
Sign up to save your podcasts
Or


Ongezeko la magonjwa ya milipuko linaibua swala la kwa nini watalaam wa wanyama hawahusishwi kikamilifu katika mifumo ya afya ya binadaam
Mpango wa one Health Approach unaonadiwa kwa sasa kwa mataifa ,unahimiza kuipa kipau mbele afya ya wanyama ,ili kuchangia siha njema ,usalama wa chakula na maendeleo endelevu .
Kumekuwa na malalamishi ya maziwa yaliyo kwenye soko kusababisha madhara ya kiafya
Watalaam wa afya ,bodi inayosimamia bidhaa za maziwa nchini Kenya na wanavetirinari wanasema matatizo hayo huenda yanatokana na uzembe wakati wa uchakataji maziwa ,uhifadhi na pia wafanyabiashara wenye pupa.
Baadhi ya changamoto zinazokumba sekta ya tiba asilia ni mwitiko na ukosefu wa sheria za kuisimamia katika nchi mbali mbali
Waganga wa tiba asilia wana mchango katika ulimwengu wa uzalishaji dawa
Kuna idadi kubwa ya watu wanaoshindwa kupata maji salama kwa matumizi ya nyumbani ,hospitali na hata mashamba
Uhaba wa maji unaorodheshwa kuwa sababu kubwa ya watu kukosa chakula, kujikimu katika nchi zinazoshuhudia migogoro.
Katika nchi kama Sudan na DRC kuna ripoti za hospitali ,kambi za wakimbizi kukosa moja hivyo mashirika ya kimsaada yanapata changamoto kuwahudumia wakimbizi
Ukosefu wa lishe bora huathiri afya na elimu nchini Kenya
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la linalowahudumia Watoto (UNICEF) imeonesha kuwa takriban watoto milioni mbili nchini Kenya wanakabiliwa na matatizo yanayotokana na utapiamlo.
Mipango ya lishe bora shuleni eneo la Nyanza na maghari mwa Kenya umeonekana kuwa suluhu huku wanafunzi wakipata vyakula vilivyo na virutubishi bora vinavyosaidia kuboresha kinga ya mwili,hivyo kuimarisha afya .
WHO imetaja ukosefu wa huduma za kuokoa maisha wakati wa kujifungua huchangia vifo vingi vya wanawake waja wazito
Huduma hizo za wanawake hata hivyo zina bei kubwa
Serikali za Afrika zitalazimika kuchangia ufadhili wa mipango ya kupambana na Malaria kufidia pengo kubwa la ufadhili
Muungano wa viongozi wa Afrika wa kupambana na Malaria ,Africa Leaders Malaria Alliance unasema Afrika inahitaji dola bilioni 5 nukta nane mwaka huu wa kifedha hadi 2026.
Hali hii pia imechangiwa na Marekani kukata ufadhili wa misaada kwa nchi za kigeni
Mamia ya wakaazi wa kaskazini mashariki mwa Kenya maeneo yanayopakana na Somalia na waathiriwa wakubwa wa mzozo wa Somalia hawajakuwa na maji masafi , hali hiyo ikizidisha mgogoro wa kijamii ndani ya jamii hii ya wafugaji wanaotokea upande wa Kenya na upande mwingine wa Somalia.
Kukabili hali hii ,kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu , International Committee of the Red cross ,ICRC , shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya ,Kenya Red Cross,KRC katika mkakati wa kuleta amani na ustawi imekuwa ikifanya miradi ya kuwapa wakazi maji .
Carol Korir amezuru eneo la Masalani ,kaunti ya Garissa kilomita chache na msitu wa Boni ambapo Al shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi na kujificha .
Katika siku za hivi punde magonjwa ya milipuko imeripotiwa katika mataifa ya Afrika ,ikiwemo Ebola Marburg na Mpox
From the publisher's feed
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners