Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 08 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi makubwa ya kijeshi nchini Ukraine yaliyotekelezwa na Urusi, na miradi ya maji nchini Sudan Kusini. Makala inamulika biashara kwa wakulima, vijana na wanawake, na mashinani inatupeleka nchini Ethiopia, kulikoni?Nchini Ukraine Jumatatu ya leo Julai 8 imeanza na wimbi jingine la mashambulizi makubwa ya kijeshi yaliyotekelezwa na Urusi na kuua makumi ya watu, hospitali ya watoto ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa.Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Beth Bechdol amefanya ziara ya siku sita nchini Sudan Kusini na kuzindua miradi inayo saidia ukuaji wa kiuchumi huku ikipunguza migogoro na kuongeza uwezo wa wanachi kwenye kilimo.Katikamakala Assumpta Massoi akimulika mafunzo yaliyotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na wadau ili kuimarisha biashara kwa wakulima, vijana, wanawake na wasimamisi wa mashamba ya kuzalisha mbegu mkoani Kigoma, kaskazini magharibi mwa Tanzania.Mashinani tutakupeleka Tigray nchini Ethiopia katika shule ya msingi ya Siye kusikia jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiana na Muungano wa Ulaya lilivyoongeza kiwango cha uandikishaji na uhifadhi wa wanafunzi shuleni kupitia ukarabati wa madarasa na mpango wa mlo shuleni lakini kwanza ni makala.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Miradi ya maji yasaidia kupunguza migogo ya wafugaji nchini Sudan Kusini - FAO
    Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Beth Bechdol amefanya ziara ya siku sita nchini Sudan Kusini na kuzindua miradi inayo saidia ukuaji wa kiuchumi huku ikipunguza migogoro na kuongeza uwezo wa wanachi kwenye kilimo.Akiwa ameambatana na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Rukia Abdullahi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Sudan Kusini Onyoti Adigo na viongozi wengine wa ngazi za juu wa FAO, wametembekea maeneo mbalimbali ikiwemo mji wa Kapoeta ulioko jimboni Equatorial Mashariki unaokabiliwa na ukame ambapo mifugo ndio chanzo kikuu cha chakula na lishe na tegemeo la kuwaingizia kipato wananchi.Ziara ya Bi. Bechdol inakuwa wakati huu kukiwa na wasiwasi wa kuzorota kwa hali ya uhakika wa upatikanaji wa chakula kutokana na mafuriko yanayotarajiwa kuathiri nchi hiyo mwezi Septemba. Lakini kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika jumla ya dola milioni 44 zimewekezwa kwenye miundombinu ya uvunaji wa maji inayozingatia mabadiliko ya tabianchi (wananchi wa Kapoet wakiita Haffirs).Mradi huu umesaidia kupunguza migogoro na mivutano baina ya kaya za wafugaji iliyokuwa ikisababishwa na uhaba wa maji pamoja na kupunguza tabia za wafugaji kuhama hama kwani sasa zaidi ya kaya 13,000 zinanufaika kwa upatikanaji wa maji.Akiwa katika jijiji cha Riwoto huko Kapoeta Kaskazini Bi. Bechdol alizindua visima cha maji na kueleza kuwa, “Huu ni mfano kamili wa jinsi tunavyoshirikiana na serikali ya Sudan Kusini na washirika muhimu wa rasilimali kama Benki ya Maendeleo ya Afrika, na kuleta uwezo kamili wa uongozi wa FAO kwa watu wa Sudan Kusini.”Bi. Marta Nakwee mkulima kutoka Riwoto anashukuru kwa mradi huo kwani umebadilisha maisha yao.“Hapo awali nilikuwa naenda mbali sana kuteka maji ilikuwa ikinichukua sehemu kubwa ya siku yangu. Nililazimika kuwaacha watoto wangu wakiwa na njaa siku nzima na maranyingine waliugua lakini kwa sasa sina tatizo hilo tena.”Mbali na miradi ya maji FAO na washirika wake kujenga uwezo wa kustahimili hali ya maisha kwa kusaidia wananchi kuzalisha mbegu zao wenyewe kwa ajili ya kilimo, kujenga miundombinu, kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama, kutoa chakula chenye lishe bora kwa watoto mashuleni na kupunguza utegemezi wa misaada ya kibinadamu.
    2 min
  • DRC ni zaidi ya muziki, tutatumia Kiswahili kueneza utamaduni wetu - Balozi Ngay
    Kufuatia lugha ya Kiswahili kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kutengenewa siku maalum, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC sasa imesema itajengea uwezo wasanii wake wanaoimba kwa lugha ya Kiswahili kama njia mojawapo ya kusambaza utamaduni wa taifa hilo.Mwakilishi wa Kudumu wa DRC kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zénon Mukongo Ngay amesema hayo katika ujumbe wake kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.Ikumbukwe kuwa tarehe 1 Julai mwaka huu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kutangaza tarehe 7 Julai kuanzia mwaka huu kuwa siku ya Kiswahili dunia na kutaka nchi wanachama na wadau pamoja na mashirika kuchukua hatua kusongesha lugha hiyo ya 10 kwa kuwa na wazungumzaji wengi zaidi duniani, kwa mujibu wa UNESCO.Balozi Ngay kwenye ujumbe wake amesema DRC imefurahishwa na kitendo cha Kiswahili kutambulika katika kiwango cha kimataifa.DRC ni zaidi ya muziki, tutatumia kiswahili kueneza utamaduni wetu“Siku ya Julai 7 itabakia katika kumbukumbu. Kiswahili ni lugha itakayokuwa chombo cha biashara duniani kote, ni jambo la kujivunia,” amesema Balozi Ngay.Ametanabaisha kuwa DRC ni mashuhuri si katika muziki peke yake, akisema utamaduni wa DRC ni mkubwa, muziki ni kipengele kimoja tu cha utamaduni wetu.Amesema idadi kubwa ya wakongomani wanaoimba kwa lugha ya kiswahili wameingia kwenye injili na nyimbo zao nyingi zinatambulika kwenye sehemu ya eneo la Mashariki mwa Afrika.Tutahimiza matumizi ya Kiswahili kweney muziki wa kijamiiKwa kuzingatia uzito wa sasa wa Kiswahili, DRC pia itahimiza matumizi ya lugha hiyo katika kile kinachoitwa muziki wa kijamii.Balozi Ngay amesema watakachofanya wao sasa ni kukuza wasanii wanaoweza kuimba kwa lugha ya Kiswahili.Tarehe 1 Julai mwaka huu wa 2024 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio (A/78/L.83) la kutambua Julai 7 kuwa Siku ya Kimataifa ya Kiswahili.Awali siku hii ilikuwa inatambuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kupitia azimio lililopitishwa mwezi Novemba mwaka 2021.
    3 min
  • Machungu yakumbayo wahamiaji na wakimbizi njia za ardhini ni makubwa kuliko baharini Mediteranea
    Ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yabaini kuwa wahamiaji na wakimbizi wanaotaka kuelekea Ulaya kusaka maisha bora kupitia njia za ardhini Afrika, wanakumbwa na ukatili sio tu wanapokuwa baharini, bali pia ardhini wanapokatiza nchi zingine kuelekea fukwe za bahari ya Mediteranea. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Ikipatiwa jina Katika safari hii hakuna anayejali unaishi au unakufa, ripoti imeandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na la wahamiaji, IOM kwa ushirikiano na lile la Kimataifa la Wahamiaji Mseto (MMC).Ripoti inasema wakimbizi na wahamiaji wanazidi kupita maeneo ya ardhini ambako makundi ya waasi, wanamgambo na wahalifu wengine wanafanya kazi, na ambapo biashara haramu ya binadamu, utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi, utumikishwaji kwenye kazi na ukatili wa kingono umeenea.Hayo yanatokea wakati inakadiriwa kuwa watu wengi huvuka zaidi kulekea Ulaya kupitia jangwa la Sahara kuliko bahari ya Mediterania huku vifo vya wakimbizi na wahamiaji jangwani vikidhaniwa kuwa ni maradufu zaidi ya vile vinavyotokea kwa wanaovuka kupitia bahari ya Mediterania huku ikionya juu ya ongezeko kubwa la watu wanaojaribu kuvuka eneo hilo hatari.Licha ya ahadi zinazofanywa na Jumuiya ya Kimataifa kuokoa maisha na kushughulikia udhaifu unaondelea, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, mashirika hayo matatu yanaonya kwamba hatua za sasa za Kimataifa hazitoshi kutokana na mapungufu makubwa kwenye ulinzi katika njia ya kati ya Mediterania.Yanachotaka sasa mashirika hayo ni ulinzi mahsusi kulingana na njia wanazotumia wakimbizi na wahamiaji ili kuokoa maisha, kupunguza machungu na kung’oa mzizi wa kile kinachosababisha watu kukimbia nchi zao kwa kusaka mbinu bora za ujenzi wa amani. 
    2 min
  • 05 JULAI 2024
    Hii leo kwenye jarida mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akimulika shamrashamra za Kiswahili, wakimbizi na wahamiaji na mateso njiani Afrika, mafunzo kwa wataalamu wa mifugo Tanzania na harakati za OCHA Sudan kusaidia wahitaji.Wadau wa Kiswahili duniani kote wakiendelea na shamrashamra baada ya Umoja wa Mataifa kutambua lugha hiyo kuwa ya kimataifa na hadi kutengewa tarehe 7 Julai kuwa siku maalum kusherehehea siku hiyo, Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zénon Mukongo Ngay naye ametoa ujumbe wake.Ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yabaini kuwa wahamiaji na wakimbizi wanaotaka kuelekea Ulaya kusaka maisha bora kupitia njia za ardhini Afrika, wanakumbwa na ukatili sio tu wanapokuwa baharini, bali pia ardhini wanapokatiza nchi zingine kuelekea fukwe za bahari ya Mediteranea. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Makala inatupeleka nchini Tanzania ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili ya Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo (USAID), limehitimisha awamu ya nne ya mafunzo kwa maafisa mifugo 30 wa serikali ya Tanzania, yatakayowawezesha kutambua na kutibu magonjwa ya mifugo ili kuboresha ufugaji wenye tija na kulinda soko la Mifugo kimataifa. Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM ya Morogoro, amehudhuria shughuli ya uhitimishaji wa mafunzo hayo na kuandaa makala inayoanza na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanzania, Profesa Riziki Shemdoe.Mashinani Clementine Nkweta-Salami ambaye ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa kwa Misaada ya kibinadamu nchini Sudan akitueleza jinsi changamoto ya usalama wa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu inavyokwamisha ufikishaji wa misaada kwa wahitaji.
    10 min
  • FAO Tanzania na USAID wafanikisha mafunzo kwa Maafisa Mifugo Tanzania
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili ya Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo (USAID), limehitimisha awamu ya nne ya mafunzo kwa Maafisa Mifugo 30 wa serikali ya Tanzania, yatakayowawezesha kutambua na kutibu magonjwa ya mifugo ili kuboresha ufugaji wenye tija na kulinda soko la Mifugo kimataifa. Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM ya Morogoro, amehudhuria shughuli ya uhitimishaji wa mafunzo hayo na kuandaa makala inayoanza na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanzania, Profesa Riziki Shemdoe.
    4 min
  • 03 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia tunaangazia maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa. Makala tunatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili, na mashinani tunakupeleka nchini China kusikia ujumbe wa mdau kuhusu lugha y aKiswahili.Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Maadhimisho haya yanafanyika tarehe 3 kwa kuwa siku yenyewe ya Kiswahili duniani yaani tarehe 7 Julai itaangukia siku ya Jumapili na Anold Kayanda anafuatilia kwenye maadhimisho hayo.Tukiendlea na maadhimisho ya Siku ya Kiswahili duniani mwenzetu Assumpta Massoi naye anafuatilia maadhimisho hayo na ametuandalia taarifa pamoja na mazungumzo yake na aliyehudhuria maadhimisho hayo.Katika makala Bosco Cosmas anatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili.Na katika mashinani Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili inaadhimishwa Jumapili Julai 7, Masika Yang, Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) anatoa ujumbe kuhusu lugha ya Kiswahili.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 
    10 min
  • Umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili nchini Ghana
    Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili.Maadhimisho haya yanafanyika tarehe 3 kwa kuwa siku yenyewe ya Kiswahili duniani yaani tarehe 7 Julai itaangukia siku ya Jumapili. Katika makala hii Bosco Cosmas anatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili.
    4 min
  • 02 JULAI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia tukio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Julai Mosi la kuidhinisha tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani kama zifutazo…Huko Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA linasema wiki chache tu baada ya jeshi la Israeli kulazimisha watu kurejea mji wa Khan Younis ulioharibiwa, leo hii mamlaka za Israeli zimetoa amri mpya ya kuhama kutoka eneo hilo licha ya kwamba hakuna pahala paliko salama Ukanda wa Gaza. Watu 250,000 watalazimika kuhama tena.Nchini Sudan vita ikiendelea kurindima, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeziongeza Libya na Uganda kama nchi zinazopokea wakimbizi kutoka Sudan na hivyo kufanya nchi zinazowapokea kufikia saba zikiwemo Libya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Chad na Ethiopia, na sasa linahitaji fedha dola bilioni 1.5 badala ya dola bilioni 1.4 iliyotangazwa awali.Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Bruno Lemarquis, amelaani vikali shambulio la tarehe 30 Juni mwaka huu dhidi ya msafara wa shehena za misaada ya kiutu huko Butembo jimboni Kivu Kaskazini, shambulio lililosababisha vifo vya wahudumu wawili wa misaada ya kibinadamu. Bwana Lemarquis ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki za watumishi hao.Na katika mashinani tutamsikia Estelle Zadra wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni (UNESCO) akieleza mikakati yao katika kukuza lugha ya Kiswahili duniani.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • Hizi ndizo shughuli zetu CIMIC ya TANBAT 7 - Kapteni John Zablon Mashamy
    Kutokana na hali tete ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa kwa miaka mingi umekuwa ukifanya juhudi za kuleta amani na kuilinda kwa kutuma ujumbe wake, MINUSCA ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa huchangia vikosi mbalimbali. Kikosi cha 7 kutoka Tanzania, TANBAT 7 ni miongoni mwa walinda amani waliko huko, hususani wakihudumu katika eneo la Berbérati, magharibi mwa nchi.Kupitia makala hii, Afisa uhusiano wa TABAT 7, Kapteni John Zablon Mshamy anaeleza shughuli zinazofanywa na kitengo cha uhusiano, CIMIC anachokiongoza.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners