Leo tunaangazia juu ya hatua ya serikali ya Burundi kusimamisha baadhi ya viongozi na maafisa waandamizi wa serikali iliyoko madarakani wengi wao wakiwa watumishi wa ikulu. Serikali ya Burundi ilifahamisha kwamba waliosimamishwa kazi akiwemo aliyewahi kuwa msemaji wa serikali Willy Nyamitwe na wengine, wamesimamishwa kupisha uchunguzi kwa tuhuma za kuchelewa kazini.
Leo tunaangazia juu ya Kinywaji haramu cha ‘Gongo’ nchiniTanzania na ‘Chang’aa’ nchini Kenya. Baadhi ya wanywaji wa pande zote walioongea na RFI wanaomba serikali za nchi zao kuhalalisha kinywaji hicho cha Gondo ambapo kwa Kenya wao huiita Chang’aa, na kwa upande wa Tanzania huiita Gongo au Supu ya Mawe au Machozi ya Simba na kadhalika.
Leo tunaangazia juu ya Maadili ya Viongozi wa Umma nchini Tanzania. Tutakuwa na baadhi ya wachambuzi ambao ni Ndugu Mjungu akiwa Karagwe mkoani Kagera, pamoja na Dokta. Peter Bujari mchambuzi wa kisiasa, kiuchumi na mshauri wa sera akiwa jijini Dar es Salaam.
Tunaangazia juu ya hatua ya Serikali ya Burundi kupitia upya mikataba ya madini lengo ikiwa ni madini ya nchi hiyo kunufaisha pande zote yaani Burundi na muwekezaji. KWa mjibu wa serikali ya Burundi, kwa sasa taifa hilo linanufaika na pato la madini aslimia 10% -15% na Burundi ingependa kiwango zaidi.
Leo tunaangazia juu ya utamaduni wa kuandika na kusoma vitabu nchini Tanzania. RFI imefika jijini Dar es Salaam kukutana na waandishi wa vitabu Bw. Yerick Nyerere pamoja na Dr. Cyrilo Christopher ambao wamejitahidi saana kuandika vitabu na kuhamasisha usomaji vitabu nchini Tanzania.
Leo tunaangazia juu ya changamoto ya ajira kwa Vijana wa nchi za Afrika ya Mashariki, na leo tunaungana na baadhi ya vijana wa Kenya na Tanzania. Baadhi ya vijana hao wanabainisha kuwa juhudi na bidii ndio njia muafaka ya vijana kufikia ndoto zao. Vijana wanashauri vijana wenzao kutumia elimu na vipaji ili kujiinua kiuchumi.
Leo tunaangazia juu ya changamoto ya Vijana na wataalamu wa nchi za Afrika ya Mashariki wanaofikiria kupata fursa zaidi za ajira na kipato nje ya nchi zao na bara la Afrika.
Tunaangazia juu ya Mkoa wa Kigoma, nchini Tanzania. Mkoa wa Kigoma uko magharibi mwa Tanzania, kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika, ambapo Tanzania inapakana nan chi za Burundi, Jamhuri yakidemokrasia ya Congo, na Zambia.
Tunaangazia juu ya vipaji kwa vijana nchini Tanzania. RFI imefika tarafani Rulenge, Wilayani Ngara, mkoani Kagera magharibi mwa Tanzania na kuongea na baadhi tu ya vijana walioamua kuunda kukindi cha ‘JM Group’ kuendeleza vipaji vyao, na shughuli zao za vipaji kuwa ajiri, kuwaimarisha kiafya na kudumisha mila na tamaduni.
Sekta ya elimu nchini Tanzania, inashuhudia changamoto hasa wilayani Ngara, mkoani
Kagera magharibi, ikibainika kwamba walimu wanawalazimisha wanafunzi wachote maji na kuchanja kuni
wakati wa muda wa masomo.
Juliani Rubavu anazamia hili kwenye makala haya.
10 min
About Afrika Ya Mashariki
From the publisher's feed
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani…
unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.