Siha Njema

Siha Njema

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Siha Njema episodes

  • Kwa nini watalaam wanahoji maumivu makali wakati wa hedhi si kawaida

    Maumivu wakati msichana au mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, yanaweza kuwa ya kawaida ila maumivu haya yanapomfanya kushindwa na shughuli za kawaida si kawaida

    Dkt Dominic Osiemo anasema maumivu haya makali yanaweza kuwa dalili za baadhi ya changamoto za kiafya kama vile Uvimbe au ugonjwa wa Endometriosis.

    10 min
  • Changamoto ya wanaume na wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa

    Raia mmoja wa Kenya amefika kwenye bunge la kitaifa nchini Kenya akitaka swala la wanaume na wanawake kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa kuorodheshwa kuwa ulemavu

    Kwa mujibu wa daktari Dominic Osiemo ,tatizo hilo linachangiwa na maswala kadhaa yakiwemo matumizi ya dawa za kisukari ,shinikizo la damu na msongo wa mawazo.

    11 min
  • Visa vya kung'atwa na Nyoka vyaongezeka kaunti ya Turkana Nchini Kenya

    Kaunti ya Turkana inaongoza nchini Kenya kwa visa vya watu kung'atwa na nyoka. Wataalamu wa afya wanasema mabadiliko ya tabianchi, joto kali na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya vinaongeza hatari kwa wakazi wa maeneo mengi ya kaunti hiyo,huku shirika la afya duniani WHO likisema visa vya kuumwa na nyoka vinapuuzwa wakati huu karibia watu 32000 wakifariki kila mwaka  kutokana na sumu ya nyoka.Katika makala haya ya siha njema tunaangazia kijiji cha Kapua kwenye kaunti hiyo .

    10 min
  • Mashirika ya kiraia Afrika yaanza kampeni dhidi ya madeni ya umma

    Mashirika ya kiraia yanasema nchi za Afrika zinalipa deni na kuachwa  na kiasi kidogo cha pesa kuendesha shughuli muhimu za serikali ,sekta ya afya ikiathirika zaidi

    Mashirika haya yanataka umoja wa Afrika kuja na jopo ambalo litakuwa linaangazia  maswala yote kuhusu mikopo ili kupunguza dhulma kwa nchi zinazoendelea

    11 min
  • Kampeni kuhakikisha vyakula vilivyosindikwa vina maandishi ya kuonya

    Tafiti kadhaa za kiafya zimebainisha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yana uhusiano mkubwa na vyakula vilivyosindikwa  na hali ya watu kukosa kuzingatia mazoezi  ya kila mara.

    Kenya ikiwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kupitisha  mwongozo unaotoa maelekezo kuhusu viwango vya  madini ambavyo  vyakula au vinywaji  vinavyouzwa vinafaa kukidhii  au kwa lugha ya kiingereza Kenya Nutrient Profile Model,sasa ipo mbioni kuja na sheria kushinikiza maandishi ya kuonya kuhusu vyakula venye mafuta ,sukari na chumvi nyingi kupachikwa kwenye bidhaa za vyakula na vinywaji

    10 min
  • Kwa nini ni muhimu wanaume kuzingatia afya zao haswa afya ya akili

    Mwezi Juni ni mwezi wa kutoa uhamasisho kuhusu afya ya akili miongoni mwa wanaume ,swala la afya ambalo hupuuzwa mno

    Daktari Dominic Osiemo anasema wanaume wana haki wa kuonesha hisia ,kueleza maumivu  yao na kutaka kuskizwa. Na wanapofanya hivyo wanalinda afya zao za akili.

    Anaonya wanaume wengi wanakuwa hatarini kwa sababu wanajaribu kudhihirishia jamii kuwa wao ni imara siku zote.

    Baadhi ya vipimo muhimu kwa wanaume ni kipimo cha kiwango cha sukari ,kipimo cha tezi dume na shinikizo la damu.

    10 min
  • Shinikizo kutaka mataifa kuja na sera endelevu na salama za uchukuzi

    Shinikizo zinazidi kutolewa kwa mataifa ya Afrika kukumbatia sera za uchukuzi zilizo salama na endelevu ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na barabara na madhara ya ajali za barabara kwa jamii.

    Katika  kongamano la kujadili mpango huo wa usalama ulio endelevu ,wadau wamesikitika vifo vya barabarani bado vinaripotiwa miongoni mwa watembea miguu na waendesha pikipiki.

    Katika makala ya Siha Njema wiki hii tunajadili kwa nini swala hili ni muhimu kwa ustawi wa jamii.

    10 min
  • Majanga yanaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa watoto

    Mataifa ya Afrika yameshuhudia mafuriko katika miaka ya hivi karibuni ,hali ambayo imesababisha wananchi wengi kulazimika kuhama makazi yao

    Nchini Kenya ,ukanda wa magharibi ,katika eneo la Busia,mafuriko hayo yamevuruga kalenda za wanafunzi wa shule ,watoto wengi wakishindwa kuendelea na shule au kukubaliana na msongamano kwenye shule chache ambazo ziko maeneo salama

    Hali hii imewasababisha changamoto za afya ya akili anavyoeleza mwaandishi wetu Petronila Ogalo.

    10 min

About Siha Njema

From the publisher's feed

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu…

More shows like Siha Njema

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners