Jukwaa la Michezo

Jukwaa la Michezo

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Jukwaa la Michezo episodes

  • CAF: Ligi ya klabu bingwa barani Afrika 2024 kwa kina dada yaanza nchini Morocco

    Tumeangazia klabu ya Chaux Sport kutoka DRC kubanduliwa kwenye mechi za kufuzu Ligi ya Basketboli Afrika 2024, masaibu ya Yanga SC nchini Tanzania, uchaguzi wa FKF nchini Kenya, mashindano ya kuendesha baiskeli Afrika kwa kina dada nchini Burundi, kifo cha rais wa soka nchini Algeria, matokeo na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya na fainali ya tenisi kwenye mashindano ya WTA

    24 min
  • Senegal kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki ya kwanza kabisa Afrika, 2026

    Tuliyokuandalia ni pamoja na bodi mpya ya uchaguzi wa shirikisho la soka nchini DRC, waziri wa michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro abainisha viwanja 20 kwa ajili ya AFCON 2027, timu ya REG nchini Rwanda yafuzu Ligi ya Basketboli Afrika 2024 kwa kina dada, mechi za kufuzu CHAN 2025, hatma ya kocha wa Rwanda Torsten Spittler, Senegal kuandaa michezo ya Olimpiki ya kwanza barani Afrika ya chipukizi mwaka 2026, kocha mpya wa Man Utd, mashindano ya Paris Masters na Brazilian GP

    Afrika inatarajia michezo ya kwanza ya Olimpiki ya vijana itakayoandaliwa barani Afrika mwaka 2026, jijini Dakar, mji mkuu wa Senegal.

    Michezo hiyo imepangwa kufanyika kati ya Oktoba 31 na Novemba 13, 2026, tukio ambalo litaleta pamoja wanariadha bora zaidi ulimwenguni kushiriki katika michezo 35 tofauti kwa siku 14.

    Tamasha la Dakar en Jeux (Dakar in Games) lilipangwa awali kwa kipindi cha Dakar 2022, katika miji mitatu ya mwenyeji wa Dakar, Diamniadio, na Saly.

    Tangu wakati huo, Dakar en Jeux imekuwa sherehe ya kila mwaka ya michezo na utamaduni, ikihudumu kama mtangulizi wa Dakar 2026 wakati ikihimiza kuongezeka kwa ushiriki wa vijana katika michezo.

    Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach ameripotiwa kuunga mkono Senegal kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Vijana, akibainisha umoja wa Afrika na utamaduni wake wa michezo.

    "Kwa idadi ya vijana na shauku ya michezo, ni wakati wa Afrika, ni wakati wa Senegal," alisema katika ripoti ya olympics.com.

    "Hatuwezi kusubiri muda urudi hapa na kufurahia tukio hili la kwanza la Olimpiki katika ardhi ya Afrika, ambalo litawakaribisha vijana wa dunia nchini Senegal." Bach alitoa matamshi hayo wakati wa ziara yake nchini Senegal mwaka 2022, akifichua matarajio yake ya tukio hilo.

    Wachambuzi wa michezo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika wanachukulia tukio hilo kuwa la kihistoria huku Rufai Shuaib kutoka Senegal akisema;

    "Kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Vijana huko Dakar inawakilisha hatua kubwa katika kuonyesha talanta kubwa na uwezo wa wanariadha wetu wachanga kwenye jukwaa la kimataifa," alisema.

    Taarifa ya ziada: Olympics

    24 min
  • Nitawania tena urais wa CAF mwaka 2025, amethibitisha Dkt Patrice Motsepe

    Tuliyokuandalia ni pamoja na taarifa ya Rais wa CAF Patrice Motsepe kuwania tena urais muhula wa pili, hukumu ya CAF katika mechi ya Nigeria dhidi ya Libya, yaliyotukia kwenye ziara ya rais wa Olimpiki ya kimataifa nchini Kenya na Kongamano la tatu la kibiashara la soka Afrika, uchambuzi wa michuano ya Kombe la Dunia la kina dada U17, Senegal ikihifadhi ubingwa wa Afrika soka ya ufukweni, michuano ya ndondi Afrika jijini Kinshasa, PSG kumlipa Mbappe €55M na uchambuzi wa El Clasico leo usiku.

    24 min
  • Tanzania na Kenya zafuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika U20 mwaka ujao

    Tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya kufuzu AFCON U20 mwaka ujao, namna timu za Afrika zilicheza kwenye wiki ya kwanza ya Kombe la Dunia la kina dada wasiozidi miaka 17, timu ambazo tayari zimefuzu AFCON ya 2025 nchini Morocco na nafasi ya timu za Afrika Mashariki na Kati, AFCON ya ufukweni yaanza leo nchini Misri, droo ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, mashindano ya magari ya Rwanda Mountain Gorilla Rally, kutimuliwa kwa kocha Kavazovich klabuni Vipers na Ligi za ukanda na Ulaya

    25 min
  • AFCON U20: DRC yafuzu Kombe La Mataifa Ya Afrika ya mwaka ujao

    Tuliyokuandalia ni pamoja na faniali za kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20, uchambuzi wa vikosi vilivyotajwa na wakufunzi kuelekea raundi ya tatu ya kufuzu AFCON 2025, masaibu ya Samuel Eto'o na kocha wa Senegal Aliou Cisse kutemwa, kifo cha nyota wa basketboli Dikembe Mutombo pamoja na matokeo ya mechi za ligi ya mabingwa ulaya.

    25 min
  • Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano ya juu zaidi ya baiskeli barani Afrika

    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa mechi ya Kombe la Super Cup Afrika, Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano ya baiskeli Afrika kwa mara ya kwanza, matokeo ya riadha jijini New York, sura mpya za wanariadha watakaoshiriki Berlin Marathon hapo kesho, Ligi za ukanda kwenye soka, voliboli na basketboli lakini pia matokeo ya Kombe la Europa League raundi ya kwanza.

    25 min
  • CHAN 2024 kuanza Februari 1-28 mwaka 2025 nchini Uganda, Kenya na Tanzania

    Tuliyokuandalia ni pamoja na taarifa ya ziara ya rais wa CAF Patrice Motsepe nchini Kenya, awamu ya pili kufuzu hatua ya makundi mechi za klabu bingwa Afrika, timu za Kenya za soka na mchezo wa Kabaddi tayari kushiriki Kombe la Dunia, timu za taifa Afrika Mashariki zimepanda kwenye msimamo wa dunia wa FIFA, uchambuzi wa raundi ya kwanza mechi za UEFA na mchezo wa ndondi kati ya Anthony Joshua na Daniel Dubois leo usiku.

    25 min
  • Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei azikwa kwa heshima kamili za kijeshi

    Tuliyokuandalia hii leo ni mkusanyiko wa uchambuzi na matokeo ya mechi za kufuzu AFCON 2025, mechi za klabu bingwa Afrika kufuzu awamu ya makundi, washindi wa riadha za Diamond League, matokeo ya lLigi ya basketboli ya Afrika U18, droo ya AFCON U20 ukanda wa CECAFA, ligi za ukanda na ulaya pamoja na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya msimu mpya utakaoanza wiki ijayo

    24 min
  • AFCON 2025: Safari ya kuelekea Morocco yaanza kwa mataifa ya Afrika

    Tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo na uchambuzi wa mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, kifo cha mwanariadha wa Uganda nchini Kenya, matokeo ya Zurich Diamond League, matokeo ya U18 Afrobasket na Congo Cup, uchambuzi wa matokeo ya  mataifa ya Afrika kwenye Olimpiki ya walemavu jijini Paris, mechi za Ligi ya Mataifa ya Ulaya na tuzo za Ballon D'Or mwaka 2024

    25 min

About Jukwaa la Michezo

From the publisher's feed

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano…

More shows like Jukwaa la Michezo

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners