Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNRWA: Gaza hali si hali tena huku watu milioni 1 wakikimbia Rafah
    Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. Katika tarifa yake iliyotolewa leo kupitia mtandao wa kijamii wa X UNRWA imesema mji wa Rafah kwenye mpaka wa kusini wa Gaza na Misri ulikuwa nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao kwa karibu miezi minane ya mashambulizi ya kila siku ya jeshi la Israel, kujibu shambulio la kigaidi lililoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana."Maelfu ya familia sasa wanaishi katika vituo vilivyoharibiwa na kusambaratishwa huko Khan Younis ambapo UNRWA inaendelea kutoa huduma muhimu, licha ya changamoto zinazoongezeka. Masharti hayaelezeki,” Haya yanajiri siku tatu tangu Rais wa Marekani Joe Biden kuzindua pendekezo la usitishaji mapigano kwa kuzingatia usitishaji wa hatua kwa hatua kwa vita hiyo, pendekezo likiripotiwa kujumuisha kuondolewa kwa majeshi ya Israel kutoka maeneo wyalikorundikana, kuachiliwa kwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina, pamoja na mpango wa ujenzi mpya wa Gaza.Kulingana na UNRWA, maelfu ya familia zimelazimika kutafuta makazi katika majengo yaliyoharibiwa vibaya huko Khan Younis jiji ambalo liko kaskazini mwa Rafah, na linakadiriwa kuwa na watu wapatao milioni 1.7. Imeripotiwa kwamba makao yote 36 ya UNRWA huko Rafah sasa yamesalia matupu.Shirika hilo limeongeza kuwa Takriban wanawake na wasichana 690,000 wanaaminika kukosa vifaa vya msingi vya usafi wakati wa hedhi, faragha na maji ya kunywa.Ikiangazia mapambano ya kila siku yanayowakabili watu walio hatarini sana huko Gaza, UNRWA imelinukuu Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya uzazi UNFPA ambalo linakadiria kwamba karibu wanawake 18,500 wajawazito wamelazimika kukimbia Rafah. "Takriban 10,000 zaidi wamesalia huko katika hali mbaya na upatikanaji wa huduma za afya na vifaa vya uzazi ni mdogo. Afya ya mama na mtoto iko hatarini.”Likirejea wasiwasi huo mkubwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP  kupitia Matthew Hollingworth, Mkurugenzi wa WFP katika eneo linalokaliwa la Palestina lisema sasa hakuna "kikubwa tunachoweza kuwafanyia watu ambao bado wako Rafah, ambako barabara si salama, hazifikiki vizuri, na washirika wetu wengi na mashirika mengine ya kibinadamu yametawanywa”.Ameonya kwamba hofu ya afya ya umma sasa imevuka viwango vya janga, wakati sauti, harufu, na maisha ya kila siku, ni ya kutisha na ya kuzimu. Watu "wamekimbilia maeneo ambayo maji safi, vifaa vya matibabu na usaidizi havitoshi, usambazaji wa chakula ni mdogo, na mawasiliano ya simu yamesitishwa."
    2 min
  • 03 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na afya ya uzazi nchini Randa. Mashinani tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto.Katika makala Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wa baiskeli tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama nafuu, hakichafui mazingira na zaidi ya yote afya kwa watumiaji kwani ni mazoezi.Na mashinani tutaelekea Mwanza nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu mikakati ya kudhibiti uhalifu katika mipaka Afrika mashariki.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • UNICEF yafanikisha mradi wa Lishe Bora kwa Wanawake Wajawazito nchini Rwanda
    Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto. Nshimiyimana Clementine, ni Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kabaya, Wilayani Ngororero katika Jimbo la Magharibi nchini Rwanda anasema, “Wajawazito wanapata taarifa kutoka kwa Wahudumu Afya Jamii ambao wanawaelekeza kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya vipimo muhimu na kupata vidonge vya lishe.”“Tunawashauri kumeza kidonge kimoja kila siku angalau kwa miezi sita. Na sasa kwa kuwa tumeanza kusambaza vidonge lishe hivi tunaamini vitakuwa na manufaa kwa kuzingatia lishe zilizomo. Wajawazito hawatakosa virutubisho kutoka kwenye matunda na mbogamboga kwa kuwa hivi vidonge vinavyo. Japo bado tunawahimiza wajawazito kula matunda na mbogamboga, lakini wale wasiomudu hawataathirika na upungufu wa virutubisho. ”Umugwaneza Yvette ni mmoja wa wajawazito wanufaika wa programu hii iliyowezeshwa kwa ukarimu wa KIRK Humanitarian shirika lisilo la kiserikali linalojitolea kuhakikisha Virutubisho lishe kupitia Umoja wa Mataifa vinawafikia wajawazito kokote waliko duniani.“Wakati usambazaji wa vidonge vya MMS ulipoanza, nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kupokea. Mwili wangu umevipokea vizuri. Sijapata changamoto yoyote. Ninameza mara kwa mara na ninajisikia mwenye afya.”
    2 min
  • Akili Mnemba inarahisisha mambo lakini inahitaji usimamizi - Profesa Pillay
    Kila uchao, mikutano ifanyika kona mbali mbali za dunia kubonga bongo ni kwa vipi akili mnemba inaweza kutumika kwa manufaa ya binadamu na si vinginevyo kwani Umoja wa Mataifa unataka nyenzo hiyo iwe ya manufaa hasa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Huko Geneva, Uswisi kumetamatika mkutano wa kujadili ni kwa vipi akili mnemba italeta manufaa. Suala hilo hilo pia lilikuwa miongoni mwa mijadala ya jukwaa la 4 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali huko Manama, Bahrain ambapo mmoja wa wanajopo alikuwa Profesa Dokta Selvaraj Oyyan Pillay kutoka Malaysia ambaye katika makala hii Assumpta Massoi alizungumza naye na kuumuliza iwapo ana shaka na shuku kuhusu mustakabali wa akili mnemba na nini kifanyika.
    4 min
  • UNICEF inawasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia kujifunza kidijitali nchini Kenya
    Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo hayo ni Terika Gevera, Mwalimu katika Shule ya Viziwi ya Maseno katika Kaunti ya Kisumu."Wanafunzi wetu mara nyingi hupata ujifunzaji wao kupitia hisia ya kuona, kwa sababu usikivu wao hauwafai sana. Kwa hivyo, UNICEF kuunganisha shule kwenye intaneti kumesaidia sana hasa katika kuboresha ufundishaji wetu. Watoto wetu wanaweza kujifunza na hasa kujifunza kupitia njia ya kuona wanaweza kupata maarifa kwa njia bora zaidi.”Mwalimu Terika Gevera anafafanua zaidi akisema,"Intaneti ni sehemu muhimu sana katika kujifunza. Tuliamunganishwa katika nyenzo za E-Kitabu. E-Kitabu wamejaribu kuandika hadithi zao kwa lugha ya ishara, hivyo wanafunzi hutazama picha, huangalia ishara na mwisho wa kila hadithi, wanafunzi huulizwa maswali kuhusu hadithi ambayo imesimuliwa kwa ishara. Kupitia hilo wanafunzi wamefahamu kuwa wanaweza kusoma hadithi, kuelewa na kujibu maswali.”
    2 min
  • 31 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Burkina Fasso na mradi unofahamika kama GIGA unaosaidia kufanikisha masomo ya kidijitali kwa wanafunzi nchini Kenya. Makala inamulika usimamizi wa Akili Mnemba na mashinani inatupeleka Garissa nchini Kenya, kulikoni?Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai ya kuwajibika na mauaji hayo kutoka pande zote, makundi yenye silaha na serikali. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Makala inaturejesha Bahrain kufuatilia usimamizi wa Akili Mnemba wakati huu ambapo huko Geneva, wabobezi wa Akili Mnemba na wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi wakibonga bongo kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia hiyo, Assumpta Massoi amezungumza na mwanazuoni kutoka Malaysia kandoni mwa jukwaa la Umoja wa Mataifa la Uwekezaji kwa wajasiriamali lililomalizika hivi karibuni huko Manama.Na katika mashinani tutasalia nchini Kenya kaunti ya Garissa ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM linaendelea kutoa msaada kwa maelfu ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na mafuriko yanayoendelea.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Volker Türk: Mauaji ya raia Burkina Faso yamefurutu ada lazima yakome
    Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai pande zote, makundi yenye silaha na serikali kuhusika na mauaji hayo. Kwa mujibu wa tarifa ya ofisi ya Kamishina Mkuu wa haki za binadamu OHCHR kati ya Novemba 2023 na Aprili mwaka huu 2024 imepokea madai ya ukiukwaji wa haki na ukatili unaokiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu ukiwaathiri takriban watu 2732 hili likiwa ni ongezeko la asilimia 71 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu ukilinganisha na miezi sita iliyopita.Taarifa inasema watu 1794 ay asilimia 65 miongoni mwa watu hao ni waathirika wa mauaji ya kinyume cha sheria.Ofisi hiyo ya haki za binadamu imesema Makundi yenye silaha, kama vile Jamāʿat nuṣrat al-islām wal-muslimīn, Kundi kubwa la Kiislamu katika Jangwa la Sahara na makundi mengine yanayofanana na hayo, yamezidisha mashambulizi yao dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na dhidi ya wakimbizi wa ndani. Kwa mujibu wa Bwana Türk "Wakati makundi yenye silaha yanadaiwa kuhusika na idadi kubwa ya matukio na waathirika, na yanapaswa kuwajibika, pia ninasikitishwa sana kwamba vikosi vya usalama na ulinzi na wasaidizi wao ambao ni watu waliojitolea kwa ulinzi wan chi yao wanadaiwa kutekeleza mauaji ya kiholela, ikiwa ni pamoja na kunyongwa,”Awali mkuu huyo wa haki za binadamu alizungumzia masuala haya na Kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso, wakati wa ziara yake nchini humo Machi mwaka huu.Türk ameongeza kuwa "Ninatambua kikamilifu vitisho tata vya usalama ambavyo Burkina Faso inakabiliana nayo. Jawabu dhidi ya vitisho hivi litafaulu tu ikiwa sheria za kimataifa zitaheshimiwa kikamilifu kote nchini. Kwa hivyo narudia wito wangu kwa mamlaka nchini Burkina Faso kuchukua hatua zote zinazowezekana ili kuhakikisha ulinzi wa raia,” Kamishna Mkuu ametoa wito kwa Serikali ya Burkina Faso kuunga mkono uchunguzi wa kina, huru na wa uwazi kuhusu tuhuma zote za ukiukaji wa haki na ukiukwaji wa sheria za kimataifa, na kuhakikisha kuwa wahalifu wanafikishwa mahakamani, katika kesi zinazokidhi viwango vya kimataifa, ili kuhakikisha haki ya kweli kwa waathirika na fidia.Amesisitiza kwamba ni “Lazima kuweka na haki na uwajibikaji endapo mamlaka inataka kweli kuihakikishia jamii inarejesha mshikamano wa kijamii na kujenga upya uaminifu kati ya raia na vikosi vya usalama." 
    2 min
  • 30 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ni kwa vipi wabunifu wanaweza kumiliki kazi zao na zikasongesha SDGs ikiwemo kutokomeza umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Sudan, Gaza na jukwaa la Kimataifa la “AI for Good”, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kwamba dalili zote zinaonesha kuzorota kwa kiasi kikubwa kwa hali ya lishe kwa watoto na wanawake katika nchi ya Sudan inayokumbwa na vita. Uchambuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Mashirika hayo matatu la Kuhudumia Watoto (UNICEF), la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la afya ulimwenguni (WHO) unaonesha kwamba uhasama unaoendelea unazidisha visababishi vya utapiamlo kwa watoto. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutoa wito wa usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza kwasababu hali inazidi kuwa tete kila uchao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema hakuna mengi ambayo linaweza kufanya kwa sasa huko Rafah kwani akiba ya chakula ni ndogo na kuna vikwazo vingi kuwafikia watu.Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa wa Akili Mnemba umeanza leo Mei 30 mjini Geneva, Uswisi kujadili matumizi bora ya Akili Mnemba (AI) ili kuharakisha kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na unaunganisha wabunifu wa Akili Mnemba na watoa uamuzi wa sekta ya umma na binafsi ili kusaidia kuongeza ufumbuzi unaotokana na akili Mnemba kote duniani.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    11 min
  • Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan
    Makala hii inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Sara alikuwa na ujauzito wa miezi 9 wakati bomu lilipopiga nyumba yake na kumlazimu kukimbia na hatimaye kujifungua mtoto wake peke yake bila uangalizi wowote wa kitabibu. Familia nyingi nchini Sudan zimesambaratishwa na mzozo unaoendelea. Selina Jerobon ndiye msimulizi wetu..
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners