Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 23 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada ka kina inayotupeleka huko wilaya ya Abyei iliyoko kati ya mpaka wa Sudan Kusini na Sudan lilifanyika shambulizi la kuvizia wakati gari la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likisafirisha raia waliojeruhiwa, ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”  Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambalo ni tundu kati ya njia ya uzazi na kibofu cha mkojo, inayosababishwa mara nyingi na uchungu wa muda mrefu wakati wa kuelekea kujifungua, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na masuala ya kijinsia UNFPA Natalia Kanem amesema Fistula ya uzazi ni matokeo ya kusikitisha ya kushindwa kulinda haki za uzazi za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu zaidi na ni lazima itokomezwe kwa watu wote. Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Palestina Matthew Hollingworth ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba maelfu ya familia zinazokimbia Rafah zinajikuta zikiwa na uhaba wa chakula na maji safi.Mvua nyingi zaidi kuliko kawaida inatabiriwa katika maeneo mengi ya Pembe ya Afrika kuanzia mwezi Juni hadi Septemba mwaka huu. Maeneo yatakayotarajiwa kuwa na hali hiyo ni Djibouti, Eritrea, kaskazini na katikati mwa Ethiopia, magharibi na pwani ya Kenya, sehemu kubwa ya Uganda, Sudan Kusini, na Sudan.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Kanga hazai ugenini.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    11 min
  • Waathirika Garisa Kenya washukuru UNICEF kwa msaada wa fedha baada ya mafuriko
    Kenya inashuhudia kiwango kikubwa cha mvua zaidi ya kile cha kawaida ambacho kimesababisha mafuriko makubwa,maporomoko ya udongo na maelfu ya watu kutawanywa hivi karibuni. Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaunti ya Garisa , ambako hivi sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake kama shirika la Norway kwa ajili ya ushirikiano wa maendeleo NORAD, Mamlaka ya Kitaifa ya kudhibiti Ukame Kenya NDMA, na serikali ya Kaunti ya Garasa  kwani kaya zilizoathirika na mafuriko zinapokea msaada wa fedha taslim kupitia M-pesa na vocha za kielektroniki ili kujikimu kimaisha. Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii
    4 min
  • UNICEF: Vurugu zinatikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka
    Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini Port-Au-Prince imeeleza kwamba vurugu zimeutikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka kutokana na kwamba makundi yenye silaha yamenyonga minyororo ya usambazaji, na kuweka mamilioni ya watoto katika hatari ya magonjwa na utapiamlo.Kila hospitali nchini Haiti imeripoti ugumu wa kupata na kutunza vifaa muhimu vya matibabu, kwani safari za ndege za kimataifa na za ndani za mizigo kutoka na kwenda katika viwanja vya ndege vya Port-Au-Prince zilirejea kufanya kazi hivi majuzi tu, zikiwa na uwezo mdogo na mrundikano mkubwa, kama ilivyokuwa kwa bandari kuu ambayo hapo awali ilikuwa mikononi mwa makundi yenye silaha."Mfumo wa afya wa Haiti uko karibu kuporomoka," Bruno Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti amesema akiongeza kwamba, "Mchanganyiko wa vurugu, ufurushaji wa watu wengi, milipuko hatari, na kuongezeka kwa utapiamlo kumeupinda mfumo wa afya wa Haiti, lakini kunyongwa kwa minyororo ya usambazaji kunaweza kuwa ndio kunauvunja."Makontena yaliyojazwa vifaa muhimu yamezuiliwa, au kuporwa, kama ilivyokuwa kwa maghala na maduka mengi ya dawa. Wakati huo huo, mamia ya makontena yaliyosheheni vifaa vya kibinadamu yamekwama huko Port-Au-Prince ikiwa ni pamoja na kontena za UNICEF zilizo na vifaa vya watoto wachanga, wajawazito na vya matibabu.Port-Au-Prince, kitovu kikuu cha Haiti, kwa kawaida hupokea na kutuma mizigo ya uagizaji wa vifaa tiba vya Haiti. Sasa jiji hilo limelemazwa na vurugu, na wakazi wake zaidi ya 160,000 wameyakimbia makazi yao, jiji hilo haliwezi kutosheleza mahitaji ya watu ambao kwa wakati mmoja wanapambana na majeraha ya kimwili na hatari ya magonjwa, inafafanua taarifa ya UNICEF.Mawimbi ya familia zilizofurushwa zinazotafuta usalama, hasa katika sehemu ya kusini mwa nchi, yanaleta shinikizo la ziada kwa huduma za afya za wanakokimbilia, ambazo hata kabla ya kuongezeka kwa mzozo hazikuweza kuhimili mahitaji. Uhaba wa wafanyakazi umeenea, na takriban asilimia 40 ya wafanyakazi wote wa matibabu wameondoka nchini Haiti kutokana na viwango vya juu vya ukosefu wa usalama.Kati ya Oktoba 2022 na Aprili 2024, Haiti iliripoti jumla ya visa 82,000 vinavyoshukiwa kuwa na kipindupindu. Takriban watu milioni 4.4 nchini Haiti wanahitaji msaada wa haraka wa chakula, na watu milioni 1.6 wanakabiliwa na viwango vya dharura vya uhaba wa chakula, jambo ambalo linaongeza hatari ya kupata tatizo la uzito mdogo kwa watoto na utapiamlo. Kuwasili kwa msimu wa mvua kunatazamiwa kuzidisha hali kuwa mbaya zaidi, hivyo kusababisha ongezeko la visa vya magonjwa yatokanayo na maji pamoja na magonjwa yanayoenezwa na mbu, kama vile malaria.Ili kukabiliana na hali hiyo, UNICEF na wadau wanatafuta njia mbadala za kuagiza na kusambaza mizigo. Kupitia njia za pili za uingizaji na utoaji, pamoja na Wizara ya Afya, wafadhili wa kimataifa na washirika, UNICEF imeweza kuendelea kupeleka chanjo, dawa na vifaa vya matibabu kwa watoto nchini Haiti ambao wanahitaji zaidi.Tarehe 18, 20 na 21 Mei 2024, UNICEF iliwezesha kuwasilisha tani 38 za vifaa vya kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na vifaa vya afya na kipindupindu, na bidhaa nyingine muhimu za matibabu nchini Haiti kupitia njia ya anga kwa kuungwa mkono na Muungano wa Ulaya na WFP kutoka Panama hadi mji mkuu wa Haiti, ambapo UNICEF na Umoja wa Mataifa wameanzisha kituo kipya cha kufanya kazi. Lakini msaada zaidi unahitajika."Hatuwezi kuruhusu vifaa muhimu ambavyo vinaweza kuokoa maisha ya watoto kubaki vikiwa vimezuiliwa kwenye maghala na makontena. Lazima viwasilishwe sasa,” amesisitiza Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti.
    2 min
  • 22 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya kwa watoto nchini Haiti na simulizi afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO kuhusu yanayoenndelea Gaza. Makala tnakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”Makala inatupeleka Kaunti ya Garisa nchini Kenya ambako waathirika wa mafuriko na maporomoko ya udongo ya hivi karibuni walio katika makambi za muda za wakimbizi wa ndani wanapokea msaada wa fecha na vocha kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake ikiwaweze kujikimu.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    11 min
  • Niliyoshuhudia Gaza yanatisha na kusikitisha - Nika Alexander
    Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”Ni Nika Alexander kiongozi wa timu ya mawasiliano ya dharura kutoka WHO akieleza tofauti ya kwanza anayoona sasa akiwa amerejea kutoka Gaza ambapo wakati angali kule siku baada ya siku wakisikia mlio wa ndege basi bomu linaweza kuanguka dakika yoyote, wakati sasa ukiwa sehemu ambayo si ya vita akisikia mlio wa ndege pengine ni watu wanaendea likizo ni kama watu wa Gaza wanaishi kinyume na ulimwengu. Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kurejea Gaza Bi.Nika anasimulia hali ya kule. “Nilichoondoka nacho ni mawazo ya jinsi hali ilivyo mbaya kwa watu wa Gaza, jinsi hali ilivyo ngumu kwa watu wanaojaribu kuwasaidia watu wa Gaza na jinsi kulivyo hatari.” Amesema hospitali zinazofanya kazi ni chache na hazifanyi kazi kamili.“Kimsingi, kote Gaza, ni theluthi moja ya hospitali ndio zinafanya kazi. Kwa hivyo takriban hospitali 12 kati ya 36 bado zinaweza kufanya kazi kwa namna fulani. Hawawezi kutoa huduma kamili. Baadhi yao wanafanya kama sehemu ya kutoa huduma ya kwanza na kusaidia wenye kiwewe, ambapo wanajaribu tu kutibu wake wanakuwa wanavuja damu na vyovyote vile wawezavyo ilimradi watu wasife kutokana na majeraha.”Afisa huyu wa mawasiliano ya dharura anasema pamoja na yote hayo lakini lipo lililompa matumaini licha ya kutokuwepo kwa eneo lolote salama katika Ukanda wa Gaza. “Kilichonivutia sana ni kwa jinsi kila mtu anavyofanya kazi kwa bidii licha ya hali mbaya ambapo kila kelele inaweza kuwa ni mlipuko karibu yako, au unaweza kuwa unakulipukia wewe. Nilipoondoka Rafah wiki moja iliyopita, tulikuwa wafanyakazi 19 wanaondoka na wengine 20 wa Umoja wa Mataifa wanaingia Rafah. Ninawaona wenzangu hao kuwa wajasiri sana, na sio kwamba wanakuja kujifanyia kazi wenyewe bali wanakuja kushirikiana na wafanyakazi wa Gaza wa sekta ya afya.” 
    3 min
  • 21 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa mradi wa Cookfund, Elisabeth Ngoye amezungumza na Laurien Kiiza wa UNIC Dar es Salaam. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za afya, Gaza na Ukraine. Mashinani inatupeleka nchini Kenya, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo Mei 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO inaashiria ongezeko kubwa la magonjwa ya zinaa duniani, huku kukiwa bado na changamoto za Virusi Vya Ukimwi na homa ya ini. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X ameeleza wasiwasi mkubwa walio nao juu ya usalama wa wagonjwa na wafanyakazi waliokwama katika hospitali ya Al-Awda kaskazini mwa Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Ukraine, limeeleza kuhusu wasiwasi mkubwa kutokana na hali inayozidi kuwa mbaya na kusababisha ongezeko la mahitaji ya kibinadamu kwa Waukraine na kulazimishwa kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi mapya ya ardhini ya Jeshi la Urusi katika eneo la kaskazini-mashariki la Kharkiv.Na katika mashinani leo tunakupeleka katika eneo Bunge la Ngong lililoko katika kaunti ya Kajiado  nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa utunzaji wa chemichemi ya maji.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    11 min
  • Ninajisikia fahari sana kutatua changamoto za wanawake na watoto wa CAR - Meja Lilian Laizer
    Makala hii inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na watoto katika kikosi na jamii ya wenyeji. Msimulizi ni Anold Kayanda
    4 min
  • Baadhi ya wapalestina warejea kwenye nyumba zao zilizoathiriwa na mabomu baada ya kulazimishwa kuondoka Rafah
    Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama hama inaweza kusababisha janga la kibinadamu, nakupelekea kusimama kwa shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu.Baada ya kufika nyumbani kwake, Ibrahim Kamal Ibrahim Amtair anamuonesha mtoto wake mdogo wa kike box lililojaa bidhaa mbalimbali za msaada aliopokea kutoka WFP. Ibrahim ni mmoja wa watu waliokimbia makazi yao Khan Younis na kukimbilia Rafah baada ya amri ya Jeshi la Israel lakini baada ya Israel wiki iliyopita kutoa tena amri ya kuwataka kuondoka Rafah ameona hana tena pa kukimbilia na kuamua kurejea katika nyumba yake. Amekuta nyumba yake imeathirika vibaya na mabomu pamoja na risasi, baadhi ya maeneo hakuna madirisha wala milango huku kukiwa na matundu ambayo ameyafunika kwa mabox na anasema mpango wake ni kukarabati matundu hayo ili watoto wake wasijeumia. “Hawakusema kuwa eneo hili liko salama, lakini tumerudi kwa sababu hatuna mahali pa kwenda, na hatukuwa sawa katika maeneo tuliyokuwepo. Hakuna anayejisikia raha isipokuwa akiwa nyumbani kwake, hata kama nyumba ikiwa imeharibiwa.”Mbali na chakula cha msaada pamoja na vifurushi vya msaada wanavyo patiwa wananchi wa Palestina ambavyo vina vyakula kama vile makopo ya maharage, mbaazi na nyama ya kopo, Mkurugenzi wa WFP huko Palestina, Matthew Hollingworth anasema hifadhi iliyopo sasa ya chakula na mafuta itaisha baada ya siku chache.“Hatujaweza kufikia ghala letu huko Rafah kwa zaidi ya wiki moja sasa. Tuna chakula kidogo na mafuta yanayokuja kupitia vivuko vya mpaka kusini na tunajitahidi kila wakati lakini tunashindwa kwa sasa kuleta kiasi cha kutosha cha chakula. Tunajua, tunahitaji njia za ziada za kuingilia na kila njia ya kuingilia ni mshipa wa kusukuma damu kuingia Gaza. Kwahiyo, tutafanya kazi kwa bidii ili kuendelea kupata njia mpya za kuingia na kupata usaidizi zaidi, kwa wingi na mara kwa mara ili kusaidia kukomesha njaa ambayo inajongea.”Pamoja na changamoto nyingi, WFP inaendelea kusalia Gaza na kushirikiana na wadau wengine katika kutoa msaada kwa wapalestina.
    3 min
  • 20 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya sheria na uhalifu na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini CAR kufatilia kazi za walinda amani na mashinani tunakuletea ukumbe kuhusu ufugaji nyuki na thamana yao. Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza. Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama hama inaweza kusababisha janga la kibinadamu, nakupelekea kusimama kwa shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu.Makala inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na watoto.Na katika mashinani leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Nyuki tutasikia uhusiano kati ya nyuki na  jamii za watu wa asili.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    12 min
  • ICC yawasilisha ombi kwa Baraza la Usalama la hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Netanyahu wa Israel
    Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza. Ni Karim Khan, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mapema leo alipotangaza kwamba anawasilisha maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na wa Israel kwa majaji wa mahakama hiyo ambao ndio watakaotoa uamuzi wa kutolewa kibali cha kukamatwa.Bwana Khan amesema kuna sababu za msingi za kuamini kwamba Yahya Sinwar wa Hamas, Mohammed Diab Ibrahim Al-Masri (Deif) na Ismail Haniyeh "wanawajibikia kijinai" kwa mauaji, kuangamiza na kuchukua watu mateka miongoni mwa uhalifu mwingine mwingi tangu mzozo wa Gaza ulipozuka kufuatia mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana 2023.“Pia kuna misingi ya kuridhisha ya kuamini kwamba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Yoav Gallant, Waziri wa Ulinzi wa Israel, wanahusika na uhalifu mwingine na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa katika eneo la Palestina” Amesema Mwendesha Mashitaka wa ICC.Ametaja miongoni mwa vitendo vya uhalifu wa kivita vilivyotekelezwa kuwa ni pamoja na kutumia njaa dhidi ya raia kama mbinu ya vita na pia kuelekeza kwa makusudi mashambulizi dhidi ya raia.Ingawa ICC si shirika la Umoja wa Mataifa, ina makubaliano ya ushirikiano na Umoja wa Mataifa. Na kunapotokea suala ambalo haliko ndani ya mamlaka ya Mahakama, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza kulipeleka suala hilo kwa ICC, na kuipa mamlaka ya kulishughulikia.Tutaendelea kukupa taarifa kwa kina kuhusu hatua hii ya ICC ingawa pia kwa sasa unaweza kujisomea zaidi katika wavuti wetu news.un.org/sw
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners