Siha Njema

Siha Njema

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Siha Njema episodes

  • Nini magonjwa yanayoathiri kinga mwili au Autoimmune

    Unapopata magonjwa ambayo yanaathiri kinga ya mwili wako,ina maana kuwa kinga yako inaweka mifumo yote ya mwili kwenye hatari. Unaweza kujikuta unapata magonjwa kama Lupus,ugonjwa wa Tezi Koo au Mifupo yako kuwa nyepesi kiasi cha kuvunjika kwa urahisi.

    Ubainishaji wa magonjwa haya unahitaji subira na ufuatialiaji wa karibu ili kuelewa kila dalili anayoonesha mgonjwa .Gharama yake basi inamanisha ni ya juu na huhitaji muda mrefu.

    11 min
  • Madhara ya afya ya akili yanayotokana na matumizi ya kupitiliza ya simu

    Ripoti ya afya akili  duniani ,inaonya kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya simu za mkononi miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 34

    Katika mataifa ya Afrika ambapo matumizi ya simu hizi huanza kwa kuchelewa ,vijana walionekana kuwa afadhali ikilinganishwa na mataifa kama Finland ambapo watoto huanza kutumia simu katika umri mdogo mno.

     

    Katika mataifa yaliyozingatia maswala ya dini na muunganiko wa familia na jamii walionekana pia kuwa na ahueni.

    11 min
  • Kupambana na ugonjwa wa mbwa kichaa Nairobi kwa kuzingatia maslahi ya mbwa

    Mamlaka jijini Nairobi zimefanya operesheni kudhibiti ongezeko la mbwa mtaa katika mkakati wa kupambana na ugonjwa wa mbwa kichaa

    Mbwa japo anasemekana kuwa rafiki wa karibu na mwaminifu unapomfuga ,matunzo yasiyofaa au kuwatelekeza unaweza kukuweka karibu na ugonjwa wa mbwa kichaa

    Ukiwa utamfuga mbwa ,sharti kuzingatia usafi na chanjo ya kila mwaka dhidi ya ugonjwa wa mbwa kichaa

    11 min
  • Kwa nini kuna umuhimu wa kutumia dawa za minyoo baada ya miezi sita

     Shirika la afya duniani ,WHO hupendekeza matumizi ya dawa za minyoo kwa watoto kati ya mwaka moja hadi 12 ,vijana wenye umri kati ya 13- 19 ,wanawake walio kwenye umri wa kupata watoto na watu wanaoishi katika maeneo yenye minyoo. Hii ni njia mojawapo ya kupambana na utapiamlo, Anamia na matatizo yanayoletwa na minyoo.

    10 min
  • Kufunga saum inafaidi afya yako vile vile nafsi yako ikiwa utafanya mara kwa mara

    Kuna ushahidi unaoonesha kwamba kufunga kunaweza kusaidia kurekebisha miili yetu ,wakati mwingine kuongeza maisha yetu, pia  njia bora ya kupunguza uzito,

     

    Kitendo cha kukumbatia  Saum huchochea usafi wa moyo, nafsi na kusafisha mwili wako kwa kuondoa chakula ambacho mara nyingine hugeuka kuma sumu mwilini na chanzo cha magonjwa yasiyoambukiza.

     

     

    Wataalam wa afya  pamoja na watetezi wa kufunga wanasema kuna uhusiano mkubwa kati ya afya ya kimwili na afya ya kiroho.

     

    Kwenye makala hayo ya Siha Njema  tunakupa ufafanuzi huu tukisaidiwa na daktari  Julius Maleve na pia kiongozi wa kidini  Mtume Julius Suubi ,ambaye ameandika kitabu kuhusu faida za kufunga na ambaye amekuwa akifunga kwa kati ya siku 40 hadi 90 kila mwaka kwa zaidi ya mwaka 20 sasa.

    11 min
  • Juhudi za wazee kukomesha ukeketaji wa wasichana kaskazini mwa Kenya

    Ukeketaji wa wasichana bado ni changamoto kubwa katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Kenya, licha ya marufuku ya kitaifa na juhudi za uhamasishaji zinazoendelea. Takwimu za Kitaifa KNBS na  zile Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 83 ya wanawake na wasichana wa Marsabit na 66 wa Isiolo tayari wamekeketwa—ikiziweka kaunti hizi miongoni mwa maeneo yenye viwango vya juu zaidi nchini.Sasa wazee maeneo hayo wameanza mchakato kukabiliana na ukeketaji huo

    11 min
  • Je una uhakika wa usalama wa nyama unayoila kila mara nyumbani?

    Watalaam wa wanyama wanasisitiza wanyama wote wanaochinjwa ni sharti kutimiza viwango vya juu ikiwemo mwonekano ,afya  na usafi.

    Na kabla kuchinjwa wanyama hao kwa mfano ngombe ,hukaguliwa na kutengwa ili kubainisha nyama yao ni salama.

    Kwa mlaji unashauriwa kununua nyama iliyo na muhuri ambayo ni alama ya kuonesha nyama hiyo imekaguliwa na kuthibitishwa ni salama.

    Kwa wale wanaochinjia nyumbani bado unatakiwa kumpata mtalaam wa wanyama kumkagua mnyama wako na kutoa kibali cha kuchinjwa.

    11 min

About Siha Njema

From the publisher's feed

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu…

More shows like Siha Njema

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners