
Sign up to save your podcasts
Or


Katika makala haya tunajadili iwapo mila za kiafrica zimeanza kuweka na namna gani zinaweza kudumishwa.
Skiza makalaa
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakuapa fursa kuchangia mada yoyote ile.
Skiza maoni ya juma hili.
DRC imejikatia tiketi ya kucheza kwenye kupute cha kuwania kombe la dunia
Haya hapa maoni ya waskilizaji.
Ripoti ya shirika la Amnesty Interenational imeonya kuwa Kombe la Dunia la mwaka huu linaweza kuchangia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dunaini kutokana mpango wa mataifa wenyeji kuweka mikakati kali za uhamiaji na ufuatiliaji wa karibu wa mashabiki wa kigeni
Je, unahisi mashabiki kutoka Afrika Mashariki watakuwa salama kushabikia timu zao kule Merekani,Mexico na Canada?
Skiza maoni ya waskilizaji.
Katika makala haya tunajadili hatua ya jiji la Kampala nchini Uganda kutatangaza makataa ya siku 20 kwa wamiliki wa magari ya usafiri wa uma kuondoa magari yaliyochakaa barabarani, mamlaka zikisema lengo ni kupunguza ajali na uchafuzi wa hali ya hewa mjini.
Tunakuuliza, nchi nyingine za Afrika mashariki zinapaswa kuiga mpango huu?
Skiza maoni ya waskilizaji hapa.
Katika makala haya tunaangazia haki za wafanyibiashara katika soko la Gikomba nchini Kenya.
Kwa muda wafanyibiashara hao wamekuwa wakizozana na serikali kuhusu kipande cha ardhi cha soko hiyo.
Skiza makala haya kufamu mengi zaidi.
Mashabiki wa rfi Kiswahili kila Ijumaa hupata nafasi ya kuchangia mada yoyote ile kupitia makala haya.
Skiza maoni ya baadhi ya waskilizaji.
Rais wa Rwanda Paul Kagame amekanusha madai kuwa serikali yake imekuwa ikiminya uhuru wa kuabudu, akisisitiza kwamba hatua ya serikali kufuatilia taasisi za kidini ni kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji, na kuwalinda raia dhidi ya ulaghai,
Nchini Kenya, rais William Ruto na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua, wamekuwa wakirushiana maneno makali, kwenye mikutano ya hadhara na hata kwenda mbali na kutoa matusi na kushambuliana kuhusu maumbile yao, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Nini mtazamo wako kuhusu kauli za viongozi hawa ? Katika nchi yako wanasiasa, wanatupiana maneno hivi ?
Katika uamuzi wa kushangaza , Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limefuta ushindi wa Senegal kama mabingwa wa taji la AFCON na kulipa taji hilo Morocco ambao walikuwa wenyeji wa michuano hiyo.
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners