Katika Makala haya Mtangazaji wako Ali Bilali wa idhaa ya Kiswahili ya RFI amezungumza na kina Mama kutoka kundi la Warumba wa Nyakanga, ambao hutoa burudani ya kuimba kwa kutumia ngoma maharufu "Msondo" huku wakitoa pia somo la mafunzo ya kumfunda mwali katika utamaduni wa waswahili wa Buyenzi. Na kwenye Muziki utampata Kijana Khalid msanii wa miondoko ya Taarab kutoka nchini Burundi mwenye lengo la kuinua muziki huo nchini Burundi.