
Sign up to save your podcasts
Or


Makala hii imeangazia kauli ya rais wa Tanzania kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao ilivyozua gumzo katika uga wa kimataifa, msamaha wa mahakama kwa afisa mkuu wa polisi Kenya, ziara ya mjumbe wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ulinzi wa amani Jean Pierre Lacroix huko DRC, UN kughadhabishwa na kuahirishwa uchaguzi wa sudan Kusini, jeshi Ia Israeli lashambulia Hezbollah kwa kulipua vifaa vyao vya mawasiliano na kwengineko duniani.
Ni wiki iliyoshuhudia matukio mengi miongoni ni pamoja na serikali ya Kenya kuendelea na uchunguzi wa mkasa wa moto uliowauwa wanafunzi, maandamano ya maelfu ya wakimbizi kwenye mji wa Goma mashariki mwa DRC wakiomba serikali iwarejeshe makwao na kumaliza vita, kule Senegal rais Bassirou alilivunja Bunge la taifa, na mdahalo wa kwanza wa televisheni kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na makamu wa rais Kamala Harris wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi wa Novemba na mengineyo.
Makala hii imeangazia mkutano wa tisa kati ya China na Afrika huko Beijing, wafungwa zaidi ya 100 waliuawa katika gereza la makala nchini DRC, Kenya na mkasa wa moto ulivyowaua wanafunzi Kaunti ya Nyeri, uchaguzi kufanyika nchini Tunisia, na nchini Ufaransa Michel Barnier aliteuliwa kuwa waziri Mkuu, miezi miwili baada ya mvutano wa kisiasa nchini Ufaransa, na mambo mengine kwengineko duniani.
Uzinduzi wa kampeni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, anayegombea unyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kongamano la 74 la WHO mjini Brazzaville, nchini Congo, DRC na Kampeni inayoitwa ICC Haki kwa DRC, hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini Sudan, shambulio la kigaidi Burkina Faso laua zaidi ya watu 300, hali nchini Israeli, na mchakato wa uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba
Tumeangazia katika makala ya wiki hii ni pamoja na ugonjwa wa Mpox ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa, DRC ikiathirika zaidi, nchini Kenya Raila Odinga kutojihusisha tena na siasa, jeshi la Uganda lilivamia na kuharibu kambi ya kundi la waasi la LRA huko Sudan pande hasimu zasusia mkutano wa Geneva, nchini Marekani, makamu wa rais Kamala Harris akubali uteuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea wa nafasi ya urais, na mengineyo
Matukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan.
Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huo
Kule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.
Makala ya Juma hili imeangazia hukumu iliyotolewa dhidi ya kiongozi wa chama cha waasi wa M23/AFC mashariki mwa DRC Corneille Nangaa, Rais wa Kenya aapisha baraza jipya la mawaziri miongoni mwao wanasiasa wa upinzani, mapigano ya nchini Sudan, maandamano nchini Nigeria na uongozi mpya wa mpito nchini Bangladesh baada ya kutoroka kwa waziri mkuu pia tumengazia yaliyojiri kwengineko duniani.
Makala hii imeangazia kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh nchini Iran, mazishi yake yalifanyika Doha, Urusi, mataifa ya Magharibi wabadilishana wafungwa, waziri mkuu wa DRC Judith Suminwa aongoza kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya wakongo maarufu, Genocost, yaliyojiri nchini Kenya, na mgomo wa wafanyabiashara wa Uganda, hukumu dhidi ya dikteta wa zamani wa nchini Guinea na kwengineko duniani.
Makala imeangazia hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Ijumaa ya wiki hii, huku miundombinu ya treni za umeme ikishambuliwa, rais William Ruto atangaza baraza la mawaziri akiwajumuisha wanasiasa wanne wa upinzani, kesi dhidi ya kiongozi wa muungano wa waasi Corneille Nangaa jijini Kinshasa nchini DRC, Maandamano na kukamatwa kwa vijana kule Uganda, siasa za Afrika Magharibi, na Kaskazini,Joe Biden ajijiondoa katika ki nyang’anyiro cha uchauguzi huku Kamala Harris akiteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic nchini Marekani.
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto ya kuwateua mawaziri wapya baada ya mashinikizo, nchi yake ikishuhudia maandamano ya vijana, Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya watu ambao miili yao ilikutwa jalalani Kware jijini Nairobi akiri kuwaua wanawake 42, rais wa Rwanda Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kishindo, Waasi wa M23 na jeshi la congo FARDC wakubali kusimamisha vita baada ya Marekani kutangaza kuongeza muda wa siku 15 kuruhusu misaada ya kibinadamu...na mengineyo..kwengineko duniani ambako watu wamestushwa ulimwenguni kuhusu hitilafu iliyojitokeza kiteknolojia..-
From the publisher's feed
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners