Makala ya Wimbi la siasa imeaangazia kauli ya viongozi wa EAC waliokutana huko Addis Ababa Ethiopia walithibitisha kuunga mkono michakato ya Luanda na Nairobi ambayo inawataka waasi wa M23 Huko DRC kusitisha mapigano na kuondoka katika maeneo wanayoyashikilia, katika sehemu ya pili viongozi wa Afrika walisisitiza msimamo wao wa kutovumilia njia zisizo za kidemokrasia, kuchukua madaraka wakijadili hali ya mapinduzi ya kijeshi kule Burkina Faso, Guinea, Mali na Sudan..Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka akiwa na wageni wake: Francois Alwende, mchambuzi wa siasa akiwa Nairobi nchini Kenya, pia Hajji Kaburu mchambuzi akiwa Dar Es Salaam Nchini Tanzania