
Sign up to save your podcasts
Or


Shaba yetu leoinalenga nchini Kenya ambapo Vijana wameanza kuandamana kupinga kile wanadai wanasiasa kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwenye maeneo ya kuabudu ili hali wao hawana ajira.
Tumekuuliza hatua hii ni sahihi?
Haya hapa baadhi ya maoni yako.
Mwishoni mwa juma lililopita rais wa Kenya William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walitiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kisiasa, wanaosema utasaidia kutatua changamoto zinazowakabili raia wa taifa hilo.
Unaamini makubaliano ya viongozi hawa ni sahihi?
Ndilo swali tumekuuliza na haya hapa maoni yako.
Nchini Gabon, kiongozi wa kijeshi jenerali Brice Oligui Nguema ametangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwezi ujao, baada ya kutwaa madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi ya 2023.
Hili linajiri wakati huu viongozi wengine wa kijeshi kwenye nchi za Burkina Faso, Mali na Niger wakielekea kuchukua mkondo huo.
Leo ni Ijumaa ,,siku ya mada huru kwenye habari rafiki ambapo Tunakupa nafasi ya kuzungumzia suala lolote ambalo limetokea nchini mwako wiki hii au kile ambacho umekisikia kwenye matangazo yetu ya juma hili
Mada ni kuhusu..kauli ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni Akiwa katika ziara ya kawaida kuzungumza na raia wake , ameeleza kuguswa na kusikitishwa na hali ya umasikini anayoshuhudia kwenye nchi yake,,,wakati huu tatizo la umasikini linashuhudiwa pia kwenye mataifa mengine ya ukanda.Tulimuuliza mskilizaji anazungumziaje kauli ya Rais Museveni na je viongozi wa ukanda wamefanya vyakutosha kupambana na umasikini?
Karibu kwenye kipindi cha leo ambapo tunaangazia tangazo la Rais wa DRC, Felix Tschsekedi, kuwa ataunda Serikali ya umoja wa kitaifa, hatua inayokuja wakati huu akiwa katika shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi yake, kuhusu namna alivyoshughulikia mzozo wa mashariki mwa nchi yake, wakati huu waasi wa M23 wakichukua miji zaidi.
Ikiwa ni siku ya Ijumaa, ni wakati wa mada huru, yaani tunampatia mskilizaji nafasi kuchangia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii hapa RFI Kiswahili au kutueleza jambo ambalo limetokea nchini mwake juma hili.
Leo pia msikilizaji ni siku ya lugha mama, ningependa sana nikusalimie kwa lugha yako mama lakini ningependa kusikia kutoka kwako kwanza. Jambo!
Haya ni makala ya Habari Rafiki tukiangazia maoni ya waskilizaji wa RFI Kiswahili kuhusu mada kwamba, Marekani imeanza mazungumzo na Urusi, lengo likiwa kupata mkataba wa kusitisha vita nchini Ukraine.
Ukraine ambayo haijashirikishwa kwenye mchakato huo inasema haitakubali mkataba wowote bila kuhusishwa.
Tumemuuliza msikilizaji je, Marekani inaweza kumaliza vita vya Ukraine? Na anafikiri ni kwanini Marekani haijaishirikisha Ukraine na mataifa ya Ulaya kwenye harakati hizi?
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners