Leo tunaangazia juu ya fursa na ajira kwa vijana nchini Tanzania. Utawasikia vijana wa huko wilayani Rorya mkoani Mara kaskazini-magharibi mwa Tanzania jirani kabisa na mpaka wa Kenya. Kama utakavosikia kwenye mazungumzo yetu, vijana hao wanabainisha ni jinsi gani wameamua kubuni jinsi ya kujipatia kipato kwa njia ya burudani.
Julian Rubavu anaangazia juu ya uhaba wa dagaa wapatikana katika ziwaTanganyika hukoKigoma, Tanzania.
Wenyeji wanasema kuwa dagaa wa Kigomani watamu saana, lakini pia gharama za kuwavua dagaa hao ni kubwa sanaambapo mvuvi anatumia zaidi ya shilingi laki moja na elfu ishirini(120,000). Wenyeji wanasema kuwa sababu nyingine ni zana duni zauvuvi.
Katika makala haya mwanahabari Juliani Rubavu amezuru mwambao wa ziwa Tanyingika, katika kijiji na Ujiji, na kutangamana na wenyeji ambapo ameangazia kwa kina shughuli zao za kila siku.
Katika makala ya juma hili ya Afrika Mashariki, mawanahabari wetu Juliani Rubavu anaangazia hutua ya mataifa ya Afrika mashariki kuwashauri wataalamu wao kutoondoka katika mataifa hayo kutafuta kipato katika mataifa mengine kwa lengo la kuchangia kuimarika kwa uchumi katika mataifa yao.
Leo tunaangazia makubaliano ya viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokutana hivi karibuni jijini Dar es salaam nchini Tanzania na kuidhinisha rasmi Elimu ya juu ya pamoja ndani ya nchi wanachama. Hii inamaanisha nini ? Karibu sana.
Makala haya ya Afrika ya Mashariki inaangazia juu ya hofu kwa familia zenye watu wenye ulemavu wa ngozi na jamii inayowazunguka magharibi mwa Tanzania.
Makala haya ya Afrika ya Mashariki inaangazia juu ya changamoto za kiuchumi na maendeleo kwenye ukanda wa afrika ya mashariki. Katika makala haya watasikika baadhi ya raia wa Tanzania waishio maeneo ya mpakani, na pia mahojiano na waziri wa Tanzania kwenye jumuiya ya afrika ya mashariki Dr Harrison Mwakyembe akiangazia baadhi ya changamoto kwenye miradi ya kikanda inayoshirikisha jumuiya ya afrika ya mashariki.
Makala haya ya Afrika ya Mashariki yanaangazia juu ya changamoto za mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino), ambayo yamekithiri katika kanda ya ziwa Magharibi mwa Tanzania.
10 min
About Afrika Ya Mashariki
From the publisher's feed
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani…
unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.