Karibu kuungana nami jumapili hii katika Makala haya Changu Chako Chako Changu ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu mwezi wa Francophonie na kwenye le parler francophone nakuletea shughuli za kitamaduni zilizojiri kwenye vituo vya Alliance Francaise ya Mombasa, Nairobi na Dar es salaam na kwenye Muziki nakuletea mwanamuziki kutoka nchini Burundi Saidi Brazza ambae amefariki dunia alhamisi iliopita huko Ngozi magharibi mwa Burundi. Mimi naitwa Ali Bilali bienvenue.