Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 22 SEPTEMBA 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mabadiliko ya tabianchi hayawaathiri watu wote kwa kiwango sawa. 

    Baadhi ya nchi zimejenga uchumi wao kwa miongo kadhaa kupitia matumizi makubwa ya nishati ya mafuta, huku nyingine zilizochangia kidogo katika uzalishaji wa gesi chafu zikikabiliwa na mafuriko, vimbunga, ukame, ongezeko la kina cha bahari na kupotea kwa njia za kujipatia riziki. 

    Hili ndilo kiini cha mjadala kuhusu haki na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ambao utafanyika kesho Jumatano . Lakini haki hiyo ina maana gani? Nani anapaswa kubeba gharama? Na kizazi kijacho kitaachiwa dunia ya aina gani?

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefungua pazia asubuhi ya leo saa za New York, Marekani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antono Guterres kupitia hotuba yake ambayo ni ya mwisho katika tukio hili amegusa mambo mengi miongoni likiwa kuhusu ushauri wake kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya mageuzi katika Baraza la Usalama ili liakisi hali halisi ya ulimwengu wa leo na kuwa na uhalali pamoja na ufanisi unaohitajika kukabiliana na changamoto za sasa.
    2. Tuondoke hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, ambako viongozi wa ulimwengu sasa wanaendelea kutoa hotuba zao nakupeleka mashinani hususan Nairobi, Kenya kusikia vijana wanataka nini.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

    12 min
  • Balozi Thigo: Kuwalinda watoto zama za AI na teknolojia ni muhimu sana

    Kesho Jumanne tarehe 22 Septemba mbali ya kufunguliwa kwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Matanfa wa UNGA81, kandoni mwa mjadala huo kutakuwa na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. Balozi Philip Thigo anayehusika na masuala ya AI kutoka Kenya ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo amenieleza kwa nini suala hili ni muhimu katika mkutano wa kesho na nini wanakitarajia

    3 min
  • 21 SEPTEMBA 2026

    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu na vijana kuhusu siku ya amani, ufunguzi wa UNGA81, Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni.

    1. Leo ni siku ya amani duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amepongeza watu wote mashinani wakiwemo watumishi wa kujitolea, wachechemuzi na viongozi wa mashirika ya kiraia wanaojitolea kwa hali na mali kuendeleza amani.
    2. Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataofa UNGA81 unafungua pazia kesho Jumanne ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa kwa kina na nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa ikiwemo kuwasilisha tarifa zao
    3. Kesho Jumanne tarehe 22 Septemba mbali ya kufunguliwa kwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Matanfa wa UNGA81, kandoni mwa mjadala huo kutakuwa na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. Balozi Philip Thigo anayehusika na masuala ya AI kutoka Kenya ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo amenieleza kwa nini suala hili ni muhimu katika mkutano wa kesho na nini wanakitarajia.

    Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

    10 min
  • Siku ya amani duniani, vijana wapaza sauti zao

    Leo ni siku ya amani duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amepongeza watu wote mashinani wakiwemo watumishi wa kujitolea, wachechemuzi na  viongozi wa mashirika ya kiraia wanaojitolea kwa hali na mali kuendeleza amani.

    3 min
  • 18 SEPTEMBA 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DR Congo kufuatilia mapambano dhidi ya ebola ambayo yameanza kupata matumaini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.

    1. Mlipuko wa sasa wa 17 wa Ebola wa virusi vya Bundibugyo huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umegharimu zaidi wanawake na wasicha kwa kuwa wengi wao wako mstari wa mbele kuhudumia wagonjwa na familia zao licha ya hatari kubwa ya kuambukizwa. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva, Uswisi, kwa njia ya mtandao kutoka Kinshasa DRC, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, (UN Women) nchini humo, Dkt. Setcheme Mongbo, amesema.  “Wanawake na wasichana huosha miili ya marehemu na kushiriki katika shughuli nyingine za mazishi, wao ndio wanaokusanya na kutoa maji na chakula kwa wanafamilia. Na suala la utoaji wa huduma hizo ni muhimu sana katika mnyororo mzima wa maambukizi linapokuja suala la Ebola.”
    2. Kumekuwa na ripoti za kushtusha za  dhidi ya raia na wafungwa wa kivita wakati huu kukiwa na mashambulizi kamili ya kijeshi yanayofanywa na jeshi la Urusi huko Kyiv nchini Ukraine. Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu Shabia Mantoo amewaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo kuwa. “Zaidi ya wagonjwa 1,000 wamerekodiwa na wafanyakazi wetu wa Kamati ya wa Ufuatiliaji wa Haki za Binadamu kuanzia tarehe 24 Februari 2022 hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk ana wasiwasi mkubwa kwamba vitendo hivyo vya kuchukiza vinaendelea karibu katikati ya vurugu zisizoisha, na anahimiza vikomeshwe mara moja. Pia anatoa wito wa uchunguzi wa haraka, wa kina, na usio na upendeleo kuhusu madai yote ya unyanyasaji wa kingono, na kwa wale watakaopatikana na hatia wafikishwe mbele ya sheria.”
    3. Na, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeonya kuwa msaada wa dharura unaotolewa kupitia mfumo wake wa pamoja wa kibinadamu nchini Sudan unaweza kuisha ndani ya wiki mbili zijazo kutokana na ukosefu wa fedha. IOM inasema inahitaji dola milioni 15 kuendeleza operesheni hiyo kwa kiwango cha chini kwa miezi 12, wakati watu milioni 8.6 bado wakiwa wakimbizi wa ndani nchini Sudan.

    Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

    10 min
  • 17 SEPTEMBA 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda nchini Kenya ambako Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imetoa tahadhari ya kwamba taifa hilo la Afrika Mashariki litakabiliwa El Nino kuanzia mwezi ujao wa Oktoba hadi Desemba mwaka huu wa 2026. 

    El Nino huweze kusababisha mvua kubwa na kwingineko ukame mkali. Kufuatia onyo hilo, tayari shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) kwa kushirikiana na serikali wameanza kuchukua hatua za mapema ili kuepusha madhara makubwa. Sasa nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii, kupitia mahojiano yaliyofanywa na Mercy Korir, mwanafunzi wa vitendo kwenye kituo cha huduma za Habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya, UNIS, ameandaa mada hii kwa kina. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Dunia inaingia katika kipindi ambacho upatikanaji usiotabirika wa maji unazidi kuwa kawaida, imeonya leo ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO. Ripoti hiyo inasema mwaka 2025 ulikuwa miongoni mwa miaka yenye mtiririko mdogo zaidi wa mito katika miongo mitatu na nusu. Katibu Mkuu wa WMO, Celeste Saulo, amesema hali hiyo ni ishara inayoendelea kwa muongo mmoja. Akisistiza hilo Wayne Jenkinson, Mkurugenzi, Kitengo cha Hidrologia WMO anasema, “Mara nyingi maji hayapatikani mahali tunapoyahitaji, wala wakati tunapoyahitaji.”
    2. Zaidi ya watoto 57,000 wameyakimbia makazi yao nchini Yemen katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kutokana na mapigano mapya, huku wengine wakiuawa, kujeruhiwa au kutoweka. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF linaonya kuwa vurugu hizo zinazidisha janga la kibinadamu katika nchi ambako zaidi ya watoto milioni 12 wanategemea misaada baada ya zaidi ya muongo mmoja wa mzozo. Msemaji wa UNICE Joe English amesema watoto wengi nchini Yemen hawajui maisha mengine isipokuwa mzozo na kuhama kutoka kwenye makazi yao. Na kwamba “Hawa ni watoto ambao tayari wamepitia miaka ya njaa, kufurushwa makwao na migogoro, na sasa wanalazimishwa kuondoka tena katika makazi yao”.
    3. Na Wanawake duniani kote bado wanapata kwa wastani asilimia 20 chini ya wanaume, licha ya juhudi za muda mrefu za kukuza usawa kazini. Katika Siku ya Kimataifa ya Usawa wa Mishahara, Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Kazi Duniani (ILO) na la masuala ya Wanawake UN Women yanasema pengo hilo si jambo lisiloepukika, na yanataka hatua kuhakikisha wanawake wanalipwa sawa kwa kazi zenye thamani sawa. ILO inasema “Usawa wa mishahara ni suala la haki, kanuni, utu na usawa wa kijamii – kwa kila mfanyakazi, kila mahali”  wakati UN Women ikisisitiza kuwa “Usawa wa mishahara si suala la haki pekee; unaimarisha familia, uchumi na jamii.” Mashirika hayo yanasema sasa kinachohitajika ni hatua za kubadili ahadi za usawa wa mishahara kuwa uhalisia.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

    12 min
  • 16 SEPTEMBA 2026

    Hii leo jaridani tunaangazia uokoaji Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi, ushirikiano na Umoja wa Mataifa, na chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi nchini Burundi.

    1. Hofu na majonzi vimetanda Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 100, wakiwemo watoto 50, walikuwa wakiishi katika jengo hilo wakati lilipoanguka. Operesheni za uokoaji zinaendelea, huku Umoja wa Mataifa ukisema kila dakika ni muhimu katika kujaribu kuokoa maisha.
    2. Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kuhusu kuongezeka kwa vitisho, kulipiza visasi na ufuatiliaji wa kidijitali unaovuka mipaka dhidi ya watu na wadau yanayoshirikiana na mfumo wake unaohusiana na masuala ya haki za binadamu. Kufahamu kwa kina kilichomo kwenye ripoti hyo nimezungumza na Selina Jerobon ambaye amefuatilia kwa kina.
    3. Hivi karibuni, Burundi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, pamoja na wadau wengine, imezindua mpango wa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, mpango unaolenga kuwachanja wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi 14

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

8 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

10 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners