Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 14 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika ugunduzi na ukuaji uchumi. Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO ni sehemu ya wawezeshaji wa jukwaa la WEIF 2024 na mwakilishi wake amezungumza na mwenyeji wetu huko Manama Bahrain Assumpta Massoi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Huko Gaza Wapalestina zaidi waliouawa kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Israel wakiendelea kutambuliwa na mamlaka ya afya ya eneo hilo, wasaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza tena kwamba kwa hakika katika ya watu 35 ambao wameshauawa, idadi kubwa ya wanawake na watoto. Kufuatia tathmini za kina nchini Malawi na Msumbiji, Timu huru ya Tathmini ya Kukabiliana na Mlipuko wa Polio (OBRA) leo Mei 14 imependekeza kufikia ukomo wa mlipuko wa virusi vya polio aina ya 1 (WPV1) nchini Malawi na Msumbiji, kuashiria hatua muhimu katika mapambano dhidi ya polio katika eneo la Afrika. Kisa cha mwisho cha WPV1 katika Kanda ya Afrika, kilichohusishwa na aina hiyo ya polio kiliripotiwa katika Jimbo la Tete la Msumbiji mnamo Agosti 2022. Jumla ya wagonjwa tisa waligunduliwa nchini Msumbiji na nchi jirani ya Malawi, ambapo mlipuko huo ulitangazwa Februari 2022.Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa njia ya video leo amewaeleza viongozi wa kimataifa jijini Paris Ufaransa kwamba “Tunahitaji hatua ya haraka ili kumpa kila mtu, kila mahali ufikiaji wa  nishati safi ya kupikia.” Guterres amewasisitiza viongozi hao wanaoshiriki Mkutano kuhusu nishati safi ya kufikia barani Afrika kwamba, “Tunacho kichocheo cha mafanikio: Ramani yetu ya Kimataifa ya Ubadilikaji ulio wa haki na jumuishi kuelekea nishati safi ya kupikia.”Mashinani tutaelekea nchini Somalia kufuatilia ziara za Bi. Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia za kuwaaga viongozi nchini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    12 min
  • Uwekezaji kwa wajasiriamali duniani kumulikwa Manama, Bahrain
    Jukwaa la 5 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 linaanza kesho kwenye mji mkuu wa Bahrain, Manama ukileta pamoja washiriki zaidi ya 1000, wakiwemo wajasiriamali kutoka pembe zote za dunia. Jukwaa hili linafanyika kwa siku tatu na na maudhui ni kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa kuendeleza uvumbuzi na ukuaji wa kiuchumi. Jukwaa hili linalenga basi kupatia majawabu changamoto za dunia ikiwemo umaskini, ukosefu wa usawa, mabadiliko ya tabianchi, amani, haki kwa muktadha wa SDGs. Dkt. Hashim Hussein, ni mtaalamu wa kuendeleza uwekezaji katika shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO anaeleza ni nini hasa wanatarajia kutoka jukwaa hili alipopata fursa kuzungumza na Assumpta ambaye tayari yuko Manama kutujuza kitakachojiri.
    5 min
  • Mashirika ya UN yaonya kuwa maelfu ya maisha ya watu El Fasher Sudan yako hatarini
    Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. Kwa mujibu wa Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, “Shambulio hilo limeharibu paa la hospitali katika kituo cha huduma za dharura kwenye Hospitali ya Sourthen katika mji wa El Fasher ambayo ndio hospitali pekee inayofanyakazi kwas asa katika jimbo la Darfur Kaskazini na ambako vifaa vya matibabu na dawa sasa karibu vinakwisha.” Amesema takriban watu 800,000 wanaishi katika mji wa El Fasher na maelfu ya maisha yao yako hatarini huku taifa zima la Sudan likiwa katika hali mbaya.Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limesema makumi ya raia waliuawa mwishoni mwa wiki katika mapigano mapya  makubwa yaliyozuka Ijumaa kati ya vikosi vya serikali ya Sudan SAF na vikosi vya msaada wa haraka RSF katika eneo la Darfur Kaskazini ambalo ndilo lililosalia chini ya udhibiti wa serikali.Shirika hilo linasema hivi sasa karibu watu milioni 25 nchini Sudan wanahitaji msaada wa kibinadamu na watu milioni 17.7 miongoni mwao wanakabiliwa na hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula na kuna hofu kubwa ya kurejea kwa baa la njaa Darfur.Nayo mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la luhudumia wakimbizi UNHCR na la uhamiaji IOM yamesema takriban watu 570,000 wametawanywa katika jimbo la Darfur Kaskazini katika miezi 13 iliyopita, wengine milioni 6.7 nchini Sudan ni wakimbizi wa ndani huku milioni 1.8 wamekimbilia katika nchi za jirani.
    2 min
  • 13 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi makali yanayoendelea nchini Sudan, na huduma za afya uzazi Kalobeyei nchini Kenya.  Makala inatupeleka Bahrain ambako Jukwaa la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali WEIF 2024 linaanza Manama hapo kesho Jumanne, na mashinani tunasikiliza simulizi ya mkimbizi wa ndani nchini DRC.Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto.Makala inatupeleka Bahrain huko Jukwaa la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali WEIF 2024 linaanza kesho Jumanne Kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Manama likiwaleta pamoja washirika mbalimbali wakiwemo viongozi katika sekta ya biashara duniani na wajasiriamali. Jukwaa hili linafanyika kwa siku tatu na mwenzetu Assumpta tayari yuko Manama kutujuza kitakachojiri.Na mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya mkimbizi wa ndani.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    12 min
  • Kalobeyei: Wakunga wafurahia kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga
    Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto. Anasema anaitwa Jane Rose Akwam, ni mkunga anayehudumia wajawazito pamoja na watoto wachanga, huduma ambayo inatolewa bure katika katika eneo hili la Kalobeyei.  “Katika hospitali hii tunafanya kazi na jamii za wenyeji na wakimbizi, wanapokuja najitambulisha na kuwaeleza kazi yangu katika idara hii na pia nawaelezea kile ninachokuelezea ni kile ambacho hata mimi nilipitia.”Wakati ulimwengu ulisherehekea siku ya wauguzi hapo na siku ya wakina mama hapo jana Mei 12, Rose anaeleza kile kinachompa furaha zaidi katika kazi yake hii ya ukunga.“Ni furaha yangu ninapomuona mjamzito anapokuja kwa ajili ya kujifungua na mwisho wa siku anajifungua mtoto mwenye afya njema. Huduma hapa hutolewa bure ukitoa hata sumni bado itakurudia mwenyewe. Ni kama ninapotoa huduma kwa hawa wakina mama vyema najua zawadi yangu ipo pale.”
    2 min
  • Ally Mwamzola: Vijana tushiriki kuanzia kuandaa hadi kutekeleza ‘Mkataba wa siku zijazo’
    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Yeye akiwa anapeperusha bendera ya vijana kwa kuzingatia kuwa pia ni Mratibu wa Mradi wa Ujumbe wa Vijana wa Afrika kwenda Umoja wa Mataifa anayataja mambo matatu ambayo katika mkutano huu vijana walikuwa wanayalenga zaidi. Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.
    4 min
  • Peter Njenga: Mchezo wa riadha watumika kukaribisha wageni wa mkutano Kenya
    Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Bwana Njenga akaoanisha michezo na amani.
    2 min
  • 10 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) unaofunga pazia leo, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa hotuba yake kwa waandishi wa habari, na tutasikia ujumbe wa washiriki wengine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.Na katika mashinani tunasalia mjini Nairobi katika mkutano wa asasi za kiraia kusikia ujumbe kuhusu janga la mafuriko yanayoendelea nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Guterres: Afrika inaweza kuwa jabalí la nishati jadidifu
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Katibu Mkuu Guterres [GUTERESH] amesema dunia inakabiliwa na majanga lukuki, lakini Afrika ndio inaathiriwa vibaya kwa kiasi kikubwa.Bara la Afrika linatikiswa na hali mbayá ya hewa kupindukia, ikichochewa na janga la tabianchi ambalo halijasababishwa na bara hili. Kuanzia mafuriko makubwa mashariki hadi ukame mkali kusini.Afrika inaweza kuwa jabali la nishati jadidifu, amesema Guterres,  kwani ina hifadhi ya asilimia 30 ya madini muhimu kwa ajili ya nishati jadidifu, na asilimia 60 ya rasilimali ya sola au nishati ya jua. Lakini katika miongo ya karibuni, imepokea asilimia mbili tu ya uwekezaji kwenye nishati jadidifu.Amesema jopo la mpito muhimu wa madini husika kwenye nishati litaanda kanuni za hiari ili nchi zinazoendelea zinufaike na rasilimali hizo.Ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kutimiza ahadi zao wa ufadhili wa tabianchi ikiwemo kusaidia nchi kujiandaa kwa madhara makubwa ya tabianchi, na serikali za Afrika ziunge mkono juhudi za kuondokana na mafuta kisukuku.Ametumia pia hotuba yake kupongeza Kenya kwa kukubali kuongoza juhudi za kimataifa za kukabili ghasia nchini Haiti, wakati huu ambapo taifa hilo linakumbana na madhara ya mafuriko yaliyosababisha vifo, ukimbizi na uharibifu wa mali.
    10 min
  • Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuinua uchumi na kusongesha agenda ya SDGs - Zahra Salehe
    Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu. Mfano ni Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ulifanyika hivi karibuni na mmoja wa waliohudhuria ni Zahra Salehe, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, ICCAO Tanzania ambaye katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii tunapata kufahamu baadhi ya malengo yanavyotekelezwa na shirika lake nchini Tanzania. 
    6 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners