
Sign up to save your podcasts
Or


Watu wengi wanapokaribia kufunga ndoa,hujukumika kufanya vipimo vya virusi vya HIV .Wengi hufanya kipimo hicho si kwa sababu wanajua umuhimu wake bali ni kwa sababu ya ulazima kabla kufunga harusi haswa za Kikristo.
Hata hivyo watalaam wa afya wanasema kuna vipimo tele ambavyo ni muhimu pia na vinahitajika kufanywa kabla ndoa.
Mwanasaikolojia Naomi Ngugi anasema kando na kipimo cha HIV,kuna kipimo cha Rhesus Factor ambayo kama mtu na mwenzake hana ufahamu ,wanaweza kupata shida ya kuharibika mimba.
Kuna pia kipimo cha Genotype kubaini uwepo wa ugonjwa kama Selimundu ,Hepatitis B, Hepatitis C au homa ya ini,vipimo vya Magonjwa sugu, Magonjwa ya akili na Vipimo vya uzazi kubaini ubora wa mbegu za kiume na matatizo ya mirija kuziba upande wa wanawake.
Vipimo hivyo vinaweza kugharimu ndoa iwapo wanandoa hawataweka wazi.
Vyakula vinavyoandaliwa nje ya jikoni kwangu huwezi kufahamu viwango gani vya usafi vimezingatiwa
Unapoaumua unakula kwa mama nitilie ni vigezo gani unaweza ukaweka ili kuhakikisha unalinda afya yako? Alfred Lobawoi kwenye makala haya ,amewahoji wauza vyakula na walaji kujua mtazamo wao
Juhudi za serikali za Afrika kuja na mikakati ya kutoa huduma za afya kwa raia kupitia mipango ya bima ya afya ya kitaifa zimekabiliwa na changamoto za utekelezaji,ufisadi na mifumo isiyo thabiti.
Watalaam wa afya sasa wanapendekeza mipango hiyo ya afya iwe kwenye mipango ya kitaifa ya kila mwaka,ikiwa na mwongozi kamili kuhusu huduma gani serikali itatoa kwa raia na kwa kiasi gani.
Aidha watalaam wanashauri mipango hiyo iwe inaendana na mahitaji ya kila jamii kwa kuwa serikali nyingi kwa sasa hazina uwezo wa kutoa huduma zote kwa raia
Isitoshe,mifumo inyopunguza uvujaji wa raslimali za umma ni muhimu
Wanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao.
Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita.
Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika .
Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili.
Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana.
Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekundu nchini ,KRC,katika kujaribu kukabili hali hiyo ,zinatekeleza mpango wa kujaribu kurejesha mawasiliano na uhusiano wa familia za wakimbizi.
Kwa kuwatafuta namna ambao wakimbizi hao wanaweza kuwasiliana kupitia ujumbe wa kuandikiwa au kwa njia ya simu,mashirika hayo wanasema wamefanikiwa kuwarejeshea tabasamu wachache wenye bahati na wanaendelea kuwasaka wanafamilia zaidi kila mwaka.
Matunda ya mpango huo yameonekana miongoni mwa wakimbizi wanaozungumza na jamaa zao na pia kwa wahudumu wa kujitolea wanaotangamana karibu kila siku na wakimbizi hao kwenye kambi.
Hivi karibuni watalaam wa afya pamoja kwa ushirikiano na shirikisho la ugonjwa wa kisukari duniani,wamethibitisha uwepo wa Kisukari aina ya tano ambao unahusishwa na utapiamlo
Aina hii ya kisukari huathiri watu ambao hawakupata lishe bora wakiwa watoto na kuathiri ukuaji wa kongosho inayozalisha Insulin inayodhibiti sukari mwilini.
Aidha kisukari aina ya tano inaweza kuwapata watu ambao wamekumbwa na njaa kwa muda mrefu ,kufanyiwa operesheni ambayo inafanya mtu kupungua mwili kwa kiasi kikubwa.
Watu wengi hudhani kuwa Pneumonia husababishwa na baridi kuingia kwenye kifua lakini watalaam wanasema chanzo cha Pneumonia ni vimelea kushambulia mapafu na mfumo wa kupumulia
Watalaam wa afya wanasema ndani ya wiki moja, mtu aliye na Pneumonia hugundulika kwa kuwa anapata ugumu wa kupumua au hata kukosa hewa.
Hali ya afya ya watoto haswa katika mataifa ya Afrika imeendelea kuzorota huku kukiwa na ongezeko la visa vya utapiamlo mbaya,ukosefu wa lishe na uhaba wa chanjo muhimu
Taasisi zinazojikita kwenye afya ya watoto zinaonya kuwa punguzo kwenye ufadhili kwenye afya ya watoto utaathiri afya ya jamii kwa jumla.
Pengo hili limetokana na ongezeko la mizozo na uchumi wa dunia uliotetereka tangu wakati wa janga la Uviko 19,hali hii ikipunguza msaada wa kibinadaam na kushurutisha mataifa kuwekeza kwenye maswala yanayoenekana muhimu zaidi
Daktari Ahmed Ogwell afisa mkuu mtendaji wa shirika la VillageReach, anashauri kuwa uwekezaji bunifu katika kitengo hiki cha afya ni muhimu.
Dkt Ogwell anapendekeza kuwa wakati huu mataifa yanapokabiliwa na punguzo kwenye ufadhili wa kigeni ni muhimu kwa mataifa kuziba mapengo ya ubadhirifu wa pesa za umma na kuwekeza kwenye miradi ambayo inakubalika kwenye jamii na isiyo ya gharama ya juu.
Hii itahakikisha kuwa mataifa ya Afrika hayawi mataifa tegemezi kwa jamii ya kimataifa ambayo kwa wakati mwingi huwekeza kwenye miradi inayozingatia matakwa yao.
Aidha ili kuhakikisha kuwa huduma za afya kama uchomaji chanjo zinawafikia wanajamii wote ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kuimarisha huduma za wahudumu wa afya wa jamii ili kuhakikisha kuwa chanjo zinawafikia watoto walengwa baadala ya wazazi kupata ugumu wa kwenda kusaka huduma hizo.
H pylori isipotibiwa inaweza kugeuka kuwa saratani ya tumbo ,watalaam wameonya
Katika makala haya,tunaangazia sababu ambazo zinaweza kuchangia mtu kupata maambukizo ya H pylori na matibabu yake.
Matibabu yake kwa mujibu wa daktari Alex Mungala anayehudumu jijini Nairobi yanaweza kukabiliwa na usugu wa vimelea ,ni ghali na si rahisi kupatikana katika vituo vya afya vya daraja la kwanza.
Utafiti uliofanywa wa shirika la utafiti wa afya Lancet Public Health umebaini hatua elfu 7 kila siku unapunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya Saratani,Kisukari,magonjwa ya moyo, shinikizo la damu,sonona na kupoteza kumbu kumbu
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO,mazoezi ya kudumu dakika 150 kila wiki au mazoezi makali ya dakika 75 ni mkakati wa kuimarisha afya.
Katika makala haya nimejiunga na kundi la Nairobi Walk Movement,tawi la Buru Buru ambalo limejitoa kufanya matembezi ya kuanzia kilomita 10 hadi 20 na wakati mwingine hadi 40 kila Jumamosi asubuhi au Jumapili alasiri kuanzia saa tisa na nusu.
Kundi hili pia limejisajili kwenye kundi la kuhesabu hatua ambazo kila mtu hutembea kila siku ,hatua hizo zikihesabiwa kutumia application maalum ya kuhesabu hatua,lengo likiwa hatua hadi elfu 10 kila siku.
Kushindana kwa kuhesabu hatua kila siku umekuwa mchezo ambao huwatia moyo
Wanachama hao wameelezea faida nyingi kutokana na kujiunga kwenye kundi hilo na kushiriki matembezi.
Wapo waliokuwa na wanatumia dawa za kudhibiti shinikizo la damu na sasa wameachana nazo.
Aidha wengine wameeleza matembezi kuwaondolea maumivu ya viungo na pia kupata marafiki wazuri.
Kukaa kwa zaidi ya saa sita mfululizi kila siku inaweza kukuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya uti wa mgongo,kisukari,shinikizo la damu na kifo cha mapema
From the publisher's feed
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners