Makala hii imejikita katika Mji wa Mombasa pwani ya Kenya kuangazia maendeleo ya muziki wa HipHop na msanii Fikra Teule ambaye katika siku za hivi karibuni aliitoa video yake mpya na sauti inayofahamika kwa jina la SEMA YOTE akiwa amemshirikisha msanii mpya katika tasnia ya muziki anayefahamika kwa jina la Victoria Gichora, ambapo uzinduzi rasmi wa video yake ulifanyika katika kituo cha utamaduni wa Ufaransa Alliance Francaise ya Mombasa na aliwashirikisha wasanii wenzake wa Hip Hop Ohms Law Montana, Azma Mponda na Mwimbaji Babs kutoka Tanzania.
Fikra Teule alizitembelea studio zetu maridadi hapa RFI Kiswahili na kuhojiwa na mwandishi wetu mwandamizi Reuben Lukumbuka..