
Sign up to save your podcasts
Or


Makala hii imeangazia kuzorota kwa hali ya usalama pembezoni mwa mji wa Sake DRC,na kauli za rais Felix Tshisekedi mbele ya wanahabari wiki jijini Kinshasa, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Mbeya, mazishi ya mwanariadha wa Kenya aliyekuwa anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za marathon Kelvin Kiptum, yaliyojiri nchini Rwanda, na pia kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.
Wiki imejaa matukio ya kutamausha kwanza; wanajeshi wawili wa Afrika kusini waliuawa mashariki mwa DRC, kinara wa upinzani wa nchini Kenya Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, maandamano ya wapinzani nchini Tanzania, yaliyojiri Sudani, pia Senegal huko Afrika magharibi, kifo cha mpinzani huko Urusi Alexei Navalyn, shinikizo za kimataifa dhidi ya Israeli ikubali kusitisha vita dhidi ya Hamas,na mengineyo
Hali ya wasiwasi iliyoshuhudiwa kwenye mji wa Goma, baada ya waasi wa M23 kuonekana kuukaribia mji huo huko mashariki mwa DRC,ziara ya rais wa Poland nchini Kenya na huko Rwanda, kuapishwa kwa rais mpya wa muda nchini Namibia baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hague GeinGhob, yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika magharibi pia uteuzi wa baraza jipya la mawaziri nchini Ufaransa, siasa za Marekani na kwengineko duniani
Miongoni ni pamoja na watu watatu wafariki dunia katika mlipuko wa gesi jijini Nairobi nchini Kenya, kundi la waasi wa Uganda wa ADF waendeleza mauaji ya raia wa kawaida nchini DRC,lakini pia yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika Mashariki, Afrika magharibi na Mgomo wa wakulima nchini Ufaransa, hali ya Israeli na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
Yaliyojiri wiki hii inaangazia kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame kwamba ataitetea nchi yake kwa gharama yoyote ile, upinzani nchini Tanzania uliandamana kupinga mabadiliko ya sheria za uchaguzi, mauaji ya watu zaidi ya kumi mjini Mwesso mashariki mwa DRC, uchaguzi visiwani Komoro hali katika ukanda wa Afrika Magharibi lakini pia uchaguzi mdogo huko Marekani,
Makala hii imeangazia kuhusu kuapishwa rais wa DRC Félix Tshisekedi baada Mahakama ya katiba kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi wa desemba 20, viongozi wa nchi wananchama wa IGAD walikutana jijini Kampala huku wakitoa wito wa kusitishwa mapigano Sudan, waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak na mpango wa kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda.
Mahakama ya katiba huko DRC iliidhinisha ushindi wa rais Félix Tshisekedi,rais wa Uganda Yoweri Museveni awatahadharisha waasi wa ADF, Waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak akabiliwa na wakati mgumu kuhusu suala la kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda, yaliyojiri katika ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia uteuzi wa Gabriel Attal kuwa waziri Mkuu wa kwanza kijana nchini Ufaransa, mashambulio ya jeshi la Israeli yawaathiri raia wa kawaida mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
Miongoni mwa habari kuu za wiki hii ni pamoja na dunia kuukaribisha mwaka mpya 2024, mvutano kati ya rais wa Kenya William Ruto na idara za mahakama, wapinzani wa DRC waendelea kuonesha kutofurahishwa na ushindi wa rais Felix Tshisekedi kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa desemba 20 mwaka uliopita, yaliyotangazwa na CENI, yaliyojiri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia mashambulio mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
Baadhi ya habari ambazo tumeangazia ni matokeo ya uchaguzi nchini DRC ambapo Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi kwa muhula wa pili kwa asilimia 73.34, katika matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa na Ceni Jumapili jioni.
Tutaangazia pia mashambulio ya ADF kule Uganda lakini pia mkutano wa ana kwa ana kati ya majenerali wanaopigana Sudan ambao haukufanikiwa, hali kule Nigeria kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika jimbo la Plateau, Urusi kufungua tena ubalozi wake nchini Burkina Faso na ulimwenguni tutazidi kuangazia hali ya vita vya Gaza
Kwenye makala yaliyojiri wiki hii, tumeangazia uchaguzi kule DRC wakati huu shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea, kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki chaondoka rasmi nchini DRC, mapigano kule Sudan.
Pia tumeangazia uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Niger, pia siasa za Afrika Kusini na kwingineko ulimwenguni tumeangazia masaibu yanayomkabili Donald Trump lakini pia hali kule Gaza.
From the publisher's feed
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners