Watafiti tofauti wanasema kwamba kujitambua, na maisha tuliopitia zamani yana mchango mkubwa katika mitazamo yetu.
Ni mara nyingi huwa tunajisikia kama hatuna nguvu ya kubadilisha mambo mengi katika maisha yetu na hii inakua kikwazo kikubwa sana kwa vijana wengi nchini Tanzania, lakini ukweli ni kwamba mtazamo wetu unaweza kutusaidia kufikia mafanikio makubwa.
Kwenye episode hii, nimeungana na Bw. Spencer Minja, ambae ni mwanafunzi na Raisi wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es Salaam, tukijadili jinsi mtazamo wetu unavyoweza kutusaidia kutuinua, kuturudisha nyuma kimaendeleo, au kuathiri afya yetu ya akili.
Jiunge nasi ujifunze jinsi ya kujenga mtazamo chanya na kwa namna gani itasaidia kukufanya wewe kama mtoto, kijana, au mzee kuwa na maisha yenye ustawi bora.