Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UN Women: Wanawake Gaza hawataki kufa au kuzika wapendwa wao
    Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea mjini Yerusalemu, Bi. Guimond amesema unapoingia tu kwenye kivuko cha Shalom na lango linafungwa, unahisi umefungiwa kwenye dunia ya uharibifu. Kuanzia shule, hospitali, makazi yaliyolundikana watu na uhaba wa vitu, watu wakihaha kusaka usalama, wanawake wakimuuliza vita itakoma lini? Na zaidi ya yote. “Wakazi wa Gaza wanataka hii vita ikome. Kila siku ambayo mzozo huu unaendelea, inazidi kuleta uharibifu na mauaji. Lazima hii ikome. Wavulana na wasichana walikuwa wananiuliza ni lini vita hii itaisha? Nami sikuwa na jibu la kuwapatia.” Akaendelea kusema.. “Gaza ni zaidi ya simulizi zaidi ya milioni mbili za kupoteza. Kila mwanamke niliyekutana naye ana simulizi ya kupoteza mtu. Zaidi ya wanawake 10,000 wamepoteza wapendwa wao. Zaidi ya familia 6,000 zimepoteza mama zao. Wanawake na wasichana milioni 1 wamepoteza utu wao, makazi yao, familia zao na kumbukumbu zao.” Bi. Guimond akasema kwa sasa.."Swali si kwamba ni nini wanawake wanahitaji: Swali linapaswa kuwa ni nini wanawake hawahitaji. Wanawake hawataki kufa, hawataki kuzika wapendwa wao, hawataki kubakia wenyewe kupata machungu.”
    3 min
  • UNHCR: Utoaji wa vitambulisho kwa wakimbizi nchini Ethiopia waboresha maisha yao
    Wakati dunia hapo jana Juni 20 ikiwa imeadhimisha siku ya wakimbizi duniani na wito kutolewa kila kona wa kuhakikisha wakimbizi wanajumuishwa katika masuala yote ya kuweza kuwasaidia kustawi katika nchi wanayopatiwa hifadhi hii leo tunaelekea nchini Ethiopia kujionea namna mradi wa kutoa vitambulisho vya kitaifa ambao unajumuisha wakimbizi na wasaka hifadhi ulivyobadiliasha maisha ya wakimbizi. Makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inathibitisha namna mradi huo wa vitambulisho vya kitaifa uliofadhiliwa na Benki ya Dunia umeleta matumaini pamoja na upatikanaji wa ajira kwa wakimbizi na hivyo kuwaondoa katika kundi la watu tegemezi kwani sasa wanaweza kufanya shughuli za kuwaingizia kipato. Leah Mushi anatujuza zaidi. 
    4 min
  • Jengo la uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko mpakani Mutukula lakabidhiwa kwa serikali ya Tanzania
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni (WHO) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), hivi karibuni limekabidhi kwa Wizara ya Afya nchini humo jengo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza wanapopita katika mpaka wa Mutukula unaounganisha Tanzania na Uganda kaskazini. Hatua hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mapema dhidi ya milipuko ya magonjwa imekuja ukiwa umetimia mwaka mmoja kamili tangu  mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya virusi vya Marburg ulipotangazwa kuisha kabisa nchini Tanzania baada ya kuwa umetokea mwanzoni mwa mwaka jana 2023  katika mkoa wa Kagera kaskazini magharibi mwa nchi.Dkt. Janeth Masuma, Afisa wa Kitengo cha WHO Tanzania cha kuzuia na kudhibiti maambukizi anasema, “kwa hiyo kwa kuwa na mafanikio haya makubwa ya jengo la utambuzi wa wagonjwa katika mpaka wa Mutukula kutasaidia uchunguzi wa haraka na kuwatenganisha wote wanaohisiwa kuwa na maambukizi ili kuhakikisha mipaka yote imelindwa, kulinda nchi nyingine na kuhakikisha kwamba hakuna wasafiri wowote watapeleka ugonjwa nje ya Tanzania kwa mujibu wa mapendekezo na wajibu wa afya kimataifa.”Salum Rajab Kimbau, Mratibu wa Chanjo wa Mkoa wa Kagera anaeleza ilivyo faida kubwa kuwa na jengo la namna hii mpakani akisema, “huu mradi kiujumla una faida kwenye mkoa. Tumeupokea na kufurahi na pia furaha hii iko upande wa halmashauri ya mkoa n anchi kwa ujumla. Mradi una sehemu mbili za matibabu na kinga. Awali tulikuwa tunatumia hema moja ambalo lilikuwa linakusanya wahisiwa wote wa kike na wa kiume lakini hata mazingira yenyewe siyo rafiki kwa maana ya joto kali lakini pia akiingia mgonjwa badala ya kupona kwa haraka au badala ya kukaa kustahimili vizuri inakuwa kazi.”Kituo hiki ni moja ya afua nyingi zinazoendelea ili kuhakikisha uimarishaji wa mifumo ya afya nchini Tanzania ili kuongeza kasi ya ajenda ya afya kwa wote.
    2 min
  • 21 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake huko Gaza, na masuala ya afya nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Ethiopia na mashinani tunasalia nchini Tanzania, kulikoni? Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni (WHO) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), hivi karibuni limekabidhi kwa Wizara ya Afya nchini humo jengo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza wanapopita katika mpaka wa Mutukula unaounganisha Tanzania na Uganda kaskazini.Makala inatupeleka nchini Ethiopia ambako nchi hiyo kwasasa inatekeleza mpango wa kihistoria wa utoaji wa vitambulisho vya kitaifa unaojumuisha wakimbizi na wasaka hifadhi.Na mashinani tutakepeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe wa watoto kuhusu elimu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • Methali: “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”
    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”
    2 min
  • 20 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Japan kufuatilia harakati za kusongesha teknolojia rafiki na nafuu ili dunia iwe mahali salama kwa miti na binadamu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo, na uchambuzi wa methali.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi, Umoja wa Mataifa umeitumia siku hii kutoa wito wa mshikamano na wakimbizi kote duniani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema, "wanapopewa fursa, wakimbizi hutoa mchango mkubwa kwa jamii zinazowahifadhi."Mashambulizi ya Israel kwa kutumia mabomu kutoka angani, nchi kavu na baharini yanaendelea kuripotiwa katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo zaidi vya raia, kuhama makazi yao, na uharibifu wa nyumba na miundombinu mingine ya raia, imeeleza ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limeipongeza Chad kwa kufanikiwa kuutokomeza ugonjwa wa malale. Chad ni nchi ya kwanza kwa mwaka huu kutambuliwa kwa kutokomeza ugonjwa huo ulio katika kundi la magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika (NTDs) na inakuwa nchi ya 51 kufikia lengo kama hilo ulimwenguni. Ugonjwa huu husambaa kutokana na binadamu kung’atwa na mdudu Mbung’o mwenye maambukizi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • Rais wa Baraza Kuu: Redio Miraya ninakutakieni heri ya miaka mingine 18 ya utendaji
    Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis mwishoni mwa wiki Juni 16 ametumia sehemu ya muda wa ziara yake nchini Sudan Kusini kukitembelea kituo cha redio Miraya kinachoendeshwa chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS huku mwisho wa mwezi huu wa Juni redio hiyo ikitimiza miaka 18 tangu kuanzishwa kikisalia kuwa chombo muhimu kwa amani na ustawi wa watu wa Sudan Kusini. Pia akiwa kituoni hapo akaitumia nafasi hiyo kuongelea masuala mengine muhimu ya kijamii ikiwemo elimu. Anold Kayanda ameandaa makala hii kutokana na video iliyoratibiwa na UNMISS.
    4 min
  • Hongera Tanzania kwa kuanzisha kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura - UNDRR
    Nchi ya Tanzania imepongezwa kwa kuzindua kituo cha kutoa taarifa na maonyo ya mapema kuhusu dharura hivyo kuwezesha wadau mbalimbali kuchukua hatua stahiki kabla ya majanga kutokea. Akihudhuria uzinduzi rasmi wa kituo hicho cha kwanza nchini Tanzania cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura (EOCC) ambacho kimeanzishwa chini ya Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Tahadhari za Mapema na Mfumo wa kuchukua Hatu za Mapema wa Umoja wa Afrika AMHEWAS, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Kupunguza Hatari za Maafa Kamal Kishore, amelipongeza taifa hilo na kusema uzinduzi huo unaashiria hatua kubwa katika safari ya nchi kuelekea kujenga ustahimilivu wa majanga.“Leo tumezindua chumba cha hali ya hewa Dodoma Tanzania, Hii ni hatua muhimu, matokeo, matokeo ya muunganiko wa taasisi mbalimbali zinazoshirikiana katika kituo hiki yatasaidia kuwezesha jamii kuchukua hatua stahiiki na kulinda maisha na mali za wananchi.” Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu Dkt Jim. J. Yonazi amesema kituo hicho kilicho chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, na kitafanya kazi kuchanganya takwimu wanazo kusanya wakati halisi kuhusu hatari zinazojitokeza pamoja na takwimu kuhusu majanga yaliyopita ili kutoa utabiri na taarifa kwa wakati.“Tumezindua chumba hiki na kinakwenda kwa kweli kusaidia Tanzania kutabiri taarifa za aina mbalimbali za maafa yakiwemo mafuriko, ukame nakadhalika. Na hili ni muhimu sana kwetu kuweza kupanga mikakati, jinsi gani tunaweza kuzuia, lakini tena ikitokea, jinsi ya kujidhatiti baada ya majanga, na tena jinsi ya kutoa taarifa zaidi kwa wadau wetu jinsi ya kurejesha maisha katika hali yake ya awali.”Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza hatari za majanga UNDRR nchi zilizo na mifumo ya kutoa tahadhari za mapema kuhusu hatari mbalimbali zina viwango vya vifo vya maafa ambavyo ni mara sita chini ya nchi zisizo na mifumo au mifumo dhaifu. Zaidi ya hayo, utoaji wa onyo mapema kwa saa 24 tu una uwezo wa kupunguza uharibifu unaofuata kwa asilimia 30. Licha ya manufaa haya, ni asilimia 45 pekee ya nchi barani Afrika zimeripoti kuwepo kwa mifumo hiyo, kulingana na ripoti ya UNDRR ya mwaka 2023 kuhusu Hali ya Ulimwenguni ya Mifumo ya Mapema ya Utoaji Tahadhari za Hatari Mbalimbali.
    2 min
  • Watu milioni 8.1 duniani walikufa kutokana na uchafuzi wa hewa mwaka 2021
    Ripoti mpya ya kina inayoonesha athari hasi ya hewa chafuzi kwenye afya imetolewa leo nchini Marekani huku ikiweka bayana kuwa uchafuzi wa hewa umeibuka na kushika nafasi ya pili duniani kama kihatarishi kinachoweza kusababisha kifo, kuliko hata uvutaji tumbaku na ukosefu wa lishe bora. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Ikipatiwa jina Hali ya Hewa Duniani au SoGA ripoti imetolewa katika majimbo ya Massachussets na New York nchini Marekani na taasisi ya Health Effects au HEI kwa ushirikiano kwa mara ya kwanza na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.SoGA inasema mwaka 2021 watu zaidi ya milion 8 walikufa kwa sababu ya kuvuta hewa chafuzi kama vile itokayo kwenye moshi wa jiko ndani ya nyumba lisilotumia nishati safi kama vile kuni,  au uchimbaji wa mafuta kisukuku na vile vile hewa chafuzi kutoka kwenye magari.Hewa chafu imekuwa tishio zaidi kwa uhai wa mtoto kuliko hata tumbaku na lishe duni, kwani watoto zaidi ya 700,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano walikufa kwa kuvuta hewa chafu na wengi wao barani Afrika na Asia.Utafiti huo wa uwepo wa hewa chafuzi ulifanyika katika nyumba zaidi ya 200 duniani kote na kuchambua uwepo wa hewa chafuzi kama vile chembechembe ndogo au PM2.5 ambazo si rahisi kuzibaini kwa macho.Ripoti inabainisha kuwa chembe chembe hizo huweza kuingia moja kwa moja kwenye mfumo wa damu na kwenye mapafu na kusababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, moyo, kiharusi  na saratani.Asilimia 90 ya vifo vyote zaidi ya milioni 8 duniani vimesababisha na uvutaji wa aina hii ya chembe chembe za hewa.Akizungumzia ripoti hiyo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Kitty Van Der Heijden amesema ni vema serikali na sekta ya biashara wazingatie takwimu hizo na wazitumie vema ili kupunga uchafuzi wa hewa na kulinda watoto na dunia nzima.Licha ya takwimu zenye kiza, SoGa inasema kuna nuru ya matumaini kwani hatua zimeanza kuchukuliwa kuboresha hewa kupitia kupanua huduma za nishati safi na salama ya kupikia, kuboresha huduma za afya na lishe bora na kuongezeka kwa uelewa kuhusu uchafuzi wa hewa majumbani bila kusahau matumizi ya magari ya umeme.
    3 min
  • 19 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya kina ya athari ya hewa chafuzi, na uzinduzi wa kituo cha kutoa taarifa na maonyo ya mapema kuhusu dharura nchini Tanzania. Makala inafuatilia ziara za Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis nchini Sudan Kusini na mashinani inatupeleka nchini Kenya kumsikia mwanafunzi mwanaharakti wa mazingira.Ripoti mpya ya kina inayoonesha athari hasi ya hewa chafuzi kwenye afya imetolewa leo nchini Marekani huku ikiweka bayana kuwa uchafuzi wa hewa umeibuka na kushika nafasi ya pili duniani kama kihatarishi kinachoweza kusababisha kifo, kuliko hata uvutaji tumbaku na ukosefu wa lishe bora. Nchi ya Tanzania imepongezwa kwa kuzindua kituo cha kutoa taarifa na maonyo ya mapema kuhusu dharura hivyo kuwezesha wadau mbalimbali kuchukua hatua stahiki kabla ya majanga kutokea.Makala inatupeleka nchini Sudan Kusini ambako Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis mwishoni mwa wiki ametumia sehemu ya muda wa ziara yake nchini Sudan Kusini kuitembelea redio Miraya ambayo mwisho wa mwezi huu wa Juni inatimiza miaka 18 tangu kuanzishwa na ikisalia kuwa chombo muhimu kwa amani na ustawi wa watu wa Sudan Kusini. Anold Kayanda ameandaa makala hii kutokana na video iliyoratibiwa na UNMISS.Na mashinani tutaelekea katika kaunti ya Kitui nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu utunzaji wa mazingira.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    12 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners