Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNMISS yafanya kongamano na vyama vya siasa jimboni Rumbek: Uchaguzi Mkuu Sudan Kusini
    Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wake wa kwanza mwaka huu mwezi Desemba, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha kongamano la siku tatu la vyama vya siasa katika mji wa Rumbek ili kujadili masuala ambayo ni muhimu katika maandalizi ya uchaguzi huo. Mchakato wa uchaguzi nchini Sudani Kusini unafungamana na utekelezaji wa masharti ya mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2018 ambao unataka hatua za amani kuchukuliwa si tu katika ngazi ya kitaifa bali majimboni na maeneo yote ya utawala.Lakini hivi karibuni kumezuka zahma huko katika mji wa Rumbek jimboni Lakes ambako jamii zimejikuta kwenye vurugu za jumuiya mara kwa mara. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana viongozi wa mamlaka za mitaa wakaomba Umoja wa Mataifa kuja kusaidia kuleta amani na umoja kati ya vyama vya siasa vya serikali, vikosi vya usalama na mashirika ya kiraia.Christopher Muchiri Murenga, ni Mkuu wa Ofisi ya Rumber wa UNMISS, anasema "Sehemu ya kazi yetu muhimu ni kuunga mkono na kusaidia kujenga uaminifu na imani kati ya vyama vya siasa. Wote wamekaa pamoja na kujadili kufungua nafasi ya kiraia na kisiasa katika Jimbo la Lakes, na jambo moja lililotajwa zaidi na watu ni kwamba kongamano hili lisiwe katika manispaa ya Rumbek pekee.”UNMISS na washirika wa kikanda wanatumaini kuwa kongamano hili na matukio mengine kama haya yatakayo fuata nchini kote yatatengeneza jukwaa la mazungumzo ya wazi na jumuishi kati ya vyama vya siasa na wapiga kura wao kama anavyodhibitisha Waziri wa serikali za mitaa na utekelezaji wa sheria katika jimbo hilo la Lakes bwana Chol Kodowel.“Tuna jukumu la kuleta utulivu katika jumuiya yetu ili upigaji kura ufanyike katika mazingira ya amani na hilo ni jukumu si kwa serikali ya mtaa peke yake, au jimboni, bali ni jukumu letu sote kama jamii pamoja na wadau wetu.”Katika ngazi ya kitaifa, vyama vya siasa kwa sasa vinafanya kazi kwa karibu na vikundi mbalimbali ili kuwaleta katika mkondo mkuu wa mchakato wa amani na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa amani, wakidemokrasia na wa kuaminika.
    2 min
  • 11 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika yanayojiri katika Jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs, ambapo Anold Kayanda alizungumza na Katibu Mkuu Mhandisi Cyprian John Luhemeja wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zifuatazo..Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amehimiza umuhimu wa kuwekeza katika ukusanyaji wa taarifa za watu ili kuweza kufahamu matatizo, kuchambua aina ya suluhu zitakazofaa wakati wa kushughulikia matatizo hayo na kuleta maendeleo kwa haraka.Kwa mara ya kwanza hii leo dunia inaadhimisha siku ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1995 ya Srebrenica ambapo zaidi ya Waislamu 8,000 wa Bosnia waliuawa kikatili, na mabaki yao kuzikwa katika makaburi ya pamoja. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitoa ujumbe wa siku hii ametahadharisha dhidi ya ukanaji wa maujaji hayo na upotoshaji wa ukweli na kutoa wito wa kuendeleza juhudi za kutambua kila mwathirika.Na tuhitimishie huko mashariki ya kati ambapo Ofisi ya kuratibu wa misaada ya Umoja wa Mataifa OCHA imetoa takwimu za athari za mzozo huko Ukanda wa Magharibi na kueleza kuwa tangu vita kuanza kati ya Israel na Palestina mwezi Oktoba mwaka jana, zaidi ya wapalestina 550 wameuawa, zaidi ya mashambulizi elfu moja ya walowezi dhidi ya wapalestina yamerekodiwa, na takriban watu 1,400, wakiwemo watoto 660, wameyakimbia makazi yao kutokana na ghasia za walowezi na vizuizi.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili le tunakuletea ujumbe wa Balozi wa Burundi akieleza kuhusu anayofikiri itakuwa mikakati mizuri ya kukisongesha Kiswahili duniani hasa kwa kutumia balozi za kiafrika kote duniani na baadaye kuweka msukumo zaidi ndani ya UN.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Sekta ya uvuvi: Wananchi Terekeka Sudan Kusini wanufaika na mradi wa FAO
    Wananchi katika Kaunti ya Terekeka nchini Sudan Kusini wameeleza kufurahishwa na mafanikio wanayoyapata kutokana na mradi wa miaka mitano wa kuboresha mnepo wa Jamii za Wavuvi (FICREP). Cecily Kariuki na maelezo zaidi.Huyo ni Stelle Clement, mjasiriamali wa mghahawa katika jamii ya Terekeka, Equatoria ya Kati nchini Sudan Kusini. Anasema, “faida ninayopata kutokana na biashara yangu ni tegemeo la familia yangu. Inaniwezesha kuwaandalia watoto wangu mahitaji, kuweka chakula mezani, na kuhakikisha wanapata matibabu yanapohitajika.”Stelle Clement ni mmoja wa wanufaika wa mradi huu wa uvuvi ambao umeiinua sana jamii ya hapa kupitia ufadhili wa dola za Kimarekani milioni tano kutoka Ufalme wa Uholanzi ikiwa ni moja ya njia za kushughulikia baadhi ya changamoto kuu za janga la tabianchi.Samaki ndiyo bidhaa pekee ya kilimo ambayo inasafirishwa mara kwa mara kutoka Sudan Kusini kwenda nje ya nchi, na inazalisha takribani dola milioni 30 kwa mwaka.Miongoni mwa malengo mengine, mradi umeunda vikundi 20 vya wavuvi na, kwa mara ya kwanza, mradi umeanzisha kituo bora cha kuunda mitumbwi kwa ajili ya vijana.Yametolewa mafunzo kwa watengeneza mitumbwi 40 chipukizi ili kuunda mitumbwi ya kienyeji lakini sasa kwa kutumia gundi imara zaidi ili kuiewezesha mitumbwi hii kudumu kwa muda mrefu na pia kukarabatiwa kirahisi.Demissie Redeat Habteselassie, Afisa Uvuvi wa FAO nchini Sudan Kusini anaeleza zaidi akisema, “Tumeboresha tanuri za kukaushia samaki, tumeboresha chanja za kukaushia samaki, na hii imesaidia jamii za wavuvi kupata mapato zaidi, kupunguza hasara zao na kuongeza mapato yao kupitia bidhaa za samaki zilizoongezwa thamani. Na hapa, kwa kawaida, jamii za wavuvi zinategemea zaidi samaki na uwezo wao wa kuzalisha na kuongeza faida yao ni muhimu sana. Kwa hiyo, hilo ndilo mradi wetu kimsingi unafanyia kazi.”Uchumi wa Sudan Kusini unategemea zaidi mafuta, yakichangia takriban asilimia 95 ya mauzo ya nje na ni kichocheo kikuu cha mapato ya serikali.Hata hivyo, nchi inakabiliwa na ukuaji tete wa uchumi huku mfumuko wa bei ukisukuma takriban watu milioni 1.6, au takriban asilimia 12 ya watu wote, kuwa hatarini na hivyo njia mbadala za kujipatia kipato ni muhimu.
    2 min
  • WHO na wadau wake Tanzania yasaidia kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua
    Hakuna mwanamke anayepaswa kufa wakati wa kujifungua, ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Ulimwenguni WHO nchini Tanzania baada ya kushuhudia ongezeko la vifo vya wajawazito kutokana na wajawazito kupata ugumu kuvifikia vituo vya afya ilitafuta fedha ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu na kuongeza maarifa kwa wataalamu wa afya.Hatimaye WHO Tanzania wakafanikiwa kupata fedha kutoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania na kuzielekeza katika kutatua changamoto mbalimbali na sasa vifo vya uzazi vimepungua katika kanda ukanda huo. Ni kwa vipi basi ? Tuungane na Leah Mushi katika makala haya.
    4 min
  • 10 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya Uchumi wa kidijitali 2024, na uvuvi nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania kumulika afya kwa wajawazito na mashinani nchini Kenya kusikia simulizi ya mwathirika ya mafuriko.Ripoti mpya iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTAD kuhusu “Uchumi wa kidijitali 2024” imeweka bayana kuhusu athari za kimazingira za sekta ya kimataifa ya kidijitali na mzigo mkubwa wa athari hizo unaobebwa na nchi zinazoendelea.Wananchi katika Kaunti ya Terekeka nchini Sudan Kusini wameeleza kufurahishwa na mafanikio wanayoyapata kutokana na mradi wa miaka mitano wa kuboresha mnepo wa Jamii za Wavuvi (FICREP).Na kikao cha 56 cha kawaida cha Baraza la Haki za Binadamu kikiendelea huko Geneva Uswisi Katika kikao hicho Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameitaka jumuiya ya kimataifa kufikiria upya kuhusu kusitisha makubaliano yake na nchi za Kaskazini mwa Afrika kuhusu watafuta hifadhi.Katika tutakupeleka katika mitaa ya Mathare iliyoko Nairobi nchini Kenya kusikia simulizi ya mwathirika wa mafuriko.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • UNCTAD: Uchumi wa kidijitali ni lulu lakini pia unaathari za kimazingira hasa kwa nchi zinazoendelea
    Ripoti mpya iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTAD kuhusu “Uchumi wa kidijitali 2024” imeweka bayana kuhusu athari za kimazingira za sekta ya kimataifa ya kidijitali na mzigo mkubwa wa athari hizo unaobebwa na nchi zinazoendelea. Flora Nducha ameisoma ripoti hiyo na anafafanua zaidiRipoti hiyo iliyozinduliwa mjini Geneva Uswisi imetanabaisha kwamba kuanzia kwa uchimbaji wa malighafi na matumizi ya teknolojia za kidijiti hadi uzalishaji taka, inachunguza asili na ukubwa wa athari za kimazingira za sekta hii.Kinachoonekana karika ripotihiyo ni kwamba nchi zinazoendelea zinateseka kupita kiasi kutokana na athari mbaya za mazingira za uwepo na ukuaji wa sekta ya kidijitali, huku zikikosa fursa za maendeleo ya kiuchumi kutokana na pengo kubwa la kidijitali.”Ripoti hii ya kina inaangazia kwamba ingawa uboreshaji wa kidijitali huchochea ukuaji wa uchumi duniani na kutoa fursa za kipekee kwa nchi zinazoendelea, athari zake za kimazingira zinazidi kuwa kubwa na mbaya.Iesisitiza kuwa Nchi zinazoendelea zimesalia kuathiriwa kwa njia isiyo sawa kiuchumi na ikolojia kutokana na pengo liliopo la kidijitali na maendeleo lakini zina uwezo wa kutumia fursa ya mabadiliko haya ya kidijitali ili kukuza maendeleo.Katibu Mkuu wa UNCTAT Rebeca Grynspan, amesema “Kuhusu athari za Uchumi wa kidijitali ni lazima tujumuishe masuala ya mmazingira katika sera za kidijitali. Tukumbtie Uchumi wa mzunguko, tutoe kipaumbele katika ujerejelezaji wa bidhaa, utumiaji tena wa bidhaa za kidijitali, kutekeleza mikakati ya matumizi ikiwemo mufa wa matumizi ya vifaa vya kielektroniki tunavyotumia.”Amesisisitiza kuwa “Kuna haja ya kuwa na mtazamo wenye uwiano, ni lazima tukumbatie nguvu ya kidijitli ili kusongesha ujumuishaji na maendeleo endelevu huku tukikabiliana na athari za kimazingira za sekta hiyo hasa kwa kubadili mwelekeo na kuwa na Uchumi wa kidijitali wa mzunguko ukijumuisha uwajibikaji wa matumizi na uzalishhaji, matumizi ya nishati jadidifu na udhibiti wa taka za kielektroniki kwani athari za kimazingiza zinaweza kudhibitiwa.”Ripoti hiyo pia inasisitiza haja kubwa ya kushughulikia gharama za kimazingira za mabadiliko ya haraka ya kidijitali.Wasiwasi mkubwa ni pamoja na kupungua kwa malighafi za teknolojia ya kidijitali na matumizi madogo ya hewa ukaa, kuongezeka kwa matumizi ya maji na nishati na suala linalokua la taka zinaohusiana na masuala ya  kidijitali.Kadiri uboreshaji wa kidijitali unavyoendelea kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kuelewa uhusiano wake na uendelevu wa mazingira kunazidi kuwa muhimuUNCTAD inatoa wito wa kuwepo kwa sera za kimataifa zinazohusisha wadau wote kuwezesha uchumi wa kidijitali wa mzunguko zaidi na kupunguza athari za kimazingira kutokana na mfumo wa kidijitali, huku zikihakikisha matokeo ya maendeleo jumuishi.
    2 min
  • Nafasi ya elimu ya sanaa katika kueneza na kukuza lugha ya kiswahili
    Hivi karibuni dunia imeadhimisha siku ya Kiswahili duniani ikiwa ni maadhimisho ya tatu, lakini ya kwanza tangu Umoja wa Mataifa utambue Julai 7 kuwa siku ya lugha ya Kiswahili duniani. Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa maadhimisho yalifanyika Julai 3 maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kueneza na kukuza lugha ya kiswahili. Anold kayanda anakuletea kwa muhtasari yaliyojiri.
    6 min
  • 09 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia ujumbwa wa viongozi katika maadhimisho ya hivi karibuni ya siku ya Kiswahili duniani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, Libya na Kusini mwa Afrika. Mashinani inayotupeleka nchini Sudan.Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo wamesema ni dhahiri shahiri kuwa baa la njaa imeenea katika ukanda mzima wa Gaza kufuatia vifo vya hivi karibuni vya watoto wa kipalestina kutokana na njaa na utapiamlo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP limesema takriban dola milioni 409 zinahitaji mara moja ili kusaidia zaidi ya wananchi milioni 4.8 katika nchi za Malawi, Zambia na Zimbabwe.Na kikao cha 56 cha kawaida cha Baraza la Haki za Binadamu kikiendelea huko Geneva Uswisi Katika kikao hicho Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameitaka jumuiya ya kimataifa kufikiria upya kuhusu kusitisha makubaliano yake na nchi za Kaskazini mwa Afrika kuhusu watafuta hifadhi.Katika mashinani Alfatih Awad Alkheder, Mfanya biashara mwenye watoto 6 ambaye pia ni mkimbizi wa ndani kutoka Port Sudan na katika video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP anasimulia kilichomkumba yeye na familia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Mafunzo ya FAO/ILO yataniwezesha kupanga bei sahihi ya mazao- mnufaika wa mafunzo
    Elimu ya Biashara imekuwa na faida kubwa kwa wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na kilimo, ikiwemo wakulima wadogo wadogo, vijana, wanawake, na wasimamizi wa mashamba ya uzalishaji mbegu mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Kwa kutambua hilo, washiriki kutoka wilaya za mkoa huo chini ya Mradi wa Pamoja Kigoma (KJP) awamu ya Pili)  wakiwemo Vijana, wanawake, wasimamizi wa mashamba toka gereza la Ilagala huko Uvinza na kambi ya jeshi la kujenga Taifa kikosi cha 824 Kanembwa huko Kakonko walipata fursa ya kupata mafunzo ya kuendesha miradi kibiashara yaliyofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kupitia KJP. Je nini ambacho washiriki waliondoka nacho? Assumpta Massoi wa Idhaa hii anakufafanulia zaidi kwenye makala hii.
    5 min
  • Ukraine yakumbwa na wimbi jipya la mashambulizi ya makombora ya Urusi
    Nchini Ukraine Jumatatu ya leo Julai 8 imeanza na wimbi jingine la mashambulizi makubwa ya kijeshi yaliyotekelezwa na Urusi na kuua makumi ya watu, hospitali ya watoto ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa. Flora Nducha ameifuatilia taarifa hiyo. Mashambulizi haya ya leo yaliyotokea wakati watu waliopokuwa ndio kwanza wanaianza siku, yameilenga miji kadhaa ya Ukraine ikiwemo mji mkuu, Kyiv na mji mingine kama Kryvyi Rih na Pokrovsk.Akilaani mashambulizi hayo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine ambaye pia ni mratibu mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini humo, Denise Brown, amesema, "ni jambo lisilokubalika kuona kwamba watoto wanauawa na kujeruhiwa katika vita hii. Chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, hospitali zina ulinzi maalum. Raia lazima walindwe."Mbali na Hospitali ya Watoto ya Ohmatdyt huko Kyiv, miundombinu mingine ya umma pia imeharibiwa, pamoja na majengo ya biashara na makazi katika miji ikiwa ni pamoja na Dnipro, Kramatorsk, Kryviy Rih, Kyi na Pokrovsk.Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, takriban watu 20 wameuawa katika mashambulizi haya ya leo Julai 8.Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine amesema zaidi ya makombora 40 yamerushwa.
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners