Makala hii imeangazia hali inayoendelea huko mashariki mwa DRC ambapo hivi karibuni maelfu ya raia kwenye mji wa Goma, waliandamana kupinga uwepo wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanavyosema vimeshindwa kuwadhibiti waasi wa M23, ni maandamano ambayo yalifanyika siku chache baada ya viongozi wa Jumuia ya EAC kukutana jijini Bujumbura Burundi ambapo waliwataka waasi kusitisha mapigano, kuheshimisha mkataba wa Luanda unaowataka kuondoka katika maeneo wanayoyashikilia, wakati huu kundi hilo likiripotiwa kuchukua miji zaidi.