Katika makala wimbi la siasa tunaangazia hisia mseto zinazoenea kwenye eneo la ukanda wa nchi za maziwa makuu, baada ya mwishoni mwa juma lililopita, wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya SADC waliokutana mjini Luanda, Angola, kushindwa kutoa terehe kamili ya vikosi vyake kupelekwa mashariki mwa DRC. Aidha, viongozi wa SADC walikubaliana kumpa muda zaidi rais wa Angola, Joao Lourenco, kuendelea na juhudi za upatanishi kati ya nchi ya DRC na Rwanda. Mwandishi wetu George Ajowi anazungumza na Haji Kaburu akiwa Tanzania na Guershome Kahebe akiwa Marekani..