Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii episodes

  • ADF waendesha mashambulizi jijini Kampala Uganda, Magaidi watatu wakamatwa Kenya
    Makala hii imeangazia tukio la mashambulizi ya kigaidi siku ya jumanne ya November 16 jijini Kampala, idara za usalama zikiwataka raia kuchukua tahadhari huku shughuli za kibiashara zikiripotiwa kuendelea kama kawiada, ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken nchini Kenya, mauaji mapya ya nchini DRC huko Mikenge Kivu kusini, na Vuhesi wilatani Beni mkoani Kivu kaskazini, na hatua ya Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya viongozi wa Burundi ni miongoni mwa mengi yaliyopewa uzito katika matangazo ya juma hili.
    21 min
  • Kifo cha De Klerk Afrika kusini, DRC waasi wa ADF wauwa kikatili, Ethiopia hali bado
    Makala hii imeangazia mambo mengi ikiwa ni pamoja kifo cha rais wa zamani mweupe wa Afrika kusini F W De Klerk, akiwa na umri wa miaka 85, nchini Ethiopia mgogoro wa kisiasa waendelea kufukuta, huku serikali ikionesha nia ya kufanya mazungumzo na waasi, kule DRC mashambulizi ya waasi wa M23 maeneo ya Chanzu na Runyoni, na pia mauaji ya waasi wa ADF wilayani Beni mashariki mwa nchi hiyo. Kenya yashuhudia kuchomwa Shule kadhaa, pamoja na mambo mengine mengi..kutoka kila kona dunia.
    21 min
  • Makundi tisa ya waasi nchini Ethiopia yaungana kuuangusha utawala wa Addis Ababa
    Makala hii imeangazia hali ya mapigano yanayoendelea nchini Ethiopia ambapo makundi tisa ya wapiganaji wenye silaha yamejiapiza kuuangusha utawala wake Abiy Ahmed, kundi moja la waasi lauvamia mji wa Bukavu huko mashariki mwa nchi hiyo, lakini pia mkutano wa COP26 uliofanyika huko Glasgow, Scotland nchini Uingereza na mambo mengine yameangaziwa katika makala hii ya yaliyojiri wiki hii.
    21 min
  • Umoja wa mataifa wasikitishwa na hali nchini Sudan
    Makala hii imeangazia vurugu zinazoshuhudiwa nchini Sudan baada ya kufanyika mapinduzi ya kijeshi na baadaye kuachiwa huru kwa waziri mkuu Abdallah Hamdok ambapo Umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika, zimelaani hali hiyo ambapo maandamano yameendelea nchini humo. Huko DRC tumeangazia kuhusu kuapishwa kwa mwenyekiti mpya wa CENI Denis Kadima anayepingwa na dhehebu la kikatoliki na lile la kiprotestanti pamoja na mambo mengine yaliyojiri duniani.
    21 min
  • Kenya na Malawi zaimarisha ushirikiano wao, rais wa DRC amwidhinisha mkuu mpya wa CENI
    Makala hii imeangazia hatua ya rais wa DRC Felix Tshisekedi kumwidhinisha Denis Kadima kuwa mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi CENI pamoja na wajumbe 12 ikitarajiwa kwamba upinzani utatoa majina ya wajumbe watatu ili kukamilisha orodha ya wajumbe 15. Kenya na Malawi zilitiliana saini makubaliano kadhaa ikiwemo ya kibiashara na usalama pamoja na mambo mengine mengi..Karibu kuungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza zaidi
    21 min
  • Ziara ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini Marekani, kuachiwa huru kwa Kambidi DRC
    Makala hii imeangazia ziara ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini Marekani na ahadi za mwenyeji wake rais Joe Biden, hali ya wasiwasi inayosababishwa na waasi wa ADF huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika maeneo ya Mutwanga jeshi la congo FARDC lashirikiana na askari walinzi wa mbuga ya wanyamapori ya Virunga katika kukabiliana na kundi la ADF, hali ya kisiasa nchini Rwanda na mataifa ya magharibi pia mambo mengine mengi.
    Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
    21 min
  • Guteress ataka Ethiopia kutoa ushahidi dhidi ya wafanyakazi wa UN waliofukuzwa
    Makala hii imeangazia kufukuzwa kwa wafanyakazi wa umoja wa mataifa nchini Ethiopia, mvutano kati ya viongozi wa madhehebu ya kikatoliki kiprotestanti na makanisa ya uamsho huko DRC washindwa kuafikiana kuhusu uteuzi wa mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi, CENI. Huko Burundi wafanyakazi wa serikali waaswa kuhalalisha ndoa zao; la sivyo wafukuzwe kazi...pamoja na mengine mengi duniani kwa wiki hii.
    Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi.
    21 min
  • Ethiopia yawafukuza viongozi wa Umoja wa Mataifa
    Miongoni mwa taarifa kuu za dunia tulilozipa uzito wiki hii ni pamoja na Ethiopia kuwafukuza viongozi wa Umoja wa Mataifa nchini mwake, hali ya usalama kuendelea kuzorota Mashariki mwa DRC na Majenerali wa Marekani wasema walimshauri rais Joe Biden kutowandoa wanajeshi wote nchini Afganistan.
    20 min
  • Diplomasia kati ya Kigali na Brussels mashakani, mwanahabari akamatwa DRC
    Makala hii imeangazia kuzorota kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Ubelgiji kufuatia kesi ya Paul Rusesabagina, na huko DRC kukamatwa kwa mwandishi wa habari Sosthene Kambidi kupisha uchunguzi kuhusu mauaji ya wataalamu wawili wa Umoja wa mataifa Zaida Catalan na Michael Sharp mwaka 2017, pamoja na mengine mengi yaliyojiri kwenye Mataifa kadhaa.
    21 min
  • Umoja wa mataifa washutumu Burundi kuhusu haki za binadamu wiki hii
    Makala hii imeangazia ripoti ya tume ya umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Burundi ambayo imeonesha kuzorota kwa haki za binadamu, katika kipindi cha miezi 15 iliyopita, nchini DR Congo polisi jijini Kinshasa walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa muungano wa upinzani wa Lamuka walipoandamana kupinga kuingiliwa kisiasa kwa CENI, Septemba 14 aliuawa mwanachama maarufu wa wakimbizi wa Rwanda nchini Msumbiji Revocat Karemangingo, afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda lililopinduliwa na mwenye cheo cha luteni pamoja na mambo mengine mengi kutoka kila kona ya dunia.
    21 min

About Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

From the publisher's feed

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

More shows like Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners