
Sign up to save your podcasts
Or


Waasi huko mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wameendelea kujiimarisha kiutawala, kisiasa na kimiundo mbinu katika kujenga barabara, kutangaza orodha ya mawakili, hatua inayodhihirisha kuwa waasi hao wanaendea kutengeneza serikali mbadala na ile ya Kinshasa. Makala ya habari rafiki inaangazia hatua hiyo
Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC imemhukumu rais mstaafu wa nchi hiyo Joseph Kabila Kabange adhabu ya kifo bila ya yeye mwenyewe kuwepo mahakamani, ikimtia hatiani kwa usaliti na uhalifu dhidi ya binadamu. Chama chake PPRD kimesema kesi hiyo ni ya kisiasa dhidi ya mpinzani mkubwa wa serikali. Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anaungana na wasikilizaji wa Idhaa kupata maoni yao kuhusu kesi hii, makinika kwa kusikiliza makala hii.-
Serikali ya DRC kupitia wizara ya sheria imesitisha utoaji wa leseni za Makanisa, katika kupambana na Rushwa! kwa maoni yako unaamini kusitisha utoaji wa leseni kutasaidia kupambana na rushwa? Hali ya rushwa ikoje katika taasisi za umma nchini mwako? Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka pamoja na wasikilizaji wetu wanajaribu kupata jibu kwa maswali hayo
Makala ya habari rafiki ya jumatatu septemba 29 2025 imeangazia hatua ya tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC kuzindua zoezi la kuwaandika wapiga kura ambalo limeonekana kuwavutia vijana wengi, maarufu kama Gen Z.Tumekuuliza msikilizaji je? unaona vijana wote wako tayari kujiandikisha na katika nchi yako vijana wanahamasishwa vipi. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka, kwa kutuma maoni ya sauti kupitia nambari yetu ya whatsApp: +254110000420 ama pia kupitia Facebook : RFI Kiswahili
Kila Ijumaa rfi kiswahili inakupa nafasi ya kuchangia mada yoyote, iwe kila kinaendelea hapo ulipo au yale umeskia kwenye matangazo yetu.
Skiza maoni ya juma hili
Je mataifa ya Africa yanatumia raslimali zake kujinufaisha?
Skiza maoni ya wakilizaji
Shaba yetu inalenga Nchini Kenya, ambapo madai ya kupora kwa pesa za bima ya afya ya serikali yanaendelea kutatiza utowaji wa huduma ya afya hili likiwaathiri raia wa kawaida.
Mskilizaji nchini mwako huduma za afya ni nafuu na bora, au bado wananchi wa kawaida wanahangaika kupata matibabu.
Skiza maoni ya waskilizaji wetu
Je umoja wa mataifa umesalia kimya ukiukaji wa haki ukiendelea?
Skiza makala haya kuskia hisia za waskilizaji wetu.
Kila mwaka tarehe 8 Septemba ulimwengu husherehekea maendeleo katika ujuzi wa kusoma na kuandika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa. Mwaka huu imekuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina kuhusu maana ya kusoma na kuandika katika enzi hii ya kidijitali.
Tunazungumzia hatua ya Kenya na Uganda kukubaliana rasmi kuondoa vizuizi vyote vya kibiashara, vikiwemo vizuizi vya ushuru na visivyo vya ushuru, ili kuwezesha mtiririko huru wa bidhaa, huduma, na watu kati ya mataifa hayo mawili
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners