Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 07 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia usalama wa chakula, na ripoti ya ILO kuhusu suala la ajira Gaza wakati huu wa machafuko. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. Tukimulika suala la ajira Gaza ambapo ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda huo wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5..Katika makala Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa anatupeleka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mashambulizi ya mara kwa mara kutoka makundi ya waasi waliojihami dhidi ya raia, yamesababisha Umoja wa Mataifa na kuja na mfumo wa kutoa tahadhari mapema ili kuimarisha ulinzi wa wa raia.Mashinani leo ikikiwa ni siku ya usalama wa chakula duniani tunakwenda nchini Sudan kumulika masuala ya lishe.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    11 min
  • Vita katika ukanda wa Gaza yasababisha ukosefu wa ajira kufikia asilimia 80 – ILO
    Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5. Takwimu hizo zinamaanisha kuwa kati ya kila watu 10 Ukanda wa Gaza wenye uwezo wa kufanya kazi, ni watu wawili tu wenye ajira, imesema ripoti hiyo iliyoandaliwa na ILO kwa ushirikiano na Ofisi Kuu ya Takwimu ya Palestina kuonesha ni kwa vipi vita imeathiri soko la ajira na njia za kujipatia kipato kwenye eneo hilo la Palestina linalokaliwa na Israeli.Ripoti inasema miezi minane ya vita imesababisha watu kupoteza kwa kiwango kikubwa ajira na mbinu zao za kujipatia kipato Gaza.Ukingo wa Magharibi nako vita hiyo imeathiri vibaya kwani ukosefu wa ajira umefikia asilimia 32.Ripoti inaonya kuwa takwimu hazijumuishi wale waliolazimika kuacha kazi kwa sababu ya vita, na kwamba idadi halisi ya waliolazimika kuacha kazi ni kubwa kuliko kinachodokezwa kwenye ripoti.Biashara zikiwa zimefungwa, kipato cha kaya nacho kimepungua kwa asilimia 87 na zinatuma watoto wao kufanya kazi ili kupata kipato.Mkurugenzi wa ILO Kanda ya nchi za kiarabu Ruba Jadarat anasema vita Gaza imesababisha vifo, hali ngumu ya kibinadamu ikiambatana na kusambaratika kwa hali ya kiuchumi na kujipatia kipato Gaza na Ukingo wa Magharibi. Hivyo kurejesha mbinu za watu kujipatia kipato na kuweka fursa za ajira zenye hadhi ni muhimu ili wapalestina waweze kukwamuka kutoka kwenye vitisho na ukatili ambao vita imewatumbukiza.Amesema kukwamuka huko kuende sambamba na harakati za sasa za usaidizi wa kibinadamu na kwamba ILO na wadau wake wanatekeleza kupitia Mpango wa Hatua wa Dharura kwa Palestina.
    3 min
  • 06 JUNI 2024
    Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Gaza Nuiserat Israel imeshambulia shule moja iliyokuwa inahifadhi wakimbizi 6,000 wa kipalestina na kuua watu 35, na wengine wengi wamejeruhiwa,-Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo kumefanyika tukio la kukumbuka wafanyakazi 188 wa chombo hicho waliouawa mwaka 2023 pekee wakiwemo 135 watumishi wa UNRWA waliouawa ukanda wa Gaza-Duniani kote mtoto mmoja kati ya wanne anaishi katika mazingira ya umaskini wa chakula akila aina moja au mbili tu ya mlo kutokana na vita, mizozo, janga la tabianchi na ukosefu wa uwiano, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. -Katika mada kwa kina utamsikia Erick Mukiza mmoja wa wanasheria waliothibitishwa kuwa wapatanishi au wasuluhishi wa migogoro nje ya mahakama nchini Tanzania na mipango yake ya kujumuisha wenye ulemavu ili wanufaike na mpango huo wa serikali ya Tanzania.-Na katika jifinze Kiswahili Onni Sigalla anafafanua maana ya neno Nyendea
    10 min
  • UN: Kila mtu ana wajibu wa kuhusika na urejeshaji wa ubora wa ardhi
    Leo ni siku ya mazingira duniani na Umoja wa Mataifa unaisa dunia kuchukua hatua sasa kurejesha Uhai wa ardhi iliyoharibiwa na kujenga mnepo dhidi ya kuongezeka kwa hali ya jangwa na ukame na hiyo ndio kaulimbiu ya siku ya mwaka huu. Akisisitiza maudhui hayo Inger Andersen Mkurugenzi mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP amemtaka kila mtu kujiunga na harakati za kimataifa za kurejesha ardhi yenye afya na kujenga mnepo wa majanga mengine kama vile ukame na hali ya jangwa. Flora Nducha anatupasha zaidi katika makala hii..
    5 min
  • Lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani kwenye nyuzijoto 1.5 linaning’inia - Katibu Mkuu
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres asubuhi ya leo saa za New York, Marekani kupitia Hotuba Maalumu kuhusu Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ametahadharisha kuhusu hatari ya wazi ya uwezekano wa ongezeko la joto juu ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi linaloukabili ulimwengu ikiwa uzalishalishaji wa hewa chafuzi utaendelea kwa viwango vya sasa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Ni hotuba ambayo imepewa jina “Wakati wa Ukweli”…Hotuba ambayo Katibu Mkuu wa Guterres ameitumia kuuleza ulimwengu ukweli kuwa utafiti wa kitaalamu unaonesha kuwa ni tani bilioni 200 tu za hewa ukaa ambazo dunia inaweza kuzihimili kabla ya kuvuka nyuzijoto 1.5 za Selsiasi  juu ya viwango vya kabla ya viwanda jambo ambalo ni hatari kubwa kwa ulimwengu.Ikumbukwe kuwa chini ya Mkataba wa Paris mnamo mwaka 2015, nchi zilikubaliana kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa chafuzi duniani ili kuwezesha ongezeko la muda mrefu la wastani wa joto la uso wa dunia kuwekwa chini ya nyuzijoto 2 za selsiasi juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda na kuendeleza juhudi za kulipunguza joto hadi nyuzijoto 1.5 za selsiasi kisha kuhakikisha halizidi hapo.Lakini kiongozi huyu wa Umoja wa Mataifa anaeleza kwamba kwa kasi ya sasa ya uzalishaji hewa chafuzi kwa kiasi cha tani bilioni 40 kwa mwaka ni wazi uwezo wa dunia kuendelea kudhibiti joto lisipande utaisha mapema.  “Sote tunaweza kufanya hisabati. Kwa kiwango hiki, uwezo wote wa dunia kuhimili hewa ukaa utaondolewa kabla ya mwaka 2030. Ukweli ni kwamba uzalishaji wa hewa chafuzi duniani unahitaji kushuka kwa asilimia tisa kila mwaka hadi mwaka 2030 ili kuweka hai kikomo cha ongezeko la nyuzi joto 1.5. Lakini zinaelekea kubaya. Mwaka jana zilipanda kwa asilimia moja. Ukweli ni kwamba tayari tunakabiliwa na mashambulizi katika eneo la nyuzijoto 1.5 za Selsiasi.” Amesema Guterres.Guterres ameeleza kwamba hakuna nchi inayoweza peke yake kutatua janga la tabianchi akisema, “Huu ni wakati wa kila mtu kushiriki. Umoja wa Mataifa unajitolea kufanya kazi ili kujenga uaminifu, kutafuta ufumbuzi, na kuhamasisha ushirikiano ambao ulimwengu wetu unahitaji sana.”Na kwa vijana, kwa mashirika ya kiraia, kwa miji, mikoa, biashara na wengine ambao wamekuwa wakiongoza hatua kuelekea ulimwengu salama na safi, Katibu Mkuu amesema, Asante.
    3 min
  • 05 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya mazingira duniani, na msaada wa kibinadamu nchini Haiti. Makala tunamulika hatua za kurejesha afya ya ardhi iliyoharibiwa na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe wa Martin Griffiths anayestaafu mwishoni mwa Juni. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres asubuhi ya leo saa za New York, Marekani kupitia Hotuba Maalumu kuhusu Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ametahadharisha kuhusu hatari ya wazi ya uwezekano wa ongezeko la joto juu ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi linaloukabili ulimwengu ikiwa uzalishalishaji wa hewa chafuzi utaendelea kwa viwango vya sasa. Licha ya machafuko na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha huko nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani limeendelea kuimarisha operesheni zake katika mji mkuu wa Port-au-Prince na kusaidia jamii zilizoathiriwa na ghasia ambapo kwa mwezi Mei shirika hilo limeweza kuwafikia zaidi ya watu 93,000.Katika makala ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani Umoja wa Mataifa unaisa dunia kuchukua hatua sasa kurejesha afya ya ardhi iliyoharibiwa na kujenga mnepo dhidi ya kuongezeka kwa hali ya jangwa na ukame. Na hiyo ndio kaulimbiu ya siku ya mwaka.Mashinani tunasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kusikiliza ujumbe, wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura Martin Griffiths anayestaafu wadhifa huo mwishoni mwa Juni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • WFP yafanikiwa kufikisha Msaada wa chakula nchini Haiti licha ya hali tete ya usalama
    Licha ya machafuko na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha huko nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani limeendelea kuimarisha operesheni zake katika mji mkuu wa Port-au-Prince na kusaidia jamii zilizoathiriwa na ghasia ambapo kwa mwezi Mei shirika hilo limeweza kuwafikia zaidi ya watu 93,000. Kwa mujibu wa tathmini ya viwango vya njaa iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu nchini Haiti, takriban watu milioni 5 ambao ni sawa na nusu na idadi ya watu wote wa taifa hilo, wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakula ikiwemo watu milioni 1.64 ambao wametajwa kuwa hatua moja tu kabla ya kufikia baa la njaa yani IPC4. Maisha ya wanajamii yamebadilika sana, wale waliokuwa wanaweza kujikimu sasa wamegeuka ombaomba kama anavyoeleza bibi Heugenie Pierre Charles, mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa Port- au – Prince. “Kuna wakati mwingine nakuwa na njaa sana. Nawaomba watu wanaokula wanigawie kidogo wanachokula. Lakini wananidhalilisha. Huko nyuma sikuwahi kuwa naomba, nilikuwa naweza kuendesha biashara zangu. Inaniuma sana. Nilikuwa na kazi yangu, lakini magenge ya wenye silaha yamesababisha nifunge. Na sasa naishi katika hali ambayo inanifanya nalia. Nipo hapa katika kambi ya wakimbizi wa ndani. Nilikuwa nimebakiwa na birika tu. Kwa bahati mbaya imeibiwa. Sasa sina kitu chochote. Nilikuwa natumia birika yangu kuchemsha chai na chakula.”WFP kwa kutambua madhila yanayowakumba wananchi mwezi Mei ilifanikiwa kuingiza shehena ya chakula nchini Haiti na miongoni mwa walionufaika ni zaidi ya wananchi 93,000 walioko Cité Soleil, mojawapo ya vitongoji vilivyo vigumu kufikika kutokana na usalama, walifanikiwa kufikishwa msaada wa chakula kwani wananchi hao wako hatarini zaidi kukumbwa na njaa.Mwakilishi wa WFP nchini Haiti Jean-Martin Bauer anasema ndege ya shirika hilo iliyotua Port au Prince mwezi Mei imekuwa mkombozi. “Barabara za kuingia na kutoka katika mji wa wa Port-au-Prince zinashikiliwa na makundi yenye silaha. Bandari ilifungwa muda mrefu uliopita Kwani iliporwa, na uwanja wa ndege nao ukafungwa, kwa ufupi Port au Prince kwa miezi michache imekuwa kama kisiwa. Kwa hivyo ni muhimu sana kwa WFP na wasaidizi wengine wa kibinadamu kuweza kuleta misaada mjini hapa na, kuendesha programu muhimu. Kwa hivyo huduma muhimu ambazo watu wanategemea, iwe huduma ya afya, maji na usafi wa mazingira, chakula, zinahitaji usafirishaji wa bure wa bidhaa na watu, na hivi sasa hatujapata hiyo. Kwa hivyo tunachofanya na safari hii ya ndege ni kufungua tena mlango huo na kuhakikisha kuwa mahitaji muhimu yanaingia ili kuruhusu huduma hizi muhimu kufanya kazi.”Mbali na kusambaza misaada mbalimbali ya chakula kwa mwaka huu WFP imesaidia zaidi ya watu 108,000 waliokimbia makazi yao kwa kuwapatia chakula cha moto. Pia wanatoa Msaada wa kuwapatia fedha taslimu na mwitikio huu wa kibinadamu pia unajumuisha nyongeza ya lishe kwa kaya zilizo na wajawazito au watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
    4 min
  • 04 JUNI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako UNICEF na wadau wake imefanikisha utengenezaji wa sodo za kufuliwa. Piatunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, wahamiaji kutoka bara la Afrika na watoto katika migogoro. Mashinani inatupeleka nchini DR Congo, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura (OCHA) imeripoti ubomoaji wa makazi leo kwenye eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu katika miji ya Shuqba, Al Jwaya na Mantiqat Shi'b al Butum, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) imeangazia hatari zinazowakabili wakimbizi na wahamiaji wanapokuwa njiani kutoka Afrika kwenda Ulaya. UNHCR imeweka wazi kuwa wengi wao hufariki dunia wakivuka jangwa au karibu na mipaka, hufanyiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Shirika hilo limetoa wito kwa wafadhili kuangazia usaidizi na watu kuelezwa njia mbadala halali za kuhama nchi.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kukumbuka watoto walio kwenye maeneo yenye mizozo ikihusisha ukatili na unyanyasaji, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Denise Brown ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kukataa kuhalalisha vita na athari zake kwa watoto. Akitathimini hali ya watoto nchini Ukraine kutokana na uvamizi wa Urusi amesema zaidi ya watoto 600 wameshauawa na 1,420 wamejeruhiwa tangu Februari mwaka 2022.Katika mashinani na ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka watoto wasio na hatia waathiriwa wa uvamizi na ukatili tunaelekea nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya msichana ambaye alitumikishwa na makamanda wa kundi la waasi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    14 min
  • Watumiaji wa baiskeli wasema manufaa ni zaidi ya afya
    Baiskeli! Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wake tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama nafuu, hakichafui mazingira na zaidi ya yote afya kwa watumiaji kwani ni mazoezi. Huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, taifa lililo Afrika Mashariki, utamaduni wa kutumia baiskeli kama njia ya usafiri unazidi kushamiri na miongoni mwa watumiaji hao wanaelezea kwenye makala hii msingi wa matumizi, changamoto na nini kifanyike ili matumizi ya baiskeli yawe salama.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners