Makala ya wimbi la siasa hii leo inaangazia hali ya kamata kamata inayotekelezwa na vyombo vya usalama dhidi ya wapinzani kwenye mataifa kadhaa ya Afrika mfano huko DRC Salomon Idi Kalonda mshauri wa kisiasa wake Moise Katumbi, hali kama hiyo inashuhudiwa pia huko Burundi katika chama cha upinzani cha CNL, Nchini Senegal huko na Kinara wa Upinzani Ousmane Sonko alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kufuatia tuhuma za ubakaji. Mwandishi wetu Reuben Lukumbuka amewaalika Mali Ali ni mchambuzi wa siasa za Nchi za maziwa makuu akiwa Visiwani Mayotte na pia Francois Alwende ni mchambuzi na mataalamu wa siasa za DRC akiwa Jijini Nairobi nchini Kenya