
Sign up to save your podcasts
Or


Katika makala haya mshale wetu unalenga taifa la Kenya, ambapo polisi nchini humo wamefaulu kumkamata mshukiwa mkuu wa mauaji wanawake 42, ambao sehemu za miili yao iliyokuwa imekatwa vipande vipande na kuwekwa kwenye magunia kabla ya kutupwa kwenye shimo la kutupa taka.
Tunauliza mskilizaji unafikiri nini huchangia mambo kama haya kutokea kwa jamii.
Haya hapaa baadhi ya mano yako.
Katika makala haya tunajadili uwezekano wa vikosi vya MONUSCO nchini DRC kusalia kwa muda kwenye taifa hilo, kutokana na ripoti za uwepo wa wanajeshi wa Rwanda wanaowasaidia waasi wa M23.
Tumeuliza wewe unaunga mkono vikosi vya MONUSCO kusalia DRC?
Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote ile kuhusiana na taarifa zetu au kile kinachoendelea pale ulipo.
Juma hili waskilizaji walikuwa na kauli hii.
Kenya imetuma polisi wake nchini Haiti kwenda kujaribu kudhibiti magenge ya wahalifu ambayo yametatiza usalama wa taifa hilo kwa kipindi kirefu.
Polisi wa Kenya wanaenda Haiti licha ya mataifa kama Marekani kushindwa kurejesha amani nchini Haiti.
Je Polisi wa Kenya watafaulu? ndilo swali tumekuuliza.
Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Katika makala haya tunaangazia taifa la Burundi linalozidi kushuhudia uhaba mkubwa wa mafuta, hili likitatatiza shughuli za usafiri katika taifa hilo la Africa mashariki.
Tumekuuliza unafikiri nini huwa chanzo cha ukosefu wa mafuta katika mataifa yetu?
Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Katika makala haya tunajadili maadimisho siku ya kimataifa ya wakimbizi, yaliofanyika juma lililopita ripoti zikionesha watu zaidi ya millioni 120 duniani wanakimbia mataifa yao kutokona na mizozo, uchumi mbaya na mabadiliko ya tabia nchi.
Tumekuuliza nini kifanyike kukabiliana na wimbi la wakimbizi duniani?
Haya hapa baadhi ya maoni yako
Ofisi ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta imelalamikia kuhujumiwa kwa kutopewa ufadhili unaofaa
Kisa cha hivi punde nchini Kenya ambapo raia alimshambulia ofisa wa polisi ,kimeibua mjadala
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners