Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 29 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa. Makala inatupeleka nchini Sudan kusikia simulizi ya mmoja wa wakimbizi na mashinani tunakupelekea nchini Ethiopia kusiki jinsi ambavyo wasichana wanavyosaidiwa kubaki shule.Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee  wa kimataifa. Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Makala inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.Na mashinani tutaelekea Gambella nchini Ethiopia  kusikia ni kwa jinsi gani shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF linahakikisha kuwa wasichana hawakosi masomo yao kwa kukosa sodo au taulo za kike wakati wa hedhi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    10 min
  • Ulinzi wa amani wa UN ni ushirikiano wa kipekee wa kimataifa
    Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee  wa kimataifa. Katika ujumbe wake kwa siku hii Antonio Guterres amesema "Leo tunawaenzi walinda amani zaidi ya 76,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wanadumisha lengo bora zaidi la ubinadamu, amani. Siku baada ya siku, wakihatarisha Maisha yao, wanawake na wanaume hawa wanafanya kazi kwa ujasiri katika baadhi ya maeneo hatari na yasiyo na utulivu duniani ili kulinda raia, kudumisha haki za binadamu, kumsaidia masuala ya uchaguzi na kuimarisha taasisi. Zaidi ya walinda amani 4,300 wamelipa gharama ya Maisha yao wakati wakihudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Hatutawasahau kamwe.”Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa maudhui ya siku ya mwaka huu yanaashiria kwamba wakati ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa umethibitika kuwa sehemu ya suluhu kwa zaidi ya miaka 75 ukizisaidia nchi mwenyeji kuvuka mapito kutoka kwenye migogoro hadi amani muhtasari wa Sera wa Katibu Mkuu wa Ajenda mpya ya amani unaweka njia ya operesheni za kimataifa za amani na usalama mbele ili kusalia kuwa zana zinazofaa kushughulikia vita na migogoro ijayo.Naye mkuu wa operesheni za Umoja wa Mataifa za ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix,akiongeza sauti yake katika siku hii amesema "Ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unasalia kuwa ushirikiano wa kipekee wa kimataifa, huku walinda amani kutoka zaidi ya nchi 120 wakifanya mabadiliko yenye tija kila siku kwa mamilioni ya watu katika baadhi ya maeneo magumu zaidi duniani. Tunapokabiliana na changamoto za kesho, ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unaendelea kubadilika, na kuhimiza ushirikiano kuwa mahiri, msikivu na unaofaa kwa madhumuni yaliyokusudiwa, kukuza utulivu, kulinda walio hatarini na kusaidia kujenga amani ya kudumu."Siku ya Kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kila mwaka Mei 29 na ilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2002 ili kuwaenzi wanaume na wanawake wote katika operesheni za ulinzi wa amani na kuenzi kumbukumbu ya wale wote waliopoteza Maisha yao kwa lengo la kuleta amani.
    3 min
  • Jenerali Birame Diop: Ulinzi wa amani uwe na mkakati wa kudhibiti habari potofu na za uongo
    Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya walinda amani duniani, Jenerali Diop ambaye anatamatisha jukumu lake anasema angalau kwa sasa kuna jawabu la ulinzi wa amani ambalo licha ya changamoto zake linaleta nuru.“Na ulinzi wa amani umethibitisha kuwa unaweza kutatua baadhi ya mizozo. Ninaweza kukupatia mfano wa Timor-Letse [TIMORLETSI]. Ninaweza kukupa mifano ya Côte d'Ivoire, ya Sierra Leone, ya Liberia, ambako ulinzi wa amani umesaidia kurejesha amani na utulivu. Na sasa nchi hizi hata zinashiriki kwenye ulinzi wa amani.”Ingawa ulinzi wa amani unazaa matunda, kwa Jenerali Diop ambaye anatoka Senegal, jambo muhimu ni kuzidi kuboresha huduma hiyo kwani itaendelea kuwa muhimu huku Umoja wa Mataifa ukihakikisha ujumbe wa ulinzi wa amani unapatiwa mamlaka na majukumu sahihi ili kukidhi mantiki ya uwepo wake. Na zaidi ya yote.“Tunatakiwa pia leo hii kuambatanisha ujumbe wa ulinzi wa amani na mfumo wa kimkakati wa mawasiliano ili kuzuia habari potofu na habari za uongo zinazoharibu kila kitu tunachofanya. Ulinzi wa amani hautafanikiwa iwapo nchi mwenyeji haiungi mkono ujumbe wa ulinzi wa amani.”
    2 min
  • 28 MEI 2024
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Watu zaidi ya 2000 wahofiwa kufunikwa na maporomoko ya udongo Papua New Guinea , Umoja wa Mataifa wasaidia-Ripoti ya UNRWA inasema wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na dharura ya kiafya isiyokuwa na mfano wake iliyosababishwa na vita mbaya zaidi katika historia ya Gaza- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  ameuambia Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS4) Antigua na Barbuda kwamba ulimwengu unahitaji kuchukua hatua ili kusaidia vyema na kuhamasisha ufadhili kwa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS) -Katika kuelekea siku ya walindamani hapo kesho leo kikosi cha Tanzania TANZBAT11 nchini DRC chashikamana na wananchi katika miradi mbalimbali-Na mashinani utamsikia mlindamani kutoka Italia anayehudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL
    11 min
  • Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ yaamua juu ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu Gaza
    Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo.Leo Kwa kura 13 dhidi ya 2 mahaka ya ICJ imeamua kwamba:1. Inathibitisha tena hatua za muda zilizoainishwa katika Maagizo yake ya tarehe 26 Januari 202 na 28 Machi 2024, ambayo yanapaswa kutekelezwa mara moja na kwa ufanisi2. Imeainisha hatua zifuatazo za muda kwamba : Taifa la Israeli, kwa kuzingatia wajibu wake chini ya Mkataba juu ya Kuzuia na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, na kwa kuzingatia hali mbaya ya maisha inayowakabili raia katika Jimbo la RafahIsitishe mara moja mashambulizi yake ya kijeshi, na hatua nyingine yoyote katika jimbo la Rafah ambayo yanaweza kusababishia kundi la Wapalestina Gaza hali hiyo ya maisha inayoweza kuleta uharibifu wa kimwili kwa ujumla au sehemu;Iendeleel kukiacha wazi kivuko cha Rafah  kwa utoaji usiozuiliwa kwa kiwango cha haraka cha huduma za msingi zinahitajika na msaada wa kibinadamu;Kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha ufikiaji usiozuiliwa wa Ukanda wa Gaza kwa tume yoyote ya uchunguzi, ujumbe wa kutafuta ukweli au chombo kingine cha uchunguzi kilichoagizwa na vyombo vyenye uwezo wa Umoja wa Mataifa kuchunguza tuhuma za mauaji ya kimbari;3. Mahakama imeamua kwamba Israeli itawasilisha ripoti kwa Mahakama juu ya hatua zote kuchukuliwa ili kutekeleza agizo hili, ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe ya agizo hili.
    2 min
  • WHO: COVID-19 imerudisha nyuma muongo wa maendeleo ya umri wa watu kuishi
    Ripoti mpya ya Takwimu za Afya Ulimwenguni iliyotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, inaonyesha kuwa janga la COVID-19 limebadilisha mwelekeo wa kuongezeka kwa umri wa watu kuishi wakati wa kuzaliwa na matarajio ya maisha yenye afya wakati wa kuzaliwa HALE.Ripoti hiyo ya takwimu za afya ulimwenguni hutolewa kila mwaka na WHO ikijumuisha viashirikia vya afy na vinavyohusiana na imekuwa ikitolewa tangu mwaka 2005.Ripoti yam waka huu kwa mujibu wa WHO imetathimini Zaidi ya viashiria 50 vinavyohusiana na afya kuanzia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mikakati kazi 13 ya WHO au GPW13.Ripoti inasema Janga la COVID-19 limefuta karibu muongo mmoja wa maendeleo katika kuboresha umri wa watu kuishi ndani ya miaka miwili tu. Kati ya 2019 na 2021, umri wa kuishi duniani ulipungua kwa mwaka 1.8 hadi miaka 71.4 ukirejea nyuma hadi kiwango cha mwaka 2012.”Pia ripoti imeongeza kuwa umri wa kuishi kwa afya duniani ulipungua kwa miaka 1.5 hadi miaka 61.9 mwaka 2021 ukiwa umerudi nyuma kwenye kiwango cha mwaka 2012. Ripoti hiyo ya 2024 pia imeainisha ni jinsi gani athari hizo zimehisiwa tofauti na hazilingani kote duniani.Maeneo ya WHO yaliyoathirika Zaidi ripoti inasema ni Ukanda wa Amerika na Kusini-Mashariki mwa Asia, ambako umri wa kuishi ukishuka kwa takriban miaka 3 na matarajio ya maisha yenye afya yakishuka kwa miaka 2.5 kati ya mwaka 2019 na 2021.Kinyume chake, Kanda za Pasifiki Magharibi zimeathiriwa kidogo wakati wa miaka miwili ya kwanza ya janga hla COVID-19 na kupata hasara ya chini ya miaka 0.1 katika umri wa kuishi na miaka 0.2 katika matarajio ya maisha yenye afya.
    3 min
  • Wanajeshi walinda amani wa UN wana majukumu mengine muhimu zaidi ya bunduki: TANBAT 7
    Zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika  Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA)
    4 min
  • FAO na wadau wawakutanisha wadau wa kilimo na chakula Tanzania
    Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021. Hamad Rashid wa Redio washirika wetu Mviwata FM ya Mkoani Morogoro amehudhuria Kikao hicho na kuandaa taaarifa hii. 
    4 min
  • 24 MEI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi ya ICJ ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel, na  mifumo ya chakula nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo. Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021.Katika makaala zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika  Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA).Na mashina Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM inaendelea kutoa vifaa muhimu vya nyumbani na usafi pamoja na usaidizi wa pesa kwa maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko yanayoendelea nchini Kenya, Mahmood Abdirahman, kuongozi wa jamii katika kaunti ya Garissa anasimulia changamoto zilizowakumba jamii hizo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners