
Sign up to save your podcasts
Or


Tunakupa nafasi ya kuzungumzia tukio lolote lililotokea duniani wiki hii. Tunakutakia sikukuu njema na maandalizi mema ya kuupokea mwaka wa 2025
Serikali ya Morocco imependekeza marekebisho ya sheria kuwaruhusu wanawake kurithi mali, umri wa kuolewa kuongezwa kutoka 17 hadi 18 na kuwekwa kwa masharti kwa wanaume wanaotaka kuoa mwanamke zaidi ya mmoja.Tunamuuliza msikilizaji maoni yake kuhusu mapendekezo hayo na hali iko vipi nchini mwake kuhusu wanawake urithi mali
Mamia ya wasafiri wanaoelekea maeneo mbalimbali kwa sherehe za Krismasi wamekwama barabarani nchini Kenya kutokana na msongamano mkubwa wa magari na wengine kukosa magari ya usafiri wa umma.
Tunamuuliza msikilizaji nini kinasababisha kuongezeka kwa safari msimu wa sikukuu na nchini mwao hali ikoje.
Kwa mara ya kwanza katika historia yake, Somalia itaongoza Kikosi cha Kudumu cha Afrika Mashariki (EASF) ambacho kimetwikwa jukumu la kuimarisha amani na usalama katika eneo hilo baada ya kuchukua uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Ulinzi wa jumuiya hiyo kutoka nchi ya Rwanda katika hafla iliyofanyika jijini Kigali hapo jana.
Tunamuuliza msikilizaji maoni yake ni yepi kuhusiana na hatua hii.
RFI Kiswahili kila siku ya Ijumaa inakupa nafasi ewe msikilizaji wetu kuchangia mada yeyote uliyoiskia kwenye habari zetu au kile kinachoendelea hapo ulipo.
Haya ndio maoni ya waskilizaji wetu juma hili.
Wasikilizaji watoa maoni kuhusu hatua ya Mahakama moja nchini Kenya, kuamuru kwamba msichana wa umri wa miaka 16 anayekiri kushiriki ngono na mwanaume si thibitisho la unyanyasaji wa kigono, uamuzi ambao umeibua hisia kali nchini Kenya.
Hujambo karibu katika makala ya Habari Rafiki ambapo wasikilizaji walizungumzia tangazo la Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Edorgan,kuwa atazuru Ethiopia na Somalia mwakani, baada ya kupatanisha mataifa hayo mawili kufuatia mzozo wa bandari ya Somaliland.
Hapa wasikilizaji wamezungumzia mkutano kati ya viongozi wa Rwanda na DRC kule Angola wikendi hii, pia vijana kujituma ili kufanya kazi kujikimu kimaisha
Hujambo na karibu kwenye makala ya habari rafiki, leo tunajadili kufuzu kwa mataifa ya Tanzania Uganda na DRCongo , kucheza kwenye mchuano ya kuwania AFCON, mataifa haya yakiwakilisha Afrika Mashariki nchini Morroco mwaka ujao.
Je unazungumziaje kufuzu kwa mataifa haya?
Haya hapa baadhi ya maoni.
Katika makala tunajadili hatua ya viongozi wa dini nchini Kenya, kutuhumu serikali kwa kile wamedai imekuwa ikitoa ahadi za uongo kwa raia.
Je unazungumziaje kauli hii ya viongozi wa dini nchini Kenya?
Haya hapa maoni yako.
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners