Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Orodha mpya ya bakteria sugu dhidi ya dawa yatolewa na WHO
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Katika taarifa iliyotolewa leo, WHO inafafanua kuwa usugu wa vijiumbemaradhi dhidi ya dawa hutokea pale ambapo bakteria, virusi, fangasi, na vimelea vingine vya magonjwa haviitikii tena dawa, hivyo kuongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa, watu kuugua na hata vifo.WHO inaeleza kwamba kwa sehemu kubwa hali hii ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa inasababishwa na matumizi mabaya ya dawa za viuavijumbe maradhi.Utafiti huu mpya uliotolewa leo unajumuisha uthibitisho mpya na maarifa ya kitaalamu ili kuongoza utafiti na maendeleo kwa ajili ya viuavijiumbemardahi yaani Antibiotics mpya na kuhamasisha uratibu wa kimataifa ili kukuza uvumbuzi.Baadhi ya bakteria sugu zilizotajwa ni Neisseria gonorrhoeae inayosababisha na Mycobacterium tuberculosis inayosababisha ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).Orodha kama hii ya vijiumbemaradhi hatari kwa afya ya binadamu ambavyo vimejenga usugu dhidi ya dawa, ilitolewa na WHO miaka 7 iliyopita.Kusoma zaidi kuhusu ripoti hii mpya bofya hapa 
    2 min
  • Uchumi wa dunia umeboreka kidogo ingawa Afrika bado kuna changamoto - Nelly Muriuki
    Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya katikati ya mwaka ya hali na mtazamo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024 iliyotolewa leo inaonyesha matarajio ya kiuchumi duniani yameboreka tangu utabiri uliotolewa Januari 2024, lakini mtazamo ni wa matumaini yanayohitaji tahadhari. Je, Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezungumza na Nelly Rita Muriuki mchumi kutoka Idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA ambao ndio wamezindua ripoti hiyo. 
    7 min
  • 17 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics, na hali ya kibinadamu nchini Ukraine. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunaelekea nchini Afghanistan, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto.Makala inaturejesha hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulikozinduliwa ripoti ya nusu mwaka ya mtazamo wa ukuaji na matarajio ya uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024. Je Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezungumza na Nelly Rita Muriuki mchumi kutoka Idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA ambao ndio wamezindua ripoti hiyo.Na katika tunamsikia mama yake Hasenat, mtoto mwenye umri wa miezi saba anayeugua utapiamlo akisimulia jinsi mwanaye anaendelea kupata nafuu baada ya kula chakula cha tiba kiitwacho RUFT ambacho ni uji wenye virutubisho vya vitamini na madini kinachosambazwa na Shirikika la Umoja wa Mataifa ya kuhudumia Watoto, UNICEF.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    10 min
  • Mashirika ya kibinadamu yanahaha kuondoa watu huko Kharkiv Ukraine
    Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto. Video ya ofisi kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura ya Umoja wa Mataifa, OCHAinaanza kwa kuonesha watu wakishuka katika bus, hawa ni raia walioondolewa huko Kharkiv ambako mapigano kati ya Ukraine na Urusi yanaendelea. Uokoaji unaendelea kupitia mabasi yanayoratibiwa na mashirika ya misaada ya kibinadamu, watu binafsi wanaojitolea na serikali za mitaa. Kwa mujibu wa OCHA kati ya tarehe 10 na 15 Mei, karibu watu 2,400 wamefanikiwa kuhamishwa na kuletwa kwenye kituo cha muda ambapo wanapokea usaidizi. Mmoja wa watu hao ni Bibi huyu aitwaye Valentyna anayetujuza hali ilivyokuwa huko alipotoka "Sisi kwetu ni Okhrimivka. Tunaishi pamoja na binti yangu ambaye ni mlemavu.  Kijiji chetu kilipigwa na makombora. Kila kitu kimeharibiwa. Ni nyumba 35 tu zimesalia. Wakati wa milipuko ya mabomu tulikuwa tukijificha ghorofa ya chini.”Dmytro Filipskyi kutoka OCHA anasema zaidi ya watu 1,700 wameandikishwa kituoni hapo na wamepatiwa msaada. “Katika eneo hili utaona mashirika yasiyo ya kiserikali na ya misaada ya kibinadamu, mashirika ya Umoja wa Mataifa na ya kimataifa yakitoa msaada wa vifaa vya usafi na kujisafi, chakula, fedha, msaada wa kisaikolojia, ulinzi kwa watoto na makundi mengine yote. Mashirika yote yanahusika katika mchakato huu.” Mashirika ya kibinadamu yalikusanya rasilimali kwa haraka ili kutoa usaidizi wa dharura kwa watu wanaokimbia kusaka usalama. Wamekuwa wakifanya kazi katika kituo hicho ambacho ndio nimekuwa kitovu cha kupokea watu wote wanaokimbia machafuko katika Jiji la Kharkiv na kuratibu usambazaji wa misaada ya kibinadamu tangu kuongezeka kwa mapigano tarehe 10 mwezi huu wa Mei.
    3 min
  • 16 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Bahrain kwenye mji mkuu Manama, ambako wajasiriamali wamekusanyika kwa lengo la kutumia ugunduzi na ujasirimali kusongesha SDGs. Pia tunakuletea muhtasariwa habari kutoka ICJ, WHO na huko huko Bahrain, pamoja na uchambuzi wa neno “HIZAYA.”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea wito wake wa kutaka usitishwaji wa mashambulizi huko Rafah kwani wananchi wanazidi kuteseka kutokana na kulazimika kuhama kila wakati huku wakikosa huduma muhimu za kijamii ikiwemo msaada wa chakula na matibabu. Hii leo Mahakama ya Haki ICJ inasikiliza ombi kutoka taifa la Afrika Kusini ambalo linaiomba mahakama hiyo kuliwekea vikwazo zaidi jeshi la Israel ambalo linafanya mashambulizi ya anga na ardhini huko Ukanda wa Gaza mashambulizi ambayo yamegharibu maelfu ya maisha ya watu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO hii leo limetoa muhtasari wa ugonjwa wa kipindupindu ulimwenguni ambao mpaka sasa umetajwa kuenea katika mataifa 24 katika kanda tano za shirika hilo huku Afrika ikirekodi idadi kubwa ya wagonjwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “HIZAYA.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    12 min
  • Mafunzo ya UNIDO yameboresha bidhaa zetu sasa tunahitaji masoko ya uhakika
    Huko Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunafanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024. Zaidi ya washiriki 1000 ni wajasiriamali kutoka Afrika wakisaka kujenga mitandao na ubia ili kusaka masoko ya uhakika ya bidhaa zao na hatimaye kuondokana na umaskini, moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa. Mkutano umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya Viwanda, UNIDO ofisi ya ugunduzi wa teknolojia, ITPO nchini Bahrain. Assumpta Massoi aliyeko Manama anazungumza na mjasiriamali kutoka Kenya, Edith Lewela, Mwenyekiti wa kundi la wanawake wajasiriamali wa Taita-Taveta na pia mnufaika wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na UNIDO mwaka 2009. Bi. Lewela anaanza kuelezea manufaa ya mafunzo hayo ambayo anapatia pia wenzake.
    4 min
  • Ziara za Catriona Laing za kuwaaga viongozi Somaliland
    Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing ameendelea na ziara yake ya kuwaaga viongozi wa eneo hilo na sasa ametembelea Somaliland. Juzi Mei 12, Catriona Laing alikuwa  Dusmareb, mji mkuu wa jimbo la Galmudug katikati mwa Somalia ambako alipongeza juhudi za kupambana na ukeketaji. Kisha jana Mei 14 akatua Hargeisa mji mkuu wa Somaliland ambako  amekutana na uongozi na kujadili msaada wa Umoja wa Mataifa kwa maendeleo na juhudi za kibinadamu. Miongoni mwa aliokutana nao ni Rais Muse Bihi na wajumbe wa baraza lake la mawaziri na washauri."Tumekuwa na mjadala mzuri sana, na Rais amezungumza nami kuhusu mpango wa maendeleo, ambao unaweka maono yake ya muda mrefu ya kiuchumi kuhusu faida za 'uchumi wa buluu,' kuhusu madini, na kufikiria juu ya mabadiliko ya biashara ya mifugo kama tunajiandaa dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watu wenye maisha ya kuhamahama. Tumezungumza kuhusu jukumu la Umoja wa Mataifa katika kuunga mkono kufanikisha dira ya kiuchumi na kazi nyingine zote tunazofanya kuhusu maendeleo ya kijamii, afya, elimu, kibinadamu na katika maeneo mengine.Hali katika eneo la Laascaanood-Sool -ambako migogoro ilipamba moto mwaka jana, na kusababisha kupoteza maisha na maelfu ya watu kuyahama makazi yao pia ilijadiliwa kama anavyoeleza Bi Liang kwamba, "Kumekuwa na changamoto huko nyuma na sote tulifurahi kuona kwamba mambo yametulia, na Rais amenihakikishia kuwa ni lengo lake kwamba mambo yabaki shwari. Umoja wa Mataifa utafanya sehemu yake katika kutoa msaada wa kibinadamu na kutegua mabomu kwa manufaa ya watu katika eneo hilo.”Mwakilishi huyo Maalum wa Umoja wa Mataifa pia alichukua fursa hiyo kumtambulisha rasmi mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Hargeisa, Nikolai Rogosaroff, ambaye alichukua wadhifa wake Machi mwaka huu. Alielezea uwepo wake hapo kama ishara ya kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kusaidia maendeleo ya ndani na juhudi za kibinadamu. Hivi sasa, zaidi ya mashirika kumi na mbili ya Umoja wa Mataifa, fedha na program yanafanya kazi Somaliland.Bi. Laing atakamilisha kazi yake baadaye mwezi huu wa Mei.
    2 min
  • 15 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza, na ziara za Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing. Makala tunakupeleka mjini Manama huko Bahrain na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kuonya kuhusu hali mbayá ya Rafah Gaza ambako mashambulizi ya Israel yanaendelea kukatili Maisha ya watu na kulazimisha maelfu kufungasha vitago tena kwenda kusaka usalama. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing ameendelea na ziara yake ya kuwaaga viongozi wa eneo hilo na sasa ametembelea Somaliland.Makala tunakwenda Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunakofanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 ambapo Assumpta Massoi amezungumza na mjasiriamali kutoka Kenya, Edith Lewela, Mwenyekiti wa kundi la wanawake wajasiriamali wa Taita-Taveta. Yeye ni mnufaika wa  mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na UNIDO mwaka 2009, sasa anafundisha wenzake.Mashinani tutaelekea katika mitaa ya mabanda ya Nairobi nchini Kenya      kusikia ni kwa jinsi gani Umoja wa Mataifa unatumia michakato ya kiteknolojia ya kompyuta  kutoa msaada wa chakula kwa wakati.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    11 min
  • UN: Hali Rafah ni mbayá mashambulizi yanakatili maisha na kufurusha watu kwa maelfu
    Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kuonya kuhusu hali mbayá ya Rafah Gaza ambako mashambulizi ya Israel yanaendelea kukatili maisha ya watu na kulazimisha maelfu kufungasha vitago tena kwenda kusaka usalama. Kwa mujibu wa tarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kuendelea kwa mashambulizi ya wanajeshi wa Israel, kwenye Ukanda wa Gaza kwa njia ya angani, ardhini na baharini kunazidisha vifo vya raia, kulazimika wengi kukimbia na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya makazi na miundombinu mingine muhimu ya raia. Shirika hilo limeongeza kuwa na mashambulizi ya ardhini ya Israeli yanaendelea kupanua wigo, haswa katika maeneo ya kusini mwa mji wa Gaza na Mashariki mwa Rafah, hususan karibu na Kerem Shalom na vivuko vya Rafah.Kana kwamba hayo hayatoshi Philippe Lazzarini ambaye ni Kamishina Mkuu wa UNRWA amesema kumekuwa na jaribio lingine la uchomaji moto la watoto na vijana wa Israel kwenye majengo ya UNRWA huko Jerusalem jana usiku. Akiweka video fupi inayoonyesha moto ukiwaka nje ya majengo ya ofisi hizo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X Lazzarini amesema imetosha na mashambulizi hayo lazima yakome.Likimulika zaidi watoto shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema Kuongezeka kwa uhasama huko Rafah na kote katika Ukanda wa Gaza kumeongeza mateso ya mamia ya maelfu ya watoto, ambao wamevumilia jinamizi lisiloisha kwa siku 218 zilizopita.Shirika hilo limerejea wito wake wa kukomeshwa mara moja uhasama ili kuokoa maisha ya raia wasio na hatia wakiwemo malaki ya watoto.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaendelea kujitahidi kusambaza msaada wa chakula licha ya changamoto kubwa za kiusalama na miundombinu. Shirika hilo linasema mamia ya familia zinalazimika kushinda njaa ili chakula kidogo kinachopatikana ziweze kulisha watoto wao. Miongoni mwa chakula kinachotolewa ni lishe ambayo iko tayari kuliwa hususan kwa watoto.
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners