
Sign up to save your podcasts
Or


Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameendelea kusisitiza kufanya mazishi ya kitaifa kwa mtagulizi wake Edgar Lungu Licha ya mzozo uliopo baina yake na familia juu ya utekelezwaji ya matakwa ya marehemu ya kukataa kufanyiwa mazishi ya kitaifa.Tunakuuliza maoni yako kuhusu mzozo huo.
Kila siku ya Ijumaa, hapa RFI Kiswahili, tunampa mskilizaji wetu nafasi kuzungumzia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii au kutueleza jambo lolote ambalo limetokea nchini mwake.
Wiki hii maoni mseto yameangazia, miongoni mwa taarifa zingine, tangazo kwamba Rwanda itatia saini makubaliano na DRC tarehe 27 Juni, kumaliza mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini pia mashambulio baina ya Israeli na Iran.
Rais wa Burundi Evariste #Ndayishimiye ametoa wito kwa upinzani kushiriki katika mazungumzo na chama chake CNDD-FDD baada ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao ulikumbwa na upinzani mkubwa kwa ukosefu wa uwazi.
Hata hivyo upinzani haujaonyesha nia ya kushiriki mazungumzo hayo.
Tunakuuliza, ni sahihi upinzani kujiunga na serikali ?
skiza makala haya kuskia maoni ya mskilizaji.
Juni 12, ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto. Inakadriwa, takriban watoto milioni 200 kote duniani wanatumikishwa badala ya kuwa shuleni.
Tunakuuliza, serikali yako inafanya vya kutosha kukomesha utumwa wa watoto?
Unamfahamu mtoto anayefanyishwa kazi?
Makala haya yanaangazia afya ya akili, ikizingatiwa kuwa Juni ni Mwezi wa Uhamasishaji wa Afya ya Akili ya Wanaume.
Unafikiri ni kwanini wanaume wanashindwa kutafuta ushauri wa afya ya akili?
Unadhani afya ya akili ya mwanaume inasahaulika?
Skiliza makala ya leo usikie maoni kutoka kwa waskilizaji wetu.
Leo shaba yetu inalenga nchi ya Rwanda ambapo nchi hiyo imetangaza kujiondoa kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati, na kuituhumu jirani wake DRC, kwa kutumia baadhi ya wanachama kuendeleza ajenda zake zinazokandamiza Rwanda.
Skiza makala hay kuskia maoni ya mskilizaji wetu.
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi ya kuchangia mada yoyote iwe kila uliskia kwenye habari zetu au kile kinachoendelea hapo ulipo.
Skiza maoni ya mskilizaji.
Leo shaba yetu inalenga taifa la Uganda ambapo rais Yoweri #Museveni pamoja na mkewe wameomba raia wa nchi hiyo msamaha kwa mabaya yote ambayo serikali yao imetekeleza kwa miaka 39.
Je, unafikiri kauli ya Rais Museveni na Mama Janet kuomba msamaha ni ya kweli au ni ya kisiasa?
Skiza maoni ya mskilizaji wetu.
Katika makala haya shaba yetu inalenga jumuia ya Africa mashariki, tumekuuliza mskilizaji je unahisi una chochote cha kujivunia kuwa mwanachama wa jumuiya ya Africa Mashariki.
Skiza maoni ya mskilizaji wetu.
Umoja wa Afrika imesherekea siku ya kiafrika, kuadimisha kuundwa kwa Umoja wa Afrika, kipindi hiki nchi ya Uganda nayo ikisitisha ushirikiano wake wa kijeshi na taifa la Ujerumani.
Kuna chochote bara la Afrika linaweza kujivunia?
Ndilo swali tumekuuliza, skiza makala haya kuskia maoni ya waskilizaji.
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners