
Sign up to save your podcasts
Or


Wanamgambo wa RSF wanaopigana na jeshi nchini Sudan na washirika wake wakiwemo wanasiasa wapo jijini Nairobi nchini Kenya, wanakojadiliana kuhusu uundwaji wa serikali mbadala wakati huu inapoendelea na vita.
Unazungumzia vipi harakati hizi za RSF ?
Unafikiri ni kwanini Kenya imewaruhusu wanamgambo hao kukutana katika nchi yake ?
Makala ya leo yanaangazia Kikao cha viongozi wa Afrika, kilichotamatika rasmi mwishoni mwa juma lililopita nchini Ethiopia, mzozo wa DRC na Sudan ukigubika mijadala yao.
Hata hivyo vikao hivyo vimekamilika bila suluhu ya mizozo ya nchi zote mbili, ambapo vyongozi waliishia kwa kutoa wito wa kusitisha mapigano. tulimuuliza msikilizaji iwapo anaridhika na matokeo ya kikao hicho na anadhani nini cha zaidi viongozi hawa wangefanya kukomesha mizozo barani Afrika
Mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa Afrika umeanza rasmi jijini Addis Ababa, #Ethiopia ambapo maswala muhimu ikiwemo usalama mashariki mwa #DRC, mapinduzi ya kijeshi na vita dhidi ya makundi ya kijihadi yakitarajiwa kugubika mkutano huu.Tulimuuliza mskilizaji natarajia nini kipya kutoka kwa viongozi wa AU? na iwapo anafikiri viongozi wameshindwa kumaliza changamoto za bara hili..
Kwenye kipindi cha leo tunaangazia kauli tata ya Rais Donald #trump, kuhusu mzozo wa #Gaza, safari hii akitishia kuvunjika kwa mkataba wa usitishaji mapigano, ikiwa Hamas haitawaachia mateka wote ifikapo Jumamosi ya wiki hii.Juma lililopita alidai kuwa nchi yake itachukua udhibiti wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina.Tulimuuliza mskilizaji anazungumziaje kauli hiyo ya Trump and je huenda zikachochea mzozo zaidi kati ya #Israel na Hamas?
Makala haya yanaangazia hatua ya Serikali ya kenya kusema hakutakuwa na haja ya mahojiano kwa waomba vitambulisho toka katika maeneo ya mpakani, uamuzi ambao umeibua mjadala kuhusu masuala ya usalama.Tulimuuliza msikilizaji anazungumziaje hatua hiyo ya Kenya vile vile nchini mwake hali ikoje
kwenye makala ya leo tunaangazia hatua ya wakuu wa nchi za #SADC na EAC kutaka kusitishwa mapigano maramoja ,na kutaka kuondoka kwa vikosi vya kigeni mashariki mwa #DRC, pamoja na Serikali ya Kinshasa kuzungumza moja kwa moja na waasi wa #M23 ambapo wito huo umepokelewa kwa hisia mseto na raia wa ukanda.
Kila siku ya ijumaa ni mada huru ambapo Tunampa nafasi msikilizaji kujadili suala lolote ambalo limetokea nchini mwake wiki hii au kile ambacho amekisikiliza kwenye habari zetu juma hili.
Wakuu wa nchi za Afrika walikutana juma hili nchini Tanzania ambapo walijadiliana kuhusu changamoto za upatikanaji wa Nishati ya Uhakika katika mataifa hayo.
Licha ya rasilimali za bara la Afrika bado hakuna nishati ya uhakika na endelevu? Bonyeza uskilize maoni mbalimbali.
Uamuzi wa Rais wa Marekani #DonaldTrump, kuagiza kusitishwa kwa muda utowaji wa misaada yote ya kigeni umeibua mjadala na sintofahamu hasa kwa nchi za Afrika, ambazo sekta muhimu ikiwemo afya zinategemea msaada wa Marekani.Tulimuuliwa msikilizaji anazungumziaje hatua hii ya Marekani na Nchi za Afrika zifanye nini kuacha kutegemea misaada ya nchi za Kigeni?
Mizozo inayosibu ukanda wa Afrika ya Mashariki inaendelea kuongezeka, ikiwemo Sudan Kusini na sasa DRC. Viongozi wa Afrika wanasisitiza matatizo ya Afrika sharti kutatuliwa kwa suluhu kutoka Afrika. Je hili linawezekana?
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners