Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 26 JUNI 2024
    Hii leo jaridani Tunafuatilia machafuko yaliyotokana na maandamano yaliyoanza nchini Kenya, na ripoti ya utumiaji wa dawa za kulevya. Makala tunarejea nchini Kenya kufuatilia matibabu ya waathirika wa dawa za kulevya na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?Viongozi wa Umoja wa Mataifa wamekazia wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres kwa mamlaka za Kenya kufuatia machafuko yaliyotokana na maandamano yaliyoanza nchini humo Juni 18 kupingwa muswada wa fedha wa mwaka 2024.Kuibuka kwa dawa mpya za kulevya za kutengenezwa na rekodi ya usambazaji na mahitaji ya dawa zingine kumeongeza athari za dawa hizo ulimwenguni, na kusababisha kuongezeka kwa shida za utumiaji wa dawa za kulevya na madhara kwa mazingira, imesema leo Ripoti ya Dunia ya Dawa ya 2024 iliyozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa ya kukabili dawa za kulevya na uhalifu, UNODC.Katika makala leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya kutokomeza matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na ulanguzi wa madawa hizo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa na Uhalifu (UNODC) wamechapisha ripoti yao inayosisitiza haki ya afya kwa wote ikiomba Umoja wa Mataifa kuongza kasi katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa. Kevin Keitany wa redio Washirika wetu Domus FM anatupeleka nchini Kenya kufuatilia juhudi za mashirika ya kiraia na serikali hasa katika huduma za afya kwa waathirika wa madawa ya kulevya na pombe.Mashinani tunaelekea nchini Sudan kusikia simulizi ya mwathirika wa vita inayoendelea nchini humo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Viongozi wa UN wasihi haki ya watu kuandamana Kenya iheshimiwe - Kenya
    Viongozi wa Umoja wa Mataifa wamekazia wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres kwa mamlaka za Kenya kufuatia machafuko yaliyotokana na maandamano yaliyoanza nchini humo Juni 18 kupingwa muswada wa fedha wa mwaka 2024. Maandamano yalianza Juni 18, yakiongozwa na vijana wakitaka muswada huo wa fedha ukataliwe wakidai yaliyomo yatasababisha maisha kuwa magumu zaidi.Mathalani ongezeko la kodi kwenye bidhaa muhimu kama vile mkate na taulo za kike, mapendekezo ambayo baadaye yaliondolewa kwenye rasimu na Bunge.Wabunge waliupitisha muswada huo jana Jumanne kitendo kilichochochea maandamano zaidi katika kaunti mbali mbali za Kenya na ambapo vyombo vya habari vinaripoti vifo zaidi ya watu 18, na wengine wamejeruhiwa.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia msemaji wake alisema..“Ni muhimu sana haki za watu kuandamana kwa amani zizingatiwe. Kama tusemavyo duniani kote. Ni muhimu pia mamlaka zihakikishe kuwa haki hizo zinalindwa, na matukio ya vifo mikononi mwa vikosi vya usalama yachunguzwe. Watu wawajibishwe, polisi wa Kenya, mamlaka na jeshi wajizuie, na kwa waandamanaji waandamane kwa amani. »Inger Anderesen ambaye ni Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP pamoja na kuunga mkono kauli ya Katibu Mkuu amesihi mamlaka za Kenya kuhakikisha maandamano ya amani yanaweza kufanyika nchini Kenya.Bi. Andersen amesikitishwa pia na ripoti za vifo na majeruhi na kutuma salamu za rambirambi kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao.Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya, Stephen Jackson yeye ametumia ukurasa wake wa X kuchapisha ujumbe wa Katibu Mkuu Guterres.Wakati huo huo, Rais wa Kenya William Rutto amehutubia taifa kwa mara ya pili ndani ya chini ya saa 24 na kusema pamoja na kwamba bunge limepitisha na mabadiliko, na wananchi wamezungumza kupitia maandamano kuukataa, ameamua kutotia saini muswada huo na hivyo utaondolewa bungeni na amekubaliana na wabunge kuwa ni uamuzi wao wa pamoja.
    2 min
  • Utumiaji wa dawa za kulevya umeongezeka 2024 - Ripoti ya dawa za kulevya
    Kuibuka kwa dawa mpya za kulevya za kutengenezwa na rekodi ya usambazaji na mahitaji ya dawa zingine kumeongeza athari za dawa hizo ulimwenguni, na kusababisha kuongezeka kwa shida za utumiaji wa dawa za kulevya na madhara kwa mazingira, imesema leo Ripoti ya Dunia ya Dawa ya 2024 iliyozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa ya kukabili dawa za kulevya na uhalifu, UNODC . Kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya ulimwenguni imeongezeka na kufikia watu milioni 292 mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 katika kipindi cha miaka 10.Akizindua ripoti hiyo jijini Vienna Austria Mkurugenzi Mkuu wa UNODC Ghada Waly ameeleza kuwa uzalishaji wa dawa za kulevya na matumizi yake unazidisha ukosefu wa utulivu na usawa wakati huo huo ukisababisha madhara makubwa kwa afya, usalama na ustawi wa watu.“Tunahitaji kutoa matibabu yaliyofanyiwa uchunguzi na kuwa na Ushahidi wa kuweza kusaidia wale walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya huku tukilenga soko haramu la dawa za kulevya na kuwekeza zaidi katika kuzuia matumizi ya dawa hizo.” Amesema Bi. Waly.Matumizi ya bangi yamesalia kutumika zaidi duniani kote ambapo kuna watumiaji watumiaji milioni 228.Ripoti hiyo pia imesema uzalishaji wa cocaine umeweka rekodi mpya ya juu ya uzalishaji wa tani 2,757 mwaka2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 zaidi tangu mwaka 2021.Ingawa wastani wa watu milioni 64 duniani kote wanakabiliwa na matatizo yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya, ni mtu mmoja tu kati ya 11 anayetibiwa.Wanawake wanapata huduma ndogo zaidi za matibabu ikilinganishwa na wanaume.Ripoti hiyo imeeleza jinsi haki ya afya ni haki ya binadamu inayotambulika kimataifa ambayo ni ya binadamu wote, hivyo kutaka wale wote wanaotumia dawa za kulevya kupata haki yao ya matibabu hatakama wameshikiliwa na vyombo vya dola.Kusoma ripoti kamili bofya hapa.
    2 min
  • FAO yaimarisha Afya ya Mifugo Kupitia mradi wa ISAVET nchini Tanzania
    Nchini Tanzania, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaendesha programu ya mafunzo yanayolenga kuboresha ujuzi wa wataalamu wa mifugo katika kudhibiti magonjwa ya wanyama na kuimarisha afya ya mifugo ili kuihakikishia jamii uhakika wa chakula na chakula salama. John Kabambala wa redio washirika wetu KidsTime ya mkoani Morogoro Tanzania amezungumza na wadau kandoni mwa mafunzo hayo. 
    6 min
  • 25 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulikaza juhudi za  kuimarisha afya ya mifugo ili kuihakikishia jamii uhakika wa chakula na chakula salama. Pia tunakuletea muhutasari wa habari zikiwemo za Gaza, mabaharia, na ripoti ya ya matumizi ya pombe. Mashinani tunasalia na siku ya mabaharia duniani. Katika Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati tathmini mpya iliyofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani WFP imethibitisha wasiwasi wa kuendelea kuwepo kwa viwango vya njaa ambapo asilimia 96 ya wananchi wanakabiliwa na uhaba wa chakula.Leo ni siku ya mabaharia duniani ikibeba maudhui ya kuangalia usalama wao kazini. Katika ujumbe wake kwa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kukomeshwa kwa vitendo vya kiharamia vya meli kutekwa nyara na kueleza kuwa mabaharia hawapaswi kuwa waathiriwa wa migogoro ya kijiografia na kisiasa.Na ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO imeonesha vifo milioni 2.6 kwa mwaka vinachangiwa na unywaji pombe hii ikiwa ni sawa na asilimia 4.7 ya vifo vyote duniani, na vifo laki sita kwa matumizi ya dawa za kulevya.Mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabaharia, na kupitia ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya baharí, IMO Arsenio Dominguez anawatakia kila la heri mabaharia wote akiwaalika katika meza ya kubonga bongo kuhusu masuala ya usalama wa baharini.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • India: Majiko yaliyoboreshwa yaondolea adha wanawake kuvaa miwani wakipika
    Katikati ya bonde la mto Ganges kaskazini mwa India, ndiko liko jimbo la Bihar ambalo sasa linahaha kutokana na uchafuzi wa hewa, kwani moshi utokao kwenye majiko ya kuni na samadi ya ng’ombe yanasababisha kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa hewa. Licha ya maendeleo makubwa ya kutumia gesi kama chanzo cha nishati, halikadhalika nishati itokanayo na samadi, bado familia au kaya maskini zinashindwa kumudu vyanzo hivyo na kujikuta vikutumia kuni au samadi ya ng’ombe kupikia, ambavyo huchafua hewa. Sasa Benki ya Dunia imewezesha kuundwa kwa vikundi vya kujiwezesha au SHGs ambapo wanawake wanapatiwa elimu ya masuala mbali mbali ikiwemo nishati salama na hivyo kuboresha afya zao. Assumpta Massoi kupitia video ya Benki ya Dunia amefuatilia mradi huo na kuandaa makala hii. 
    3 min
  • UNMISS ziarani Nadiangere na uzinduzi wa shule ya msingi
    Ikiwa ni moja ya majukumu yake, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wakishirikiana na mamlaka za mitaa za nchi hiyo umefanya ziara maalum katika Kijiji cha Nadiangere na kusikiliza kero za wananchi pamoja kuzindua shule mpya ya msingi. Ndege ya UNMISS ikiwa na timu ya walinda amani na wawakilishi kutoka serikali za mitaa inafika kijiji cha Nadiangere kilichoko katika jimbo la Equatorial Magharibi na kulakiwa kwa shamsham na wananchi wa kijiji hicho wakiamini msemo wa Kiswahili usemao “Mgeni njoo mwenyeji apone.” Katika mkutano wa pamoja, wananchi hao walieleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo ukosefu wa huduma za kimsingi kama viles hule, huduma za afya pamoja na usalama. Wananchi hao wakaeleza uhaba huu umechangiwa na kuwasili kwa wakimbizi wa ndano wanaokimbia kuzuka kwa vurugu za wenyewe kwa wenyewe hivi karibuni huko karibu na eneo la Tambura. Severina Angelo mwenye umri wa miaka 21, mama wa watoto wawili akapaza sauti.“Tumechoka sana, tunahitaji amani, tumeshateseka sana. Tunahitaji shule, tunahitaji hospitali na vitu vingine vingi ambavyo tunakosa.”Jane Lanyero Kony, Ni Mkuu wa Ofisi ya UNMISS kwa jiji la Yambio na anawaeleza wanakijiji hao kuwa “Subira yavuta heri.”“Unajua sisi tuko hapa kusikiliza changamoto zenu ni zipi na kisha tunaporudi ofisini tunaenda kuangalia ni kwa kiwango gani tunaweza kuhamasisha upatikanaji wake miongoni mwa jumuiya ya Umoja wa Mataifa. Kama UNMISS, tunaendelea kufanya kile ambacho ni mamlaka yetu, ambacho ni, ulinzi wa raia. Tunaendelea kufanya kazi na serikali, ili kukamilisha juhudi zao za kulinda kila raia nchini Sudan Kusini.”Mbali na kuwasikilisha wananchi pia wamezindua shule ya msingi iliyojengwa kwa ufadhili wa UNMISS katika eneo hilo. Shule hiyo ina vyumba vitatu vya madarasa, ofisi ya walimu, na inatoa mazingira bora ya kujifunzia kwa zaidi ya wasichana na wavulana 300.
    2 min
  • 24 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu Gaza hasa kwa watoto, na ziara maalum ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS. Makala inatupeleka nchini India na mashinani nchini Uganda, kulikoni? Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, Philippe Lazzarini, hii leo Juni 24 ametahadharisha vikali kwamba UNRWA itaporomoka kama ufadhili hautapatikana haraka, na "kizazi kizima" cha watoto wako katika hatari ya kuangukia kwenye "umaskini, chuki na migogoro ya baadaye”. Ikiwa ni moja ya majukumu yake, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wakishirikiana na mamlaka za mitaa za nchi hiyo umefanya ziara maalum katika Kijiji cha Nadiangere na kusikiliza kero za wananchi pamoja kuzindua shule mpya ya msingi..Katika makala Assumpta Massoi anatupeleka India kumulika jinsi mradi wa Benki ya DUnia umeondolea kaya adha ya changamoto za kiafya na kiuchumi zitokanazo na matumizi ya kuni na samadi ya ng'ombe kwenye kupikia.Na mashinani tunaelekea nchini Uganda kusikia ujumbe wa kiongozi wa jamii ambaye ni mkimbizi kutoka Sudan Kusini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • ‘Kizazi kizima’ kinaweza kupotea Palestina, Mkuu wa UNRWA aonya
    Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, Philippe Lazzarini, hii leo Juni 24 ametahadharisha vikali kwamba UNRWA itaporomoka kama ufadhili hautapatikana haraka, na "kizazi kizima" cha watoto wako katika hatari ya kuangukia kwenye "umaskini, chuki na migogoro ya baadaye”. Katika ombi la uungwaji mkono wa kisiasa na kifedha kutoka kwa Mataifa Wanachama  wa Umoja wa Mataifa alilolitoa mbele ya Kamisheni ya Ushauri ya UNRWA mjini Geneva, Uswisi, Philippe Lazzarini amesisitiza kwamba shirika hilo linajikongoja chini ya uzito wa mashambulizi yasiyokoma huko Gaza baada ya karibu miezi tisa ya mashambulizi makali ya Israel.Mbali na wafanyakazi 193 wa UNRWA waliouawa tangu mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas na utekaji nyara kuzusha vita, Bwana Lazzarini ameeleza kwa kina ukubwa wa uharibifu huo katika majengo ya Umoja wa Mataifa akisema sasa shinikizo kwa shirika hilo ni kubwa zaidi.Amesema zaidi ya miundombinu 180  imevunjwa au kuharibiwa tangu Oktoba 7 na takribani watu 500 wameuawa wakitafuta ulinzi chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa."Majengo yetu yametumiwa kwa madhumuni ya kijeshi na Israel, Hamas na makundi mengine yenye silaha ya Palestina," mkuu huyo wa UNRWA amewaeleza wajumbe akiongeza kuwa, misafara ya UNRWA imeshambuliwa na hivyo nafasi ya uutendaji kazi inapungua.Akiangazia jinsi Gaza ilivyo sasa, Lazzarini amesema ni kuzimu kwa zaidi ya watu milioni mbili huko, akibainisha kuwa watoto wanaendelea kufa kwa utapiamlo na upungufu wa maji mwilini, "huku chakula na maji safi vikisubiri kwenye malori" nje ya eneo hilo.
    2 min
  • UN Women: Wanawake Gaza hawataki kufa au kuzika wapendwa wao
    Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea mjini Yerusalemu, Bi. Guimond amesema unapoingia tu kwenye kivuko cha Shalom na lango linafungwa, unahisi umefungiwa kwenye dunia ya uharibifu. Kuanzia shule, hospitali, makazi yaliyolundikana watu na uhaba wa vitu, watu wakihaha kusaka usalama, wanawake wakimuuliza vita itakoma lini? Na zaidi ya yote. “Wakazi wa Gaza wanataka hii vita ikome. Kila siku ambayo mzozo huu unaendelea, inazidi kuleta uharibifu na mauaji. Lazima hii ikome. Wavulana na wasichana walikuwa wananiuliza ni lini vita hii itaisha? Nami sikuwa na jibu la kuwapatia.” Akaendelea kusema.. “Gaza ni zaidi ya simulizi zaidi ya milioni mbili za kupoteza. Kila mwanamke niliyekutana naye ana simulizi ya kupoteza mtu. Zaidi ya wanawake 10,000 wamepoteza wapendwa wao. Zaidi ya familia 6,000 zimepoteza mama zao. Wanawake na wasichana milioni 1 wamepoteza utu wao, makazi yao, familia zao na kumbukumbu zao.” Bi. Guimond akasema kwa sasa.."Swali si kwamba ni nini wanawake wanahitaji: Swali linapaswa kuwa ni nini wanawake hawahitaji. Wanawake hawataki kufa, hawataki kuzika wapendwa wao, hawataki kubakia wenyewe kupata machungu.”
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners