
Sign up to save your podcasts
Or


Matibabu mengi licha ya kupendekezwa au kuorodheshwa sahihi ,yanakabiliwa na usugu wa vimelea tatizo linalofanya dawa hizo kushindwa kutibu inavyotakikana
Dawa za kutibu Malaria ,TB na Kipindu Pindu zimetajwa kuathirika sana ,haswa dawa aina ya antibiotics ambazo hutumika kuwa matibabu ya kwanza ya kuua vimelea.
Ripoti nyingi huonesha kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaougua magonjwa yaliyotengwa au kusahaulika ni akina mama au watoto
Hii ni kutokana na wao kutangamana moja kwa moja na mazingira ambayo huwa makazi ya vimelea vinavyosababisha magonjwa mbali mbali.
Vimelea hao hukaa mchangani,kwenye maji au hupatikana kwenye kinyesi .
Tafiti zimeonesha kuwa magonjwa mengi ya milipuko haswa barani Afrika yanachochewa na mabadiliko ya tabia nchi
Mafuriko ,ukame au kupanda joto yanaweza kusababisha kusambaa kwa haraka kwa vimelea vinavyosababisha magonjwa au kuzaana kwa haraka.
Sudan Kusini kando na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Kisukari ,upatikanaji wa matibabu bado ni changamoto kubwa
Watalaam nchini humo wanahoji mabadiliko ya mtindo wa maisha kama chanzo cha ongezeko la visa hivi.
WHO inashauri ukanda wa Afrika kuwekeza zaidi katika takwimu zilizo sahihi katika mikakati ya kupambana na magonjwa ya milipuko
Kila mwezi wa Oktoba, ulimwengu huadhimisha Mwezi wa Uhamasishaji wa Saratani ya Matiti, lengo kuu likiwa kuhamasisha vipimo vya mapema ili kupunguza hatari ya ugonjwa huu na kutafuta msaada wa kifedha kwa ajili ya utafiti kuhusu saratani ya matiti.
Inakadiriwa kuwa, wagonjwa wapya zaidi ya milioni 2.3 wa saratani ya matiti hugunduliwa kila mwaka, kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani.
Wengi wa wanawake waliopatwa na saratani hii walilalzimika kukatawa titi moja au yote mawili ili kuokoa maisha yao, na hivyo kupoteza kiungo muhimu cha mwili.
Mafuta ya mzeituni, alizeti, mafuta ya nazi,mafuta ya mawese ni baadhi ya mafuta kula ambayo yanapendekezwa kutokana na namna yanavyotengenezwa. Mengi hutengenezwa kwa kukamuliwa ,bila kuongezwa kemikali bila kutumia joto,hivyo ubora wake ni wa juu.
Mafuta haya hata hivyo ni ya bei juu sana na watalaam wanashauri badala ya kuchagua mafuta ambayo si mazuri na ambayo yanaweza kuongeza mafuta ya Cholesterol mwilini na kusababisha matatizo ya afya ,machaguo mbadala ni mafuta ya uto .
Mafuta haya yanaweza kutokana na mimea au mbegu.
Mfano ni mafuta ya Parachichi,Karanga na hata Canola.
Aidha watalaam wanatoa tahadhari kuwa ukitumia mafuta yako kupika ,usipende kuyarudia au kutumia kwa zaidi ya mara moja na usiyaweke mahali wazi maana yanayoweza kugeuka mabaya bila wewe kufahamu.
Kuanzia yale ya nazi hadi mizeituni, mboga hadi kanola, parachichi hadi mafuta ya wanyama maswali yameibuka kuhusu tunajuaje yapi mazuri ya kutumia, na ikiwa tunapaswa kuepuka yoyote yale kabisa
Watalaam wa afya wanahoji mafuta ni kiungo muhimu katika mwili wa binadaam kwa kuwa huchangia madini muhimu na pia husaidia utendakazi wa viungo muhimu mwilini.
Hata hivyo wanashauri mafuta kutumika kwa kiasi ili kuzuia mwili kujilimbikizia mafuta haswa ya Cholestrol ambayo yanaweza kusababisha mishipa ya kupitisha damu kuziba ,kusababisha saratani,shinikizo la damu na magonjwa ya moyo
Katika orodha ya mafuta,kuna mafuta yanayotokana na mimea ,wanyama na yale yanayozalisha viwandani maarufu kama Trans Fats
Maamuzi ya kutumia mafuta gani ,hata hivyo yanategemea ubora wake ,kazi ya mafuta na mapishi ya mtu
Mafuta ya wanyama japo ni asilia yanapaswa kutumika kwa kiasi kidogo mno .
Mafuta ya uto haswa ya mimea ni mazuri ila yanaweza kuharibika ikiwa utachanganyika na hewa ya oksijeni au yanapotumika kwa kurudiwa rudiwa.
Mwongozo wa shirika la afya duniani,WHO kuhusu usafi,unapendekeza choo kimoja kinaweza kutumika na watu 20 ila katika kisiwa cha Ndeda ndani ya Ziwa Victoria ,watu zaidi ya elfu 2 wanachangia vyoo vitano
Kama kuna kipindi watu wengi huwa tumbo joto, ni kusubiri matokeo ya kipimo cha HIV au magonjwa mengi ya zinaa.Au kuambiwa huna uwezo wa kizazi.
Hata hivyo unapofanya vipimo hivyo itakuokoa kufanya makosa ambayo yanaweza kuathiri familia yako baadaye.
Ikiwa utapima baadhi ya vipimo hivi muhimu utaweza kujipanga kifedha na kuchagua matibabu ambayo yanaweza kutatua changamoto za afya ambazo pengine umekutwa nazo.
From the publisher's feed
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners