Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 12 JUNI 2024
    Ripoti yaweka wazi Israeli na Hamas wanahusika na uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.Simulizi kutoka Sudan: Wapiganaji walitupokonya vitu vyetu.Nilikuwa mwathirika wa ajira ya watoto lakini sasa nafanya kazi ya kuizuia.Mashinani: Kutokana na kuzuka upya kwa mizozo katika jimbo la Equotoria Magharibi, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umeimarisha uwepo wa askari wake wa kulinda amani ili kuwalinda na kuwapatia msaada wa kibinadamu mamia ya watu katika kambi za wakimbizi wa ndani za eneo la Tambura.  
    10 min
  • MONUSCO yatoa mafunzo ya mbinu za kuondokana na habari potofu na za uongo DR Congo
    Umoja wa Mataifa kila uchao hivi sasa unapigia chepuo kampeni za kutokomeza habari potofu na za uongo kwani zimethibitika kuwa na madhara makubwa kwa jamii. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, habari hizo zimewahi kusababisha madhara ikiwemo vifo. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umeamua kuchukua hatua kwa kuendesha mfululizo wa mafunzo wa mbinu za kuondokana na habari hizo potofu na za uongo kama alivyotangaza Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita ambaye pia ndie mkuu wa MONUSCO. Alitangaza hayo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka jana wa 2023 na sasa hatua zimechukuliwa na matunda yanaanza kuonekana. Mwandishi wetu wa habari huko Beni, jimboni kivu kaskazini, mashariki mwa DRC, George Musubao amevinjari kufahamu madhara ya habari hizo na hatua zinazochukuliwa.
    6 min
  • 11 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika kampeni za kutokomeza habari potofu na za uongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambazo zimewahi kusababisha madhara ikiwemo vifo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, vifo vya wahamiaji na mkutano wa COSP17. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Huko Bahari ya Chumvi Jordan kwenye mkutano wa ngazi ya juu kwa ajili ya hatua za haraka za kibinadamu Gaza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ametoa wito wa msaada wa haraka wa kibinadamu kwa ajili ya Gaza akianinisha hali mbaya inayoendelea ikiwemo kutawanywa kwa watu milioni 1.7, kusambaratishwa kwa hospitali, ukosefu Mkubwa wa vifaa tiba muhimu, maji safi na chakula. Takriban wahamiaji 49 wamepoteza maisha na wengine 140 kutojulikana waliko baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama Pwani ya Yemen kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Boti hiyo iliyozama jana karibu na kituo cha Alghareef jimbo la Shabwah ilikuwa imebeba jumla ya wahamiaji 260 na miongoni wa waliopoteza maisha 31 ni wanawake na watoto.Na mkutano wa 17 wa mkataba wa watu wenye ulemavu COSP17 ambao maudhui yake makuu ni kutafakari ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika mazingira ya sasa, umefungua pazia leo hapa kwenye Mkao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani. Flora Nducha yuko ndani ya ukumbi wa Baraza Kuu kunakofanyika mkutano huo.Mashinani leo ikiwa ni siku ya michezo, tunakwenda Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania kupata maoni ya wazazi na watoto kuhusu umuhimu wa kucheza.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    12 min
  • WHO yatahadharisha kuhusu kushambuliwa kwa hospitali muhimu Al Faher Sudan
    Shambulio kubwa lililofanywa na wanamgambo wa Rapid Support Forces, au RSF mwishoni mwa wiki katika mji wa Al Fasher kaskazini mwa Sudan limelazimisha kufungwa kwa hospitali kuu inayotegewa katika eneo hilo na hivyo kusababisha kupungua upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha, limeripoti leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO. Kwa mujibu wa taarifa za WHO, Wizara ya Afya ya Sudan na shirika lisilo la kiserikali la Madaktari wasio na mipaka Médecins Sans Frontières (MSF) walilazimika kuifunga hospitali hiyo kubwa pekee inayotoa huduma za upasuaji katika El Fasher nzima baada ya wanamgambo hao wa Rapid Support Forces (RSF) kuingia ndani ya hospitali na kufyatua risasi kisha wakaiba vifaa tiba na gari la wagonjwa.  WHO Sudan imeeleza kusikitishwa na shambulio hilo na wamesema, "Kufungwa kwa hospitali hiyo kufuatia shambulio hilo kumeziongezea hospitali nyingine mbili mzigo zaidi ya uwezo wake.”Pia WHO imelaani "shambulio lingine" kwenye kituo cha afya huko Wad Al-Nura katika jimbo la Al-Jazirah kusini mwa Khartoum, ambalo lilisababisha kifo cha muuguzi ambaye alikuwa zamu akihudumia wagonjwa wakati huo.“WHO inalaani vikali mashambulizi dhidi ya huduma za afya.” WHO Sudan imeeleza kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X. “Wahudumu wa afya na wagonjwa hawapaswi kuhatarisha maisha yao ili kutoa na kupata huduma za afya.” Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesisitiza ikiwa ni siku chache pia baada ya shambulio katika moja ya vijiji nalo likiripotiwa kutekelezwa na wanamgambo wa RSF wakitumia  mizinga mikubwa kushambulia kijiji na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100.
    2 min
  • Hatutaki kuona umwagaji damu upande wowote – Mkazi Gaza
    Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Mamlaka ya Palestina, mashambulio yaliyofanywa na Israeli tarehe 8 mwezi Juni kwenye eneo la kati la Deir El Balah huko Ukanda wa Gaza yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 270 na wengine zaidi ya 700 walijeruhiwa wengine wako mahututi. Shule ilishambuliwa kwenye eneo hilo hilo siku mbili kabla ya shambulio hilo la tarehe 8 na kusababisha vifo vya watu 40, wakiwemo watoto 14 na wanawake 9. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ilifika Deir El Balah na kuzungumza na mmoja wa wakazi anayesimulia kilichotokea na wito wake, na hicho ndio msingi wa makala hii inayosimuliwa na Assumpta Massoi.
    4 min
  • 10 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya nchini Sudan huku mgogoro ukiendelea, na ndoa za utotoni nchini Uganda. Makala inatupeleka katika eneo la Deir El – Balah Gaza kusikia simulizi za waathirika wa vita, na mashinani tunakwenda Geneva, Uswisi kumsikia Deogratius Ndejembi kwe nye mkutano wa ILO.Shambulio kubwa lililofanywa na wanamgambo wa Rapid Support Forces, au RSF mwishoni mwa wiki katika mji wa Al Fasher kaskazini mwa Sudan limelazimisha kufungwa kwa hospitali kuu inayotegewa katika eneo hilo na hivyo kusababisha kupungua upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha, limeripoti leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO. Mradi wa Wasichana kuwawezesha wasichana wenzao GEG, ni mradi wa kwanza nchini Uganda wa ulinzi wa kijamii unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa ushirikiano wa mamlaka ya mji mkuu wa Kampala kupitia ufadhili uliotolewa na serikali ya Ubelgiji ukiwalenga watoto wa kike na mustakbali wao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA anatupeleka Gaza hususan eneo la Deir El – Balah ambako mashambulizi ya Israeli wiki iliyopita yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 300 na wengine wapatao 700 walijeruhiwa wakiwemo watoto.Mashinani tunakwenda Geneva, Uswisi kumsikia Deogratius Ndejembi, Wazir wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu akizungumzia ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano wa 12 wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    12 min
  • Zainab: Mradi wa UNICEF wa GEG umeokoa mustakbali wangu
    Mradi wa Wasichana kuwawezesha wasichana wenzao GEG, ni mradi wa kwanza nchini Uganda wa ulinzi wa kijamii unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa ushirikiano wa mamlaka ya mji mkuu wa Kampala kupitia ufadhili uliotolewa na serikali ya Ubelgiji ukiwalenga watoto wa kike na mustakbali wao. Mradi huo wa GEG unatekelezwa katika wilaya zote tano za Kampala na unahakikisha wasicha barubaru walio shuleni na nje ya shule wanakuwa na mabadiliko bora kutoka utotoni kuingia ukubwani kwa kupokea elimu, ushauri na mafunzo ambayo yanawajengea uwezo wa kufikia malengo yao. Wengi walio katika mradi huu wamepitia changamoto lukuki na mfano halisi ni Zainab mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa shule ya msingi Kampala“Siku moja nyanya yangu alipokea simu kutoka kijijini wakimwambia nahitajika kijijini. Na nilipowasili huko nilikuwa viroba vya sukari, mchele na kadhalika na nikamuuliza msichana niliyemkuta pale hivi vitu ni vya nani?  Kisha akaniambia haujui kwamba unaolewa? Nilikuwa na umri wa miaka 16 tu na walikuwa wananiambia mi ni mkubwa”Familia ya Zainab ilipanga na kumuandalia ndoa bila ridhaa yake na baada ya kupokea mahari alilazimishwa kwenda kuishi na bwana na mambo yalikuwa mabaya anasema ZainabMwanaume huyo alitaka kulala nami kwa nguvu, alitaka kunibaka. Nilimwambia hapana nataka kurejea shuleni. Nilikuwa nalia kila siku , sikujua cha kufanya nilichanganyikiwa. Na hapo nikamkumbuka mshauri wangu aliniambia wakati wowote ukipata tatizo nipigie nitakusaidia. Basi nikampigia naye akampigia baba yangu sijui walichozungumza lakini baada ya siku moja, nilirejea Kampala nikarejea shuleni.”Mshauri huyo ni kutoka mradi wa UNICEF wa GEG aliokoa Maisha ya Zainab ambaye baada ya kunusika ndoa ya utotoni na kubakwa ana matumaini ya muskabali wake“Sasa niña furaha sana kwani nimekuwa shuleni na bado naendelea na shule. Nimemaliza darasa la saba, naenda sekondari na nitafaulu. Nataka kuwa mwanasheria niweze kupigania haki za watoto ili kusiwe na mtoto yoyote atakayelazimishwa kufanya asichotaka.”Mradi wa GEG umegawanyika katika sehemu kuu tatu, mosi kuwawezesha wasichana kupitia mtandao wa washauri rika, pili kuwashirikisha wasichana kupitia elimu, mafunzo na kuwaelekeza kwa kupata msaada wa huduma na tatu kuwawezesha wasichana kutafuta fursa bora za maisha yao ya baadaye kupitia msaada mdogo wa fecha wanaopokea.
    3 min
  • Mfumo wa kutoa tahadhari mapema warejesha imani kwa wakazi wa Ituri, DRC
    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umeanzisha mfumo wa kutoa tahadhari mapema kuhusu mashambulizi dhidi ya raia yanayoendeshwa na waasi kwenye mji wa Bunia jimboni Ituri. Mfumo huu unaweza jamii, jeshi la serikali na MONUSCO kubadilishana taarifa na hivyo wananchi wanakuwa na hakikisho la usalama wao kwani pindi taarifa inapotolewa, hatua sahihi zinachukuliwa kama anavyosimulia Assumpta Masso kwenye makala hii iliyofanikishwa na MONUSCO.
    4 min
  • WHO: Takribani watu milioni 1.6 huugua kila siku kutokana na chakula kisicho salama
    Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. Hii leo kupitia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi uliowahusisha Dkt. Francesco Branca, Mkurugenzi wa Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula wa WHO na Markus Lipp, Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Chakula wa FAO imeelezwa kuwa madhara yatokanayo na chakula kisicho salama hayaangalii mipaka na yametapakaa katika nchi nyingi duniani.  Dkt. Francesco Branca aliyekuwa katika ukumbi huo wa mikutano ametoa taarifa kwamba "kutokana na kuugua kwa takribani watu milioni 1.6 kila siku kunakosababishwa na vyakula visivyo salama, watu 420,000 hufariki dunia kutokana na sababu hiyo."Mwaka huu, kaulimbiu ya kampeni ya Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, ni Jiandae kwa Yasiyotarajiwa, ambayo sio tu inasisitiza umuhimu wa kuwa tayari kudhibiti matukio ya usalama wa chakula ili yasiwe ya dharura, lakini pia umuhimu wa kuchukua muda kupanga, kuandaa na kuwa tayari kuchukua hatua katika mazingira ya dharura.Kwa upande wake Markus Lipp, Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Chakula katika Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), kwa njia ya video akizungumza kutoka Roma, Italia ameeleza namna FAO inavyohusisha chakula salama na utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu…anasema, “Chakula kinapozalishwa na kuuzwa katika mfumo wa kilimo salama na endelevu, kinachangia maisha yenye afya na kuboresha uendelevu kwa kuwezesha upatikanaji wa soko na tija, ambavyo vinasukuma maendeleo ya kiuchumi na kupunguza umaskini, hasa katika maeneo ya vijijini.”
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners