
Sign up to save your podcasts
Or


Nchini Uganda, wawaniaji wa urais wameshiriki mdahalo kuelekea uchaguzi wa mwezi ujao, huku rais Museveni akisusia mdahalo huo.
Je, unafikiri midahalo huwa na mchango wowote kwa wapiga kura kuelekea siku ya uchaguzi?
Skiza baadhi ya maoni ya waskilizaji.
Siku ya kimataifa ya mapambano dhidi ya UKIMWI, Umoja wa Mataifa unasema kupungua kwa misaada kunatishia dunia kufikia lengo la kudhibiti ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030, huduma za kinga zimevurugika hasa kwenye nchi masikini.
unazungumziaje siku hii, je dunia tumepiga hatua kukabiliana na ugonjwa huu?
Skiza maoni ya baadhi ya waskilizaji.
Viongozi wa Afrika na wale wa umoja wa Ulaya wamekutana nchini Angola, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa usalama na kiuchumi, rasilimali za bara hilo zikimulikwa na mataifa yenye nguvu ambayo yameongeza kasi ya uwekezaji kwenye bara hilo. Tumekuuliza unaamini ushirikiano uliopo unanufaisha pande zote ? Ushirikiano wa aina gani Afrika inapaswa kuwa nao na nchi za magharibi?
Msikilizaji juma lililopita watu wenye silaha waliwateka wanafunzi zaidi ya 300 pamoja na waalimu katika shule moja kwenye jimbo la Niger nchini Nigeria, tukio linalojiri siku chache tangu kutekwa kwa wanafunzi wengine 25 katika shule ya wasichana kwenye jimbo la Kebbi pia huko Nigeria. Vitendo vya utekaji wa watoto vinazidi kuongezeka katika nchi za Afrika magharibi na kati. Nini kifanyike kukomesha vitendo hivyo Afrika?Je taifa lako linashuhudia utekaji wa watoto? Ungana na Ruben Lukumbuka
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi ya kuchangi mada yoyote kuhusu taarifa na vipindi vyetu au kile kinafanyika hapo ulipo.
Skiza maoni ya waskilizaji juma hili.
Tunajadili hatua ya viongozi kadhaa wa Afrika akiwemo rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wamewateua watu wa familia zao katika nafasi za serikali, hali hii ikionekana kwenda kinyume na maadili ya kazi.
Tunakuuliza Je, uteuzi wa ndugu serikalini ni sahihi au si sahihi?
skiza Makala haya
Katika makala haya tunaangazia nchi ya Kenya ambapo chama cha ODM kilichokuwa cha waziri mkuu wa zamani hayati Raila Odinga, kimeadhimisha miaka 20 tangu kuasisiwa kwake.
Tunauliza je vya kisiasa vina mchango gani katika kuimarisha demokrasia hapa Afrika?
Skiza makala haya.
Aliyekuwa rais wa Malawi , Lazarus Chakwera kuteuliwa na Jumuiya ya madola kuwa mpatanishi wa mzozo wa kisiasa nchini Tanzania, hasa baada machafuko ya kipindi cha uchaguzi.
Tunakuuliza , unafikiri rais Chakwera atafanikiwa kusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini Tanzania.
Ulimwengu umeadhimisha siku ya kumbukumbu kwa waathiriwa wa ajali za barabarani.
Takwimu za umoja wa mataifa zinaonyesha kuwa, duniani kote, watu zaidi ya milioni moja hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, na millioni hamsini kujeruhiwa.
Nini kifanyike kupunguza ajali za barabarani.
Skiza makala kufahamau maoni ya mskilizaji zetu.
Katika makala ya Habari Rafiki hii leo tunazungumzia hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kutumia jeshi la nchi yake kupambana na wanajihadi wanaowauwa Wakiristo nchini Nigeria.
Kauli hii imewakasirisha viongozi wa Nigeria, ambao wanasema serikali nchini humo, haiungi mkono unyanyasaji wa kidini. Tumemuuliza msikilizaji anazungumzia vipi mpango wa huu wa Trump na ni nini kinaweza kufanyika kumaliza mauaji ya kidini nchini Nigeria.
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners