Siha Njema

Siha Njema

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Siha Njema episodes

  • Kwenye kapu la sekta ya afya kufuatia kongamano la Africa Forward

    Baadhi ya makubaliano yalitotangazwa na Ufaransa baada ya siku mbili ya kongamano la  Africa Forward ni ufadhili kwa uzalishaji wa dawa na chanjo hapa barani Afrika.

    Shirika la Unitaid  pia lenye ushirikiano na Ufaransa lilitangaza kuratibu mchakato wa kuzalishwa dawa mpya ya kuzuia virusi vya HIV ,Lenacapavir kuzalishwa Afrika Kusini.

    Na kwenye viungo vingine vilivyosheheni majadiliano ya kuimarisha mifumo ya afya Afrika ni kilimo endelevu .

    11 min
  • Watalaam wasisitiza uwekezaji wa utafiti wa DNA barani Afrika

    Utafiti unaoangazia vinasaba katika ukanda wa Afrika unaweza kuwa jawabu kwa ubainishaji potovu,gharama ya juu ya matibabu na usugu wa vimelea .

     Kwa kuanzia , Mashirika matatu ya Afrika ya kitafiti  yametangaza mkataba wa dola milioni 3 nukta 5 ambao utawekezwa  kwenye utafiti  huu wa DNA  barani .

    Mashirika haya yakiwa ni Biolinx Africa,  YTO Foundation  yenye makao Ivory Coast na  Nextgen Molecular Lab nchini Kenya.

    10 min
  • Mpango wa kuongeza ujuzi wa wahudumu wa afya kwa kutumia teknolojia

    Ufadhili wa afya ukanda wa Afrika umezidi kupungua tangu kusitishwa kwa ufadhili mkubwa wa kigeni

    Pengo hilo linamanisha serikali nyingi hazina uwezo wa kifedha wa kutosha kuendelea kutoa mafunzo endelevu ya wahudumu wa afya.

    Katika kujaribu kutatua changamoto hii ,mpango wa ECHO unaowasaidia wahudumu wa afya kujifunza wakati wanapoendelea kuwahudumia wagonjwa ,umekuja kuleta matumaini.

    11 min
  • Mataifa ya Afrika mbioni kuboresha mkataba wa kupambana na majanga

    WHO ilitoa nafasi zaidi kwa mataifa ya ulimwengu kujadililiana zaidi kuhusu vipengee muhimu kwenye mkataba wa kukabiliana na majanga ya kidunia

    Vipengee hivyo ni pamoja namna mataifa yanaweza kunufaika kutokana na mchango wao kwenye tafiti za kisayansi ,vimelea vinavyotoka kwenye mataifa yao na usawa wakati wa usambazaji wa chanjo au dawa

    11 min
  • Miaka mitatu tangu Sudan kuingia kwenye mzozo huduma za afya zimedorora

    Asilimia 37 ya vituo vya afya nchini Sudan vimeharibiwa wakati wa mapigano na haviwezi kutoa huduma za afya

    Shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF limekuwa likiwahudumia wagonjwa wenye majeraha ,waathiriwa wa magonjwa ya milipuko na waathiriwa wa ubakaji.

    Hali ya usalama imeilazimu  MSF kusitisha huduma katika maeneo kadhaa baada ya kushuhudiwa mashambulizi ya moja kwa moja kwenye vituo vya afya ,vituo hivyo kuporwa na uhaba wa bidhaa za kimatibabu unaohusishwa na vikwazo vya usafiri.

    10 min
  • Magonjwa ya Autoimune yana uwezo kukusababishia magonjwa mengine zaidi

    Magonjwa yanayoshambulia kinga yanapompata mtu ,huendelea kusambaa ,kudhuru kingamwili na  kumweka hatarini mgonjwa kiasi cha kuwa mgonjwa anaweza kupatwa na magonjwa zaidi ya moja ya aina hiyo.

    Elwyn Chebet aligunduliwa na Lupus na baadaye akajikuta anapambana na magonjwa zaidi ya tano aina ya Autoimmune.

    Mwezi Machi ambapo ulimwengu huelekeza kurunzi kwenye magonjwa ya mfumo wa kinga au Autoimmune,watalaam wanasikitika kuhusu ufahamu mdogo kuhusu magonjwa haya.

    Wagonjwa wengi huwa na dalili za kukanganya na ubainishaji wa magonjwa haya unaweza kuchukua muda mrefu na kugharimu kiasi kikubwa cha pesa.

    Na kwa kuwa vyanzo vya magonjwa haya huwa haviko wazi matibabu yake huwa yenye mtihani mkubwa.Watalaam wengi hujaribu kutibu dalili bila kushughulikia chanzo cha ugonjwa wenyewe.

    Katika makala haya tumezungumza na Elwyn Chebet ambaye ni shujaa na mwanaharakati wa ugonjwa wa Lupus ambao huathiri viungo kadhaa mwilini na hata ngozi.

    Katika simulizi yake ,anaeleza kuwa kutokana na kinga dhaifu magonjwa tegemezi kama mafua,Malaria na Menegitisi yanaweza kuhatarisha maisha yake hivyo huhitajika kupata chanzo ya mapema dhidi ya magonjwa haya.

    11 min

About Siha Njema

From the publisher's feed

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu…

More shows like Siha Njema

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners