Jukwaa la Michezo

Jukwaa la Michezo

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Jukwaa la Michezo episodes

  • Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 zitafanyika Juni-Julai

    Leo tumeangazia CAF kudhibitisha kuwa AFCON 2027 itaandaliwa Afrika Mashariki licha ya tetesi za kuahirishwa au kuhamishwa, uchambuzi wa raundi ya mwisho ya hatua ya makundi mechi za klabu bingwa, mechi za kufuzu kombe la dunia la wasichana U20, siku ya kwanza ya michuano ya raga ya wachezaji saba kila upande divisheni ya pili ya HSBC, mfumo mpya wa mashindano ya Tour du Rwanda, kiungo wa Ghana Thomas Partey akumbwa na shtaka jipya lakini pia michezo ya Olimpiki msimu wa baridi.

    24 min
  • Yanga yalenga ushindi muhimu kukaribia robo fainali michuano ya klabu bingwa

    Leo tumeangazia mechi za klabu bingwa Afrika, Yanga itachuana na FAR Rabat nayo Azam ikicheza na Maniema, matukio kuelekea michuano ya gofu ya Magical Kenya Open, mechi za kufuzu kombe la dunia la kina dada chini ya miaka ishirini, rais wa soka DR Congo asimamisha shughuli zote katika uwanja wa Tata Raphael, Rais wa FIFA Infantino asema marufuku dhidi yz Urusi hayajasaidia chochote, mzozo kati ya Ronaldo na Al Nassr waendelea kwa mechi ya pili sasa.

    24 min
  • Uamuzi wa CAF kwenye fainali ya Afcon 2025: Udhibiti wa Haki au Uharibifu?

    Leo tumeangazia kwa undani hukumu na uamuzi wa Caf kufuatia matukio yaliyoibuka kwenye fainali ya AFCON 2025, Simba inajandaa kwa mechi ya kufa kupona kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, raundi ya kwanza ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mechi za Futsal yakamilika, msimu wa sita wa Ligi ya Afrika ya basketboli kumalizia nchini Rwanda, Faith Kipyegon ajenga hospitali huko Kenya, TP Mazembe yapata kocha mpya, fainali ya Australian Open, Ligi ya Mabingwa Ulaya yaingia raundi ya mtoano.

    24 min
  • CAF: Michuano ya klabu bingwa Afrika imerejea raundi ya tatu ya makundi

    Leo kwenye kipindi tumeangazia uchambuzi wa mashindano ya AFCON 2025, vilabu vya Afrika Mashariki vinatafuta tiketi ya mchujo mechi za klabu bingwa, Kinshasa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya Voliboli mwaka huu, wachezaji kadhaa wa ligi ya NBA waonesha nia kuiwakilisha Nigeria kwenye Olimpiki ya 2028, mashindano ya Afrika ya handboli inayoendelea Kigali, Uganda yapata kocha mpya wa basketboli, mfumo mpya wa mashabiki kupata visa mapema kuelekea Kombe la Dunia wafunguliwa rasmi

    24 min
  • AFCON 2025: Senegal, Morocco zatinga fainali. Je, nusu fainali ziliendaje?

    Leo tumeangazia pakubwa uchambuzi wa matukio na matokeo ya mechi za nusu fainali mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 na mechi ya mshindi wa tatu leo usiku, hotuba ya rais wa CAF Patrice Motsepe kabla ya fainali, Droo ya mashindano ya WAFCON ya kina dada ya mwaka huu, Rwanda kuwa mwenyeji wa michuano ya Afrika ya Handboli, Rwanda na Burkina Faso zafuta kazi makocha wao.

    24 min
  • AFCON 2025: Mbio za kuwania kufuzu kwa nusu fainali zinazidi kupamba moto

    Leo tutakufahamisha matukio yote kwenye raundi ya 16 bora, uchambuzi wa mechi haswa kuondolewa kwa DRC na Tanzania walivyolakiwa kishujaa nyumbani Dar es Salaam baada ya kutoka Morocco na uchambuzi wa mechi za robo fainali za jana na leo. Morocco na Senegal washajikatia tiketi ya nusu fainali. Algeria dhidi ya Nigeria na Misri dhidi ya Ivory Coast. 

    24 min
  • Uchambuzi wa Mada: Je, AFCON 2025 inatoa msisimko kama mashindano yaliyopita?

    Leo tunajadili kwa undani kauli ya kocha wa Afrika Kusini, Hugo Broos kuwa michuano ya mwaka huu haina mvuto na msisimko kama Afcon zilizopita. Uchambuzi wa mechi za jana na leo kwenye hatua ya 16 bora - Tanzania vs Morocco, Afrika Kusini vs Cameroon, DRC vs Algeria. Hatua ya serikali ya Gabon kuvunjilia mbali timu ya Gabon huku marais wa Msumbiji na Benin wakitoa ahadi za pesa kwa timu zao. Morocco kuandaa michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu 2029 nayo Ethiopia ikiwania kuandaa Afcon ya 2028.

    25 min
  • AFCON 2025: Mtazamo wa hatua ya mtoano, timu 16 zitawania tiketi ya fainali

    Leo tumeangazia kwa undani matokeo na matukio ya hatua ya makundi iliyokamilika kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea Morocco, uchambuzi wa hatua ya 16 bora - nani atafuzu robo fainali?, tathmini ya hatua ya serikali ya Gabon kuvunja kabisa timu ya taifa ya Gabon, ahadi za pesa kutoka kwa marais kadhaa Afrika kwa timu zao kuelekea robo fainali, usajili wa Rayon Sport, kwa nini Maresca aliondoka Chelsea?, dereva wa Anthony Joshua afunguliwa mashtaka baada ya ajali Nigeria.

    24 min
  • AFCON 2025: Morocco dhidi ya Comoros kufungua mashindano leo usiku

    Leo tunaangazia pakubwa kuanza kwa mashindano ya AFCON 2025; tunachambua mechi ya ufunguzi kati ya Morocco na Comoros, mjadala kuhusu mageuzi katika michuano hii, namna timu zilivyotua nchini Morocco kwa kuvalia mavazi ya kitamaduni, Morocco wapo kwenye shinikizo ya kunyakua ubingwa kwa kuwa mwenyeji lakini pia ubashiri wa mechi ya ufunguzi na atakayebeba taji la mwaka huu.

    24 min
  • AFCON 2025: Mashindano kufanyika kila baada ya miaka minne baada ya 2028

    Usiku mmoja kabla ya kuanza kwa michuano ya Afcon 2025 tunakufahamisha mambo yote unayostahili kujua pamoja na mabadiliko ya michuano hii kuendelea mbele, michezo ya chipukizi ya Afrika yatamatika Angola, Rayon Sports na Simba zapata makocha wapya, mkenya David Munyua aweka historia katika mchezo wa darts duniani, Anthony Joshua amlaza Jake Paul kupitia knockout, droo ya nusu fainali ya kombe la Carabao.

    24 min

About Jukwaa la Michezo

From the publisher's feed

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano…

More shows like Jukwaa la Michezo

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners