
Sign up to save your podcasts
Or


Wawawake kutoka ukanda wa Afrika wanajumuika Dar Es Salaam mwishoni mwa juma kupiga jeki kampeni za kuboresha afya
Nchini DRC mikakati iliyoweka kudhibiti mlipuko wa Kipindu Pindu ulioripotiwa katika mataifa ya Afrika ya Kusini ,inaendelea kulipa na hata kuwa msaada kwa mataifa jirani kama vile Zambia
Usalama mdogo nchini Sudan Kusini umesababisha wagonjwa wengi kuchelewa kubainishwa TB na kupata matibabu ya mapema
Watalaam wa afya wanashauri ulimwengu kukumbatia teknolojia za kisasa kama vile Akili Mnemba kurahisisha ubainishaji na kuongeza usahihi wa vipimo
Idadi ya wanawake wanaongoza katika sekta mbali mbali bado ni ndogo barani Afrika.
Kauli mbinu mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake ni kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuongeza kasi ya maendeleo,tunaangazia wanawake wanasayansi na watafiti nchini Kenya ,wakijikita kwenye utafiti wa magonjwa yaliyotengwa
Mimba za utotoni ni kizingiti kikubwa kinachoathiri elimu ya wasichana barani Afrika
UNITAID imekuwa ikishirikiana na mataifa kuleta dawa mpya na za bei nafuu
Upatikanaji wa dawa zilizo za viwango vya juu na kwa bei nafuu bado ni changamoto kubwa kwa mataifa yanayoendelea.Matibabu ambayo bado ni mapya hukumbwa na vikwazo vingi kuingia soko la kimataifa na sasa UNITAID imekuwa mbioni kuziba pengo hilo
Village Reach ambayo kwa tafsiri rahisi ni kufikia maeneo ya vijijini, imefungua ofisi za kikanda jijini Nairobi kujaribu kusaidia serikali kusimamia namba ya dharura,usafirishaji wa sampuli za Polio na kuboresha utendakazi wa wahudumu wa afya wanaofanya kazi katika jamii tofauti
Baada ya kupata mafanikio makubwa katika nchi za Msumbiji, Malawi ,Village Reach inapanga kutumia mafunzo hayo kusaidia kuboresha huduma za afya katika mataifa ya Afrika.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,Village reach imeimarisha huduma za utoaji chanjo ,usafirishaji wa chanjo kutumia ndege zisizo na rubani katika maeneo yasiyo na miundo mbinu ikiwemo mkoa wa Equateur.
Aidha shirika hilo linatoa huduma kwa ushirikiano na serikali katika mataifa mengine yenye mzozo kama vile Niger na Sudan Kusini.
Afisa mkuu mtendaji Emily Bancroft amesisitiza mifumo ya afya inastahili kuwa thabiti ili kuwa na uwezo wa kustahimili majanga na hali za dharura kama ilivyoshuhudiwa wakati wa Uviko 19
Shirika la afya duniani limeorodhesha ongezeko la watu wanaokumbwa na changamoto za afya ya akili hususan tangu kuzuka janga la Corona,kupanda gharama ya maisha na mfumuko wa bei
Juhudi zinaendelea kuhakikisha dawa mwafaka ya TB miongoni mwa watoto zinaendelea
Licha ya kuwa TB inaweza kuambukiza watu wa umri wowote ,watoto kwa miaka wamekuwa wakiachwa nyuma katika matibabu ya TB. Watoto kwa miaka walilazimika kutumia donge za watu wazima.
Nchi zinazoendelea zinashuhudia ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa ukiwemo Kisukari
From the publisher's feed
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners