Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Watu wasiojulikana wapora shehena ya msaada wa chakula nchini Sudan
    Huko  nchini Sudan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP linasema msafara wake uliokuwa umesheheni misaada ya vyakula umeshambuliwa hii leo na watu wasiojulikana. Kupitia ukurasa wake wa X, zamani Twitter, WFP imesema watu wasiojulikana waliokuwa na silaha walishambulia malori matatu yaliyokuwa na msaada huo wa chakula ukilekea jimbo la kati la Darfur.WFP inasema shehena hiyo iliyoibwa ililenga maelfu ya watu wenye uhitaji.Hivyo shirika hilo limesihi mamlaka husika kwenye eneo hilo ihakikishe waliofanya kitendo hicho wanawajibishwa.Kufuatia kitendo hicho, Clementine Nkweta-Salami ambaye ni Mratibu Mkazi wa Misaada ya kibinadamu Sudan, ametumia ukurasa wake wa X kueleza kuwa kuporwa kwa shehena hizo kunamaanisha chakula kinachohitajika hakitafikia walengwa.Amesema uporaji umefanyika wakati wanakimbizana na muda kuepusha baa la njaa Sudan na kwamba kuwaibia walengwa chakula ni jambo la kusikitisha.
    1 min
  • 01 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini Sudan, na uhamasishaji wa wakulima nchini Zambia kuachana na kilimo cha tumbaku na badala yake kulima mazao mbadala. Makala inatupeleka nchini CAR na mashinani nchini Ghana, kulikoni?Huko nchini Sudan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP linasema msafara wake uliokuwa umesheheni misaada ya vyakula umeshambuliwa hii leo na watu wasiojulikana.Nchini Zambia, mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Kanda ya Afrika wa kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo cha tumbaku na badala yake kulima mazao mbadala umeanza kuzaa matunda kama anavyoelezea mmoja wa wakulima walioitikia wito huo.Makala inakupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kumsikiliza Afisa Uhusiano wa Kikosi cha 7 kutoka Tanzania kinacholinda amani  chini ya Ujumbe wa kulinda amani nchini CAR, MINUSCA, Kapteni John Zablon Mshamy  akieleza shughuli za kitengo cha kijeshi kinachofahamika kama CIMIC katika shughuli za ulinzi wa amani.Mashinani ikiwa hivi karibuni dunia itasheherekea siku ya Kiswahili Duniani ambayo bila shaka ni bidhaa ya kimataifa, tunakuletea ujumbe wa Dkt. Felix Sosoo, Mhadhiri wa lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Ghana akitoa maoni yake kuhusu wanaobeza lugha ya Kiswahili.”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    10 min
  • Mkulima Zambia: Tumegeukia mazao ya chakula kulinda afya badala ya tumbaku
    Nchini Zambia, mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Kanda ya Afrika wa kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo cha tumbaku na badala yake kulima mazao mbadala umeanza kuzaa matunda kama anavyoelezea mmoja wa wakulima walioitikia wito huo.Tuko wilaya ya Chipangali nchini Zambia ambako video ya WHO kanda ya Afrika inaanzia katikati ya shamba lililostawi la mahindi na mtu mmoja akitembea katikati na kisha anajitokeza akiwa na tabasamu! Huyu ni Titus Mwanza, mkulima wa zamani wa tumbaku ambaye amekipa kisogo kilimo hicho na kugeukia mazao mengine. Kulikoni?“Niliacha kulima tumbaku miaka minne iliyopita Kilichonifanya niache kulima zao hili ni matatizo yaliyokuweko kwenye familia yangu, na faida haikuwa nzuri. Vile vile ugonjwa wa saratani au kansa unaohusishwa na zao hili. Wale wanaovuta wanapata aina mbali mbali za magonjwa.”Uelewa huu unafuatia ziara ya mwishoni mwa mwaka 2022, ambapo Bwana Mwanza na wakulima wenzake wawili kutoka Zambia walishiriki ziara ya mafunzo nchini Kenya ambako mashamba ya kwanza kabisa yasiyo na tumbaku yalianzishwa mwaka 2021. Katika mashamba hayo wakulima 6,000 wa tumbaku tayari wameacha kulima zao hili na wanalima mazao mbadala.Baada ya kurejea Zambia anasema,“Niliacha kilimo cha tumbaku na kuanza kulima mazao mengine. Mazao kama maharage ya soya, alizeti, karanga na maharage. Hayo ndio mazao ninayolima kwa sasa.”Bwana Mwanza amekuwa mkulima kiongozi akifundisha wenzake kilimo mbadala na tayari amefundisha wakulima 50.“Kinachotuhamasisha ni kwamba tunalima kile ambacho baadaye tunakula. Tunalima mahindi, kisha tunakula. Tunalima mbaazi, kisha tunakula. Tunatengeneza maziwa kutokana na maharage ya soya. Vile vile tunatumia maharage ya soya kutengeneza soseji. Ni kitu ambacho tunalima na kisha tunakula. Ni chakula chenyewe. Tumbaku sio chakula, tumbaku ni dawa.”Video inatamatika huku Bwana Mwanza akiwa kwenye shamba lake la mahindi lililostawi vizuri, mahindi yamekomaa na tabasamu kamili usoni mwake.
    3 min
  • 28 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya mwaka 2024 ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, na juhudi za mashirika ya Umoja wa Mataifa za kuwawezesha wakulima nchini Somalia. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani ujumbe ubunifu na vijana barani Afrika.Bila uwekezaji mkubwa na kuongeza hatua, kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kutasalia kuwa mgumu, imeonya Ripoti ya mwaka huu 2024 kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa malengo hayo ikiwa imesalia miaka sita pekee kufikia muda ambao ulimwengu ulijiwekea kuwa umeyatimiza malengo yote 17.Huku takriban watu milioni 7 nchini Somalia wakihitaji msaada wa kuokoa maisha mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linahimiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kuunga mkono Wasomali wanaokabiliwa na athari za njaa,mabadiliko ya tabianchi, migogoro na kufurushwa makwao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania anamulika usaidizi wa shirika hilo kwa manusura wa mafuriko yaliyokumba taifa hilo la Afrika Mashariki.Mashinani tutasikia jinsi shirika la umoja wa mataifa la Afya ulimwenguni, WHO linakuza ubunifu miongoni mwa wanasayansi vijana wa afya barani Afrika      ili kuboresha ufanisi, ubora wa huduma za afya  na maendeleo katika matibabu na tiba.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa yaonya kuwa dunia inashindwa kutimiza SDGs
    Bila uwekezaji mkubwa na kuongeza hatua, kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kutasalia kuwa mgumu, imeonya Ripoti ya mwaka huu 2024 kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa malengo hayo ikiwa imesalia miaka sita pekee kufikia muda ambao ulimwengu ulijiwekea kuwa umeyatimiza malengo yote 17.Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo Juni 28 inafichua kuwa ni asilimia 17 tu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ndio yako katika mwenendo mzuri, huku karibu nusu ikionesha maendeleo madogo au ya wastani, na zaidi ya theluthi moja yamekwama au kurudi nyuma. Athari zinazoendelea za janga la COVID-19, mizozo inayoongezeka, mivutano ya kijiografia na kuongezeka kwa machafuko ya tabianchi kumezuia maendeleo kwa kiasi kikubwa.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo asubuhi ya leo kwa saa za New York, Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anasema,"kushindwa kwetu kupata amani, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuongeza fedha za kimataifa kunadhoofisha maendeleo. Ni lazima tuharakishe hatua kwa ajili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu na hatuna muda wa kupoteza."Kulingana na ripoti hiyo, watu zaidi ya milioni 23 walisukumwa katika ufukara na zaidi ya watu milioni 100 zaidi walikuwa wakikabiliwa na njaa mwaka wa 2022 ikilinganishwa na mwaka 2019. Idadi ya vifo vya raia katika vita vya kijeshi iliongezeka mwaka jana 2023. Mwaka huo pia ulikuwa wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa huku halijoto duniani ikikaribia kiwango cha juu cha nyuzijoto 1.5 za Selsiasi.
    2 min
  • FAO yafanikisha miradi ya kusaidia jamii nchini Somalia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
    Huku takriban watu milioni 7 nchini Somalia wakihitaji msaada wa kuokoa maisha mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linahimiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kuunga mkono Wasomali wanaokabiliwa na athari za njaa,mabadiliko ya tabianchi, migogoro na kufurushwa makwao. FAO sio kwamba wao wanahimiza wengine kusaidia wasomali, bali wao pia na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa wanatekeleza miradi mbalimbali yakuwasaidia wananchi wa Somalia hususan katika kuhakikisha wana uhakika wa kujipatia chakula na kupunguza athari za vichocheo muhimu vya uhaba wa chakula ambavyo ni kama vile mafuriko, ukame, bei juu za chakula pamoja na migogoro.Programu zinazotekelezwa ni pamoja na kuboresha kinga na kujiandaa kwa majanga ya chakula katika jamii za vijijini, kuimarisha uzalishaji wa mifugo, na kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu kilimo kinachozingatia hali ya hewa.Bi. Edeba Ali Hassan (33), ni mkulima aliyelazimika kukimbia huko Bakool kutokana na machafuko na kuhamia Dolow, ni mnufaika wa programu iitwayo Mpango wa Hatua za Pamoja za Ustahimilivu – JOSP unaotekelezwa na FAO kwa ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP).Bi. Edeba anasema programu hiyo imempatia fedha taslimu, pembejeo za kilimo kwa misimu miwili, amepewa shamba pamoja na mfumo wa umwagiliaji unaotumia nishati ya jua.“Nina watoto 10, na siwezi kuwahudumia kwa sababu hakuna kazi isipokuwa kilimo, ndiyo maana nilijiunga na Mpango wa Pamoja wa Ustahimilivu.”Alexander Jones, Mkurugenzi, Idara ya Uhamasishaji Rasilimali wa FAO anasema programu wanazozitekeleza nchini Somalia zinalenga zaidi kusaidia watu katika kupata uhakika wa chakula katika maeneo ambayo mara kwa mara yanaathiriwa na ukame na mafuriko.“Mradi wa JOSP unasaidia kukarabati eneo kubwa lenye takriban wanufaika milioni 1.5 kupitia usimamizi wa maji, kupitia programu za kijamii za maji, kwa ajili ya maeneo yanayoathirika na mafuriko na ukame.”Mpango huu mkubwa wa kuleta mabadiliko nchini Somalia unatekelezwa kwa ufadhili kutoka kwa Ubalozi wa Uingereza mjini Mogadishu, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kujenga Amani (UNPBF), pamoja na michango inayotarajiwa kutoka kwa shirika la Marekani la misaada ya maendeleo USAID na Mfuko wa Pamoja wa Somalia (SJF).
    2 min
  • Methali: “Chombo cha kuzama hakina usukani.”
    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Chombo cha kuzama hakina usukani.”
    2 min
  • 27 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiangaazia hafla maalum ya UNICEF na wadau wake pamoja na wasanii iliyofanyika Nairobi Kenya, mada ikiwa “Ungana na watoto wa Sudan”. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za maandamano Kenya, Janga la njaa Sudan, na MSMEs. Katika kujifunza kiswahili tunakuletea uchambuzi wa methali.Kufuatia madhila yaliyotokana na maandamano makubwa nchini Kenya dhidi ya mswada wa fedha, leo Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imeeleza kwamba Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk amesikitishwa na vifo na kujeruhiwa kwa watu.Zaidi ya Wasudan milioni 25 yaani zaidi ya nusu ya idadi ya watu wote nchini humo wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ya viwango vya Uhakika wa Chakula (IPC) kutokana na tathimini iliyofanywa kati ya mwishoni mwa mwezi Aprili na mapema mwezi huu wa Juni.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya biashara ndogo sana, ndogo na za ukubwa wa kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii amesisitiza jukumu muhimu la wajasiriamali hao katika uchumi wa kimataifa, ikiangaziwa michango yao katika uundaji wa nafasi za kazi, ukuaji wa uchumi, na uwezeshaji wa makundi mbalimbali yaliyotengwa.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Chombo cha kuzama hakina usukani.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya inaathiri afya, pata usaidizi uondokane nazo
    Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO imesema mamilioni ya vifo vinachangiwa na unywaji pombe na matumizi ya dawa za kulevya na imetoa wito wa haraka wa kutekeleza lengo namba 3.5 la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG la kupunguza matumizi ya pombe na dawa za kulevya na kuboresha upatikanaji wa matibabu bora kwa matatizo ya matumizi ya dawa. Halikadhalika leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya kutokomeza matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na ulanguzi wa madawa hizo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa na Uhalifu (UNODC) wamechapisha ripoti yao inayosisitiza haki ya afya kwa wote ikiomba Umoja wa Mataifa kuongza kasi katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa. Kevin Keitany wa redio Washirika wetu Domus FM anatupeleka nchini Kenya kufuatilia juhudi za mashirika ya kiraia na serikali hasa katika huduma za afya kwa waathirika wa madawa ya kulevya na pombe.
    5 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners