
Sign up to save your podcasts
Or


Wiki hii baadhi ya mambo tunayoangazia ni athari za mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki, pia mgogoro kule Sudan, lakini pia kauli ya Ufaransa kwa Rwanda kuacha kuunga mkono kundi la M23 kule DRC. Kadhalika tutaangazia uhuru wa vyombo vya habari kuminywa nchini Burkina Faso lakini pia kibali cha kukamatwa kwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Makala haya yanaangazia yaliyojiri nchini Kenya na Tanzania kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 70 ,mgomo wa madaktari nchini Kenya, Tanzania kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, safari za wahamiaji walioko nchini Uingereza kuelekea nchini Rwanda
Tutaangazia pia uchaguzi wa wabunge nchini Togo,usalama wa Burkina Faso , na Ulimweguni tutazidi kuangazia Mzozo unaondelea baina ya Israel na Hamas .
Makala hii inaangazia yaliyojiri nchini Kenya na kifo cha mkuu wa majeshi ya nchi hiyo KDF aliyepoteza maisha na maafdisa wengine tisa wa jeshi katika ajali ya helikopta Alhamisi Aprili 18, rais William Ruto alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, mgomo wa wafanyabiashara huko Kampala Uganda, ziara ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na EU huko Goma kutathmini hali ya kibinadamu kwa waliokimbia mapigano ya M23, Senegal, pia Togo kuhusu ziara ya ujumbe wa ECOWAS, lakini pia mashambulio kati ya Iran na Israel.
Makala yameangazia mambo mengi ikiwemo maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yanaendelea wiki hii, MONUSCO kuanza kuwaondoa wanajeshi wake eneo la mashariki mwa DRC, mgomo wa madaktari nchini Kenya, mwaka mmoja wa mzozo wa Sudani kutimia jumatatu ya aprili 15 na mengineyo duniani. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi
Ni makala maalum, kuhusu kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, tunahoji mchakato wa maridhiano umefikia wapi miaka 30 baadaye..... hali iko vipi kwa sasa. na dunia imepata somo gani? Pia kuhusu mauaji hayo, tutarejelea kauli ya Rais Emanuel Macron iliyoonekana kuwa inalenga kutuliza hisia za waathiriwa.
Huko DRC uteuzi wa Judith Tuluka Suminwa, mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu. Mahakama nchini Uganda ilitoa uamuzi wake kuhusu sheria dhidi ya ushoga. Kabla ya kwenda Kenya, Sudani..pamoja na Senegal ambako Bassirou DF aliapishwa kuwa rais mpya, tutakwenda Israeli na maeneo mengine duniani.
Rais mteule wa senegal akutana na rais anayemaliza muhula wake Macky Sall, chama kipya cha aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma chazuwiwa kushiriki uchaguzi wa mwezi mei,kamati ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa, yaitaka Uingereza kuachana na mpango wake wa kuwahamisha wahamiaji kwenda nchini Rwanda, na rais wa DRC Félix Tshisekedi ahitimisha ziara yake huko Mauretania, tutaangazia siasa za Kenya, Tanzania, yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani.
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Uganda Yoweri Museveni ya kumteua mwanawe kuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, mazishi ya mwanasiasa Cherubin Okende, yaliyojiri nchini Rwanda, lakini pia Sudan huko ambako wiki hii Marekani ilisema kuwa ina matumaini mazungumzo ya kumaliza mzozo wa nchi hiyo yatarejea hivi karibuni baada ya mfungo wa Ramadan, uchaguzi wa urais huko Senegal jumapili ya Marchi 24 tumeangazia yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani. Ungana nami Reuben Lukumbuka
Kwenye Makala ya wiki hii tunaangazia hatua ya Rais Kagame kukubali kukutana na mwenzake wa DRC Tshisekedi, pia tutaangalia alivyofukuzwa chamani kiongozi wa chama cha CNL nchini Burundi, Agathon Rwassa, lakini vilevile kilichojadiliwa katika mkutano kati ya marais wa Kenya, Tanzania na Uganda.
Tutatupia jicho hali ya kibinadamu nchini Sudan, lakini pia siasa za Senegal baada ya kuachiwa kwa Ousmane Sonko, siku chache kabla ya uchaguzi wa Machi 24, kule Nigeria tutaangalia yanayojiri baada ya wanafunzi kutekwa na rais Tinubu kusema hawatatii agizo la watekaji la kutaka kulipwa ili kuwaachia wanafunzi hao.
Pia hali kule Haiti baada ya waziri mkuu Ariel Henry kukubali kujiuzulu, Meli ya kwanza ya chakula cha msaada kutoka Cyprus kuwasili Gaza na pia siasa za Marekani baada ya rais Joe Biden na mtangulizi wake Donald Trump kushinda uteuzi katika vyama vyao.
Niliyeshika usukani ni Jupiter Mayaka kwa niaba ya Ruben Lukumbuka ambaye yuko Pwani ya Kenya anakula upepo wa bahari. Kwa mengi zaidi bonyeza linki usikilize makala.
Hali ya usalama kuendelea kuzorota mashariki mwa DRC baada ya waasi wa M23 kuteka miji kadhaa kama Nyanzale na maeneo jirani, wabunge nchini Uingereza kupinga mpango wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, uchaguzi wa urais kufanyika marchi 24 nchini Senegal, mpya wa 32 wa jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.
Yaliyojiri wiki hii ni pamoja na kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, na kauli za rais Felix Tshisekedi kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na rais mwenza wa Rwanda Paul Kagame, ziara ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed nchini Tanzania na pia Kenya, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Arusha, yaliyojiri nchini Rwanda, kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.
From the publisher's feed
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners