango kisichotosheleza cha chanjo ikilinganishwa na viwango vya kabla ya janga la COVID-19 mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu za ripoti mpya zilizochapishwa  leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  duniani UNICEF. Makadirio ya hivi karibuni ya WHO na UNICEF ya utoaji wa chanjo kitaifa (WUENIC) ambayo hutoa kiwango kikubwa zaidi cha takwimu duniani kuhusu mwelekeo wa chanjo dhidi ya magonjwa 14 yanasisitiza haja ya jitihada zinazoendelea za kujikwamua, kurejesha na kuimarisha mifumo ya chanjo. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell amesema "Mienendo ya hivi karibuni inaonyesha kwamba nchi nyingi zinaendelea kukosa chanjo kwa watoto wengi. Kuziba pengo la chanjo kunahitaji juhudi za kimataifa, serikali, washirika, na viongozi wa eneo hilo kuwekeza katika huduma za afya ya msingi na wahudumu wa jamii ili kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo, na kwamba huduma ya afya kwa ujumla inaimarishwa."Takwimu hizo zinaonyesha kwamba umla ya watoto milioni 14.5 duniani kote walikosa chanjo mwaka 2023  ikiwa ni Pamoja nay a ugonjwa wa surua na “Zaidi ya nusu ya watoto ambao hawajachanjwa wanaishi katika nchi 31 zenye mazingira magumu, zilizoathiriwa na migogoro na mazingira hatarishi, ambapo watoto wako katika hatari ya kupata magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa sababu ya changamoto na ukosefu wa usalama, lishe na huduma za afya.”Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema "Milipuko ya surua ni tahadhari ya hatari katika mgodi wa makaa ya mawe, ikifichua na kutumia mapengo katika chanjo na kuathiri walio hatarini zaidi kwanza. Hili ni tatizo linaloweza kutatuliwa. Chanjo ya surua ni nafuu na inaweza kutolewa hata katika maeneo magumu zaidi. WHO imejitolea kufanya kazi na washirika wetu wote kusaidia nchi kuziba mapengo haya na kuwalinda watoto walio katika hatari zaidi haraka iwezekanavyo.”Pamoja na changamoto takwimu hizo zinasema kuna matumaini hasa katika utoaji wa chanjo dhidi ya visusi vya papilloma vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi ambapo kwa msaada wa muungano wa chanjo duniani GAVI wasichana wengi wamefanikiwa kupata chanjo hiyo katika nchi 57 hasa Bangladesh, Indonesia na Nigeria.Hata hivyo, GAVI inasema chanjo ya chanjo ya HPV iko chini ya lengo la asilimia 90 la kuondoa saratani ya mlango wa kizazi kama tatizo la afya ya umma, na inafikia asilimia 56 tu ya wasichana katika nchi zenye kipato cha juu na 23% katika nchi za kipato cha chini na cha kati.
    4 min
  • Mdau wa biashara na Uchumi Tanzania waeleza faida za kuhesabiwa
    Ikiwa ni jana tu Julai 11, ambapo dunia iliadhimisha Siku ya Idadi ya watu duniani ikiwa na mahudhui ya kuangazia umuhimu wa kukusanya takwimu jumuishi kwa kuhesabu kila mtu, kila mahali na jinsi alivyo. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi UNFPA limesisitiza haja ya Sensa ili kuhakikisha usawa na jamii jumuishi duniani.Nchini Tanzania, kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika, suala hili la sensa limebeba mustakabali mkubwa kwa wananchi wa Taifa hilo. Ni kwa vipi? Tuungane na Bosco Cosmas katika Makala hii.
    3 min
  • 12 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia janga la kiafya na misaada ya kibinadamu nchini DRC, na mchakato wa uchaguzi mkuu nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani inaturejesha nchini DRC, kulikoni?Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC iko katikati ya janga la kiafya linaloongezeka limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani (WHO) na kusisitiza kwamba magonjwa ya milipuko yamezorotesha sana hali nchini humo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kuchochewa na ghasia na mafuriko.Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wake wa kwanza mwaka huu mwezi Desemba, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha kongamano la siku tatu la vyama vya siasa katika mji wa Rumbek ili kujadili masuala ambayo ni muhimu katika maandalizi ya uchaguzi huo.Katika makala Bosco Cosmas anatukutanisha na Katibu tawala katika kitivo cha Biashara na Uchumi kutoka chuo kikuu cha Mt. Agustino akieleza kuhusu jinsi kujua idadi ya watu kunavyoleta manufaa katika kuhakikisha maendeleo endelevu kwa jamii.Katika mashinani Deborah Dhra ambaye ni mama wa watoto wawili akitueleza jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usaidizi wa Dharura, CERF linaboresha afya ya jamii zilizoathiriwa na migogoro kwa kuweka matanki na mabomba ya maji safi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • WHO inasema janga la kiafya linashika kasi Congo DRC
    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC iko katikati ya janga la kiafya linaloongezeka limeonya leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO  na kusisitiza kwamba magonjwa ya milipuko yamezorotesha sana hali nchini humo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na ghasia na mafuriko. Kulingana na WHO, DRC imekabiliwa na ongezeko la migogoro na ghasia, na kusababisha watu wengi kukimbia makazi yao, magonjwa kuenea, unyanyasaji wa kijinsia, na kiwewe kikubwa cha akili, haswa mashariki mwa nchi hiyo.Dkt. Adelheid Marschang, Afisa wa Dharura wa WHO, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva kwamba"Kutokana na hali hiyo, watu wanakabiliwa na milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu, surua, uti wa mgongo, ndui na tauni, yote yakichangiwa na mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yanayoathiri sehemu kadhaa za nchi hiyo."Tangu mwanzoni mwa mwaka, WHO inasema zaidi ya visa 20,000 vya kipindupindu vimerekodiwa, viki katika eneo la Kivu Kaskazini.Pia kumekuwa na zaidi ya wagonjwa  65,000 wa surau na vifo 1,523, huku idadi halisi ikiwezekana kuwa kubwa zaidi kutokana na kutofuatilia na kuripoti magonjwa kwa kiasi cha kutosha. Wakati huo huo, kumekuwa na kesi 3,073 za homa ya uti wa mgongo ikiwa ni pamoja na vifo 251vilivyoripotiwa katika  katika nchi hii ya Maziwa Makuu.WHO pia imekuwa na wasiwasi juu ya lahaja ya mpox katika miezi ya hivi karibuni ambapo zaidi ya kesi 11,000 zikijumuisha vifo 445 zimerekodiwa, na kukiwa na kiwango cha juu cha vifo vya zaidi ya asilimia 4. Watoto wameelezwa kuathiriwa zaidi na janga hili, na viwango vya juu zaidi vya vifo.Migogoro ya silaha na watu kuhama makazi yao vimetajwa kuwa ni vichocheo vikuu vya uhaba wa chakula.WHO inasema takriban asilimia 40 ya watu ambayo ni sawa na watu milioni 40 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini DRC na, watu milioni 16 kati yao wako katika hatari ya kutokuwa na uhakika wa chakula. Jumla ya watu milioni 25 nchini humo wanategemea msaada wa kibinadamu kuweza kuishi na kuifanya DRC kuwa sasa ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners