
Sign up to save your podcasts
Or


Ukanda wa Afrika unazidi kushuhudia ongezeko la migogoro huku viongozi wakisisitiza Afrika ina majibu ya mizozo hiyo
Mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya DRC yanayoendelea na sasa yamefika jimboni Kivu Kusini,Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinadamu OCHA ikisema maelfu ya watu wameendelea kukimbia makaazi yao.Kwenye makala haya tumemuuliza msikilizaji nani wa kulaumiwa kuhusu vita hivi vinavyoendelea? na anafikiri ni kwanini imekuwa vigumu kupata suluhu?
Visa vya uchimbaji wa madini haramu vimeongezeka katika nchi mbalimbali barani Afrika .Afrika Kusini ikiwa mfano wa nchi hizo ambayo imeshuhudia miili ya wachimba midogo zaidi ya 70 ikipatikana katika mgodi wa dhahabu usiokuwa rasmi.
Kwenye kipindi cha leo tumemuuliza msikilizaji anafkiri nchi za Afrika zimeshindwa kudhibiti uchimbaji haramu wa madini ? na nini kinaweza kufanyika kuzuia uchimbaji huo haramu ?
Kwenye kipindi cha leo tunaangazia kurejea afisini kwa rais wa Marekani Donald Trump baada ya kuapishwa kama rais na kuahidi nchi mpya.Tumemuuliza msikilizaji dunia itarajie nini kutoka kwa uongozi Wake na je Waafrika wana matumaini gani kuhusu kuongozi wake Trumpµ?
Makala ya habari rafiki imewashirikisha wasikilizaji kutoka kila kona ambapo wasikilizaji wametoa maoni yao kuhusu namna ambavyo wataalamu wa afya kutoka nchi za jumuia ya Afrika Mashariki walivyojadiliana kuhusu utaratibu wa kupata vibali kwenye nchi hizo bila ya kusumbuliwa. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi.
Kila siku ya Ijumaa ni Mada huru ambapo tunakupa nafasi msikilizaji kuchangia suala lolote ambalo limetokea nchini mwake au kile ambacho amekisikia katika matangazo yetu ya wiki hii.
Katika salamu zao za mwaka mpya, viongozi karibu wote wa ukanda wa Afrika Mashariki, wametoa wito wa umoja na amani, huku kwa mataifa yenye utovu wa usalama, viongozi wakiahidi kirejesha utulivu.Tulimuuliza mskilizaji iwapo kiongozi wa nchi yake atabadili mambo mwaka huu wa 2025
Mataifa mbalimbali duniani wakiwemo raia wa ukanda wa Afrika Mashariki, wamesherehekea mwaka mpya wa 2025 kwa kila aina ya mbwembwe na shamrashamra, kukiwa na hisia mseto za matumaini tofauti na mwaka uliopita.Tulimuuliza mskilizaji atueleze aliukaribisha mwaka mpya vipi na akiwa wapi,vile vile angependa kuona kipi kinabadilika kwenye nchi yake.
Nchini Kenya mjadala mkali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii unaendelea, ambapo baadhi wamekuwa wakiitumia kuikosoa Serikali na rais William Ruto, kwa kiwango ambacho wengine wanasema wakosoaji wamevuka mipaka huku baadhi wakisema watu wako huru kukosoa wanavyotaka.Tulimuuliwa mskilizaji je anaamini iwapo vijana wamevuka mipaka au la.
Baraza la usalama la umoja wa Mataifa, mwishoni mwa juma limepitisha azimio kuunga mkono uundwaji wa kikosi kipya cha bara Afrika cha kulinda amani nchini Somalia, kikosi hiki kikichukua nafasi ya kile cha ATMIS na kitakuwa na jukumu la kuwakabili wanamgambo wa Al-Shabaab.Tumemuliza msikilizaji iwapo anaamini kikosi hiki kipya kitafanikiwa kuleta amani nchini Somalia
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners