
Sign up to save your podcasts
Or


Baraza huru kati ya viongozi wa kijeshi na kiraia limeundwa nchini Sudan, kuongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka mitatu, je, litatimiza mahitaji ya raia wa Sudan ? Tunajadili.
Karibu katika makala ya mjadala wa wiki.Kikao cha 39 cha viongozi wa mataifa ya SADC kinataraji kuanza jijini Dar es salaam nchini Tanzania ajenda kuu ni kujadili mkakati wa kiuchumi kwa kuhimiza viwanda katika mataifa hayo.Fuatilia kwa kina,wachambuzi Wetengere Kitojo na Saidi Msonga wameangazia kinaga ubaga katika makala haya na mwandishi wetu Martha Saranga.
Wiki hii Waziri wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Oly Ilunga alitangaza kujiuzulu, baada ya kushtumu uamuzi wa rais Felix Tshekedi kumwondoa kwenye Kamati maalum ya kupambana na janga la ugonjwa hatari wa Ebola, ambao tangu mwezi Agosti mwaka 2018, umesababisha vifio vya watu 1,700 na wengine zaidi ya 200 kuambukizwa katika jimbo la Kivu Kaskazini. Nani atasaidia kumaliza Ebola nchini DRC na juhudi za WHO zinafua dafu ?
Mnadhimu Mkuu wa jeshi nchini Ethiopia Jenerali Seare Mekonnen ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake jijini Addis Ababa, sawa na rais wa jimbo la Amharic Ambachew Mekonen ambaye alishambuliwa na watu wenye silaha. Ni mauaji yanayokuja wakati huu, Waziri Mkuu Abiy Ahmed akiendeleza mageuzi nchini mwake.
Hii inamaanisha nini ? Tunachambua na wachambuzi wa siasa za Kimataifa Haji Kaburu, Comrad Sambala wote wakiwa jijini Dar es salaam nchini Tanzania. Emmanuel Makundi, anashiriki pia, ni Mwanhabari wa RFI Kiswahili.
Wiki hii, uongozi wa kijeshi nchini Sudan, uliamua kuvunja kambi ya waandamanaji jijini Khartoum ambao wamekuwa wakishinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.Watu zaidi ya 60 walipoteza maisha na mamia kujeruhiwa. Nini hatima ya Sudan ? Tunajadili.
Hatimaye rais wa DRC Felix Tshisekedi amemteua Sylvestre Ilunga kuwa Waziri Mkuu. Hii inakuja baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya rais huyo na mwenzake wa zamani Joseph Kabila. Matarajio ya raia wa DRC ni nini ?
Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu, anataka maandamano yafanyike nchini humo kumshinikiza rais Felix Thisekedi aondoke madarakani kama ilivyokuwa nchini Sudan na Algeria.
Fayulu anasema yeye ndiye aliyeshinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018.
Tunachambua hili kwa kina.
Baada ya kuwa madarakani kwa miaka 20 hatimaye Abdulaziz Bouteflika amelazimika kusalimu amri na kujiuzulu kama rais wa nchi wa Algeria.
Nini hatima ya nchi ya Algeria baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika mwenye umri wa miaka 82 ambaye tangu mwaka 2013 amekuwa akitumia gari la magurumu baada ya kupatwa na kiharusi.
Kwa mujibu wa Katiba, Spika wa Senate sasa ndio rais wa muda hadi pale Uchaguzi mpya utakapofanyika.
Baada ya miezi ya mapigano, kikundi cha jihadi cha Kiislam (IS) kimepoteza Baghuz, kijiji cha mashariki mwa Siria ambacho kinaelezwa kuhitimisha utawala wa kihalifa nchini syria.Kama ambavyo mwishoni mwa 2017, IS ilivyopoteza ngome zake za Mosul nchini Iraq na Raqqa nchini Syria.
Makala ya mjadala inaangazia mvutano wa kidiplomasi akati yamataifa mawili ya Afrika mashariki,Uganda na Rwanda wakati huu jumuiya ya Afrika mashariki ikiwa kimya..wachambuzi Abbas Mwalimu na Haji Kaburu wanadadavua kwa kina.
From the publisher's feed
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners